Umenikumbusha mbali mkuu, Kuna manzi nilomchukua one night(hatukuelewana Bei). Nilikuwa na pesa ya watu 25M kwenye begi.
Kumbe usiku nilivyolala alinikagua akaziona zile pesa Ila hakutoa hata mia. Asubuhi nikampa 50k akasema nimuongeze hela nikaanza kulialia njaa kwamba Sina kitu.
Akacheka Sana akaniambia "mkiibiwa mnaanza kulialia, kwenye begi umejaza mihela na usiku umelala Kama umekufa nimekagua mpaka na nguo nimetoa zote nje then nikarudishia. Ningeamua kuondoka si ningeenda kufungua hata biashara huko mbele kwa mbele".
Asee nilitoa jasho Kama nusu ndoo nadhani, ilibidi nimpe 300k Kama zawadi nje ya ile 50k.