Kununua Pikipiki 3M, kumpa Boda kwa mkataba, Baada ya Mwaka inakua yake, wewe umeingiza lak 6, ni Wehu.

Kununua Pikipiki 3M, kumpa Boda kwa mkataba, Baada ya Mwaka inakua yake, wewe umeingiza lak 6, ni Wehu.

CONTRARIAN

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
982
Reaction score
3,137
Yaaani Unatoa 3M,
Unaletewa 10k × 365 = 3,650,000
Faida kwa mwaka = 650,000
Faida kwa mwezi = 54,000.
Faida kwa siku = 1,800, 😂😂😂
Wagonjwa wa akili ni wengi..

Issue sio aina ya biashara tuu, japo bado ni ya kufikiria mara mbili, Maana inamaanisha Piga Ua, faida ya Mmiliki wa boda boda(1,800) haiwezi endesha familia kwa siku, sasa jiulize wamama wangapi wauza matunda, mboga mboga, vitumbua wenye mtaji chini ya 500k wanalisha familia siku nzima?

Kuna issue nyingine kama
Marejesho ya Siku &
Muda wa mkataba.

Fikiria mara tatu.

BIG UP kwa Wanangu Boda boda mnaoshikilia kwenye Mkataba.💪💪

Simaanishi, Boda kupata 10k kwa siku ni simple sana, namaanisha muunganiko wa hivyo vitu vitatu hapo juu,
Bora anayenunua hizi za 2.4M.
 
Hesabu ya mkataba ni zaidi ya elf kumi kwa siku,ila uko sahihi,ni bora kuwekeza katika hisa za mashirika na benki kuliko kuwekeza kwa boda boda,hapo hujaletewa kesi za barabarani na matengenezo ya chombo,hii inamuusu mwenye chombo.
 
Wewe sio yule introvert Gunner kweli umeamua kubadili I'd upondee biashara za wanaume wenZio
Naionaga kama biashara kichaa, kuna sister mjesh alinunua 3 akawakabidhi vijana kila siku alikuwa analalamika kuhusu rejesho
a
 
Yaaani Unatoa 3M,
Unaletewa 10k × 365 = 3,650,000
Faida kwa mwaka = 650,000
Faida kwa mwezi = 54,000.
Faida kwa siku = 1,800, 😂😂😂
Wagonjwa wa akili ni wengi..

Issue sio biashara, kuna kitu kimoja kati viwili hapo
1. Marejesho ya Siku
2. Muda wa mkataba.

BIG UP kwa Wanangu Boda boda mnaoshikilia kwenye Mkataba.💪💪
Uko kwenu bodaboda ya mkataba huwa mnarejesha elfu 10 kwa siku?

Mimi sina maoni kwa hilo, kuna jamaa yangu alinunua tena used tukiwa chuo alinitangulia mwaka, akampa mtu akawa anampa hesabu na anayeisimamia ni mama yake. Jamaa alisoma chuo meals & accomodation kwa kutegemea pikipiki. Na HESLB hela yao yote alikuwa anakusanya tu.
Hadi anamaliza chuo ana pikipiki mbili.

Baadae akauza zote akanunua bajaj akaendesha mwenyewe, kutokana na kuwa na matumizi boom lilipokuwa linaingia hakuwa na kazi nalo akaanzisha biashara ndogo, baada ya chuo akafungua duka kubwa na sasa hivi anayo mawili. Hiyo safari ni ya 6 years mpaka muda huu naandika. Ila ilianza na bodaboda.

Biashara kwanza ni kipaji, pili ni kuwa serious and focused. Kama huna hivyo vitu hata upewe exclusive right, unaangukia pua. Na kila biashara ina story mbili, kufeli na kufaulu.
 
1000018776.jpg
 
Hesabu ya mkataba ni zaidi ya elf kumi kwa siku,ila uko sahihi,ni bora kuwekeza katika hisa za mashirika na benki kuliko kuwekeza kwa boda boda,hapo hujaletewa kesi za barabarani na matengenezo ya chombo,hii inamuusu mwenye chombo.
Mfanyabishara akipewa hizo options mbili atanunua pikipiki. Mjasiriamali atafanya hivyo pia.

Mwekezaji ndio atachukua option ya hisa, hana njaa ya haraka. Hisa kwa bongo hii unalaza sana hela na hakuna kampuni inakua kwa kasi, hakuna fintech yoyote DSE ni haya makampuni ya simenti na pombe ndio utegemee maajabu.
 
Niliingiza 10 million fixed deposit kwa mwka wakaniingizia laki 8. What a wasteful

Ila pikipiki 3, kwa mwaka na miezi 3 unapata faida zaidi ya fixed deposit

Ila biashara ya pikipik changamoto ni madereva. Usiingie kwa kuambiwa
Ukikadiria inflation ya mwaka jana ilikuwa 3% ambayo siiamini kabisa naona wameishusha makusudi, hapo kama ni mwaka jana hiyo 10M imepungua laki tatu.

Baki yake ukiongeza hiyo laki nane uliyoambulia kiuhalisia ulitoka na 10,500,000 bila kuingiza gharama nyingine sijui kusafiri, kufungua akaunti na makato.
 
Back
Top Bottom