Kununua gari toka Zanzibar

Kununua gari toka Zanzibar

Mwonekano wa Xtrail unavutia sana lakini kumbe ni kama Honda CR-V ukinunua jiandae kufugia sungura
Honda ndio sio gari kabisa, watu walizikurupukiaga CR-V zilivyotoka new model zikaanza kuwafia vibaya mno. Watu hawana hamu nazo kabisa.
 
Boss! Nimeipenda hiyo umeongea kisomi sana. Kuna rafiki yangu alinunua extrail bush tu zikaisha kununua ilikuwa majanga. Wakati za noa au ist ni 20 to 50.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaosifia hizo Nissan ujue hayajawakumba mazito. Kubadilisha engine oil, plug na matairi sio complicated sana. Kimbembe gari ilete technical failure na jinsi nissan ilivyo na umeme na ma sensor kila mahali ndio hapo mtu atapoelewa somo. Nissan ni gari nzuri kwa wenye residual income sio watu wa kudunduliza hela.

Tulikuwa na Nissan Terrano ikaleta shida ya suspension halafu ni zile za upepo electronically controlled, picha linaanza inatakiwa uzinunue kwa pair. Mbona ilikuwa kimbembe aisee. Hela iliotumika kui service ilikuwa ni mishahara ya miezi kadhaa ya watoa comment humu. Nikajiuliza tu je ingekuwaje hii gari anaimiliki mtu kama Mwalimu wa sekondari au bank teller?
 
Asante sana mkuu. Paper work sina shaka nayo. Nina wasiwasi na gharama za TRA. Isijenigharimu zaidi. Kwani Dar zipo nyingi ila naangalia ahuweni ya gharama.
Mwambie mje kuuziana ikishafika Dar. Kuwa mjanja saa mbaya
 
Sawa inategemea na kipato ndg.nawewe unatumia mazingira gani off road au?
You are right, mie nashangaa sana watu wamejenga mentality kwamba X trail si gari nzuri, sijapata sababu zao kwa undani. Ila kwa maoni yangu, ni gari nzuri tena imara,kama ulivyosema ukizingatia vigezo na masharti yake(wengi tunapenda short cuts). Mimi nimeitumia X trail ya 2005 tena sikuagiza bali nilinunua kwa mtu yapata miaka mitatu iliyopita, ila sijaona tatizo lake kubwa ambalo linaweza kunifanya nione haifai. Zingatia service na recommended oil (both engine na gear box), gari yako itadumu sana. Gari ina nafasi, ipo juu, four wheel nk. Nafikiri tusimtie woga mwenzetu, tumpe tu ushauri kuhusu kodi kama alivyoomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Semawew mkulu wengine tunaambiwa mara mafundi garage oooh hatujamiliki hata bajaji hahaha.
Xtrail sio gari inayofaa kwa mtu wa kipato cha chini au kati kwani ni gharama sana kuitunza hasa pale inapohitaji spare, mfano nenda dukani Kariakoo ulizia lens yake ya taa za nyuma au power window halafu ulizia gari nyingine kama Rav 4 au Noah hapo utajua naongelea nini na kumbuka gari hii ili idumu inataka spare mpya na genuine, pia jaribu kupita kwenye magereji uione Xtrail iliyogongwa utagundua kuwa robo ya bodi ni karatasi au kwa maana nyingine huwezi nyoosha labda uite fundi viatu ashonee na uzi au uagize piece mpya, na kama kawaida ya Nissan mafundi mtaani wanaozifahamu ni wachache...kwa taarifa yako gari hizi wengi wamezipaki ndani na kuhakikisha hicho kitu tangaza kuwa unatafuta Xtrail kutoka bara uone watakavyokugombania, mkuu kabla ya biashara hiyo kumbuka majuto ni mjukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu yuko Zanzibar anataka kuniuzia gari. Na gari nikiangalia iko vizuri tu. Xtrail ya 2005 ananipa kwa mil 6. Ila sasa nasikia kuleta gari Bara toka Zanzibar unalipia tena ushuru. Je hiyo ni kweli?. Na kama ni kweli, kwa gari kama hiyo yaweza garimu kiasi gani mpaka naiendesha huku Tz Bara. Anayejua au aliyewahi kununua gari toka Zanzibar naomba ushauri.
Kabla ya kununua nenda na documents za gari TRA Znz watakupa gharama unazotakiwa kulipia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
XTRAIL ni nzuri kama mtunzaji lakini hiyo sita mbona unapata hata hapa DSM .
 
Na ukute mbuzi kapona teh teh.
sio Gari kabisa hiyo
nimemuona mwanajeshi mmoja hapa Ihumwa Dom alimpitia mbuzi gari yake ikachanika mudguard ya mbele ikachanika tukaona kitu km karatasi au katani hivi (asbestos) haijaunganika hadi leo hata kwa puty au plasta
hizo si gari bodi yake haina uimara na kinga km moto au kubondeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Honda ndio sio gari kabisa, watu walizikurupukiaga CR-V zilivyotoka new model zikaanza kuwafia vibaya mno. Watu hawana hamu nazo kabisa.
Honda CR-V sijui watu wanazipendea nini. Labda ubadilishe engine iwe 1MZ
 
Nilinunua gari Zanzibar na nilichofanya nilienda na Document TRA ya Zanzibar kujua kiasi ambacho kililipiwa wakati inaingia Gari hiyo Zanzibar ,baada ya hapo nakaenda TRA ya Bongo wakatipa Amount kamili na tofauti yake ilikuwa million moja tu ambayo nilipaswa kulipia, maana Zanzibar kodi yao IPO chini ukilinganisha na TZ bara.

Ikawa hivi sasa:
Ongezeko la kodi 1,000,000
Kusafirisha gari 300,000 - 350 ,000
Clearence 500,000 inategemea na Agent

Gari ikawa mkononi ila sijui kwa sasa mambo yakoje zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

ilikua gar gani mkuu na ilitumika mda gan zanzibar!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wanaosifia hizo Nissan ujue hayajawakumba mazito. Kubadilisha engine oil, plug na matairi sio complicated sana. Kimbembe gari ilete technical failure na jinsi nissan ilivyo na umeme na ma sensor kila mahali ndio hapo mtu atapoelewa somo. Nissan ni gari nzuri kwa wenye residual income sio watu wa kudunduliza hela.

Tulikuwa na Nissan Terrano ikaleta shida ya suspension halafu ni zile za upepo electronically controlled, picha linaanza inatakiwa uzinunue kwa pair. Mbona ilikuwa kimbembe aisee. Hela iliotumika kui service ilikuwa ni mishahara ya miezi kadhaa ya watoa comment humu. Nikajiuliza tu je ingekuwaje hii gari anaimiliki mtu kama Mwalimu wa sekondari au bank teller?
Nissan ni kizungu zungu asee. Mi ninayo Fuga naendesha pale ninapotaka Show-off (kwenye sherehe au ninapoenda kung'oa demu mpya) vinginevyo nakwea daladala
 
Hivi kaka kufungua website ya TRA nayo ni kazi kuipata... www.tra.go.tz? ukiingia huko utapata kila kitu
Sawa Mkuu, Kama website ya TRA Ipo basi hata Ya Nissan Ipo, Usingemjibu hata Hiyo ungeweka Website, Mbona Ukaelezea kwa Kina hali Ukijua anaweza pata kwenye Website??

Haya Mambo ni kuelekezana tu ndugu yangu, tena kwa Upole.
 
Nissan ni kizungu zungu asee. Mi ninayo Fuga naendesha pale ninapotaka Show-off (kwenye sherehe au ninapoenda kung'oa demu mpya) vinginevyo nakwea daladala
Hahahahaaa! Asante kwa kunichekesha bure. Maana nsikia kuna watu wanalipaga kiingilio kwenda kucheka.
 
Back
Top Bottom