Kunywa pombe kuna faida gani??

Kunywa pombe kuna faida gani??

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
7,375
Reaction score
6,958
Nimekuwa najiuliza hivi pombe pamoja na kukatazwa na imani tofauti tofauti, Madaktari kuwazuia baadhi ya wagonjwa, na watu wengi kupewa ushauri waache pombe.
Lakini cha ajabu pombe inazidi kunyweka sana sana, pita mabarabarani utakuta bar zimeongozana na zimejaa watu mno wakinywa!, Kuna pombe za kila aina kuanzia za kizungu, za kichina, za kiarabu, za kiafrika( kama vile Denge, Chimpumu, Ngedule, Choya, Gongo n.k) n.k..
Hivi kweli jamani watu woote hawa wanao kunywa hizi pombe wanatumia kitu kisicho na faida???? Noo... naamini huenda zikawepo...
Faida ya pombe ninini?
 
usipokunywa utachanganyikiwa mapema....zinaburudisha mwili na kuleta furaha moyoni,,,tamu sana
 
Faida za pombe
1-Kuahirisha matatizo
2-Ngono zembe
3.............
 
Raha ya Pombe muulize Chrispin atakwambia.
Jaribu uone utaona faida yake.
 
jipe moyo kwa kujidanganya
Hivi kumbe si kweli?
Mi nikinywa pombe huwa nakuwa tajiri kwa muda. Nasahau kama kuna kufa, watu wote nawaona maskini isipokuwa mimi. Matatizo yote huisha. Sijawahi kuona hasara ya pombe kwa kweli. Mpaka sasa sijaona.
 
Raha ya Pombe muulize Chrispin atakwambia.
Jaribu uone utaona faida yake.
sema faida zake wewe hapO
Chimunguru kakupa baadhi endelea au cement hizo....
 
Hivi kumbe si kweli?
Mi nikinywa pombe huwa nakuwa tajiri kwa muda. Nasahau kama kuna kufa, watu wote nawaona maskini isipokuwa mimi. Matatizo yote huisha. Sijawahi kuona hasara ya pombe kwa kweli. Mpaka sasa sijaona.
and thats my honest big Pako!!!
 
Faida za pombe
1-Kuahirisha matatizo
2-Ngono zembe
3.............

hasara za pombe
1.Matumizi mabaya ya pesa
2.Hangover asubuhi
3.ngono uzembe
4.dhambi kwa Mungu
5.Ugomvi na watu kwa wale wasio weza kujizuia
6.Huzeesha haraka
7.Huna muda wa kukaa na familia
8.Unadharaulika (kwa wale wanakunywa kwa kupitiliza)
9.
-----------------
-----------------
----------------
--------------------
--------------------
---------------------
 
Unataka ufahamu faida zake ili uanze kunywa au ili usinywe kabisa? Kwanini usinywe kwa kuwa sio kosa la jinai ili upate majibu unayoyahitaji? Kwa kuwa mitizamo juu ya pombe inaegemea na mhusika, kama mtu nimnywaji ana majibu yake ambayo ni tofauti na shekh au pastor fulani au mlokole fulani pale.
 
Kwangu mimi Pombe haina faida(kwa mtu) bana,ina hasara(inakuletea umasikini,ngono zembe,ujasiri wa kijinga unaoweza pelekea upigane/upigwe au kufanya uhalifu wowote ule,magonjwa kama kisukari na matatizo ya ini(gongo)

Sanasana pombe ina faida kwa serikali tu maana inapata kodi nyingi kutoka makampuni yanayotengeneza vilevi...Ni mtizamo tu
 
Afya jingi (mashavu hiha).

Nna bro wangu anakata ulabu kwa kwenda mbele. Jamaa ngano imemfanya kapasuka mwili kinoma....
 
Kunywa pombe si tatizo hata kidogo, ni faida kama utakunywa ya kutosha na kwa wakati muafaka... tatizo liko kwenye ulevi hapo sasa ndio kuna matatizo mengi mengi na ya ajabu. lkn kunywa pombe kiasi inasaidia kuburudisha mwili, inasaidia kupata mda wa kujumuika pamoja kwa ndugu na jamaa, inasaidia kukata mzizi wa fitina kwa wale waliokuwa wamekosana kule kijijini mtu akikosea anapewa faini ya kununua debe la pombe na watakunywa wazee pamoja na mkosaji na mwisho wa siku jamaa anakuwa kasemehewa.... so tupige vita ulevi na si pombe kama ambavyo pia inatakiwa tupige vita ulafi mbona ulafi watu hamsemi wakati nayo ni dhambi na ina madhara kama kuwa na kitambi na kushindwa kumtimizia haja mama nyumbani,
 
Hahaaaaaa,kupasuka mwili kinoma na kuwa na shavu hiha ni afya!!!!!!...haya bana,we jifariji tu
 
Nimekuwa najiuliza hivi pombe pamoja na kukatazwa na imani tofauti tofauti, Madaktari kuwazuia baadhi ya wagonjwa, na watu wengi kupewa ushauri waache pombe.
Lakini cha ajabu pombe inazidi kunyweka sana sana, pita mabarabarani utakuta bar zimeongozana na zimejaa watu mno wakinywa!, Kuna pombe za kila aina kuanzia za kizungu, za kichina, za kiarabu, za kiafrika( kama vile Denge, Chimpumu, Ngedule, Choya, Gongo n.k) n.k..
Hivi kweli jamani watu woote hawa wanao kunywa hizi pombe wanatumia kitu kisicho na faida???? Noo... naamini huenda zikawepo...
Faida ya pombe ninini?

TBL is one of the largest taxpayers in Tanzania. Labda tujiulize pia na hiyo kosdi wanayolipa walevi tunaifanyia nini?
 
Kunywa pombe si tatizo hata kidogo, ni faida kama utakunywa ya kutosha na kwa wakati muafaka... tatizo liko kwenye ulevi hapo sasa ndio kuna matatizo mengi mengi na ya ajabu. lkn kunywa pombe kiasi inasaidia kuburudisha mwili, inasaidia kupata mda wa kujumuika pamoja kwa ndugu na jamaa, inasaidia kukata mzizi wa fitina kwa wale waliokuwa wamekosana kule kijijini mtu akikosea anapewa faini ya kununua debe la pombe na watakunywa wazee pamoja na mkosaji na mwisho wa siku jamaa anakuwa kasemehewa.... so tupige vita ulevi na si pombe kama ambavyo pia inatakiwa tupige vita ulafi mbona ulafi watu hamsemi wakati nayo ni dhambi na ina madhara kama kuwa na kitambi na kushindwa kumtimizia haja mama nyumbani,

Mkuu unanitia moyo sana, na mimi najiuliza kweli watu hawa woote wanatumia kinywaji chenye hasara tupu!!??
 
Nimekuwa najiuliza hivi pombe pamoja na kukatazwa na imani tofauti tofauti, Madaktari kuwazuia baadhi ya wagonjwa, na watu wengi kupewa ushauri waache pombe.
Lakini cha ajabu pombe inazidi kunyweka sana sana, pita mabarabarani utakuta bar zimeongozana na zimejaa watu mno wakinywa!, Kuna pombe za kila aina kuanzia za kizungu, za kichina, za kiarabu, za kiafrika( kama vile Denge, Chimpumu, Ngedule, Choya, Gongo n.k) n.k..
Hivi kweli jamani watu woote hawa wanao kunywa hizi pombe wanatumia kitu kisicho na faida???? Noo... naamini huenda zikawepo...
Faida ya pombe ninini?

Haina faida kivile sana. But TBL is one of the largest taxpayers in Tanzania. Labda tujiulize pia na hiyo kodi wanayolipa walevi tunaifanyia nini?
 
Pombe ni dawa. "Sio unywe tu maji, kunywa na mvinyo ili kuondokana na magonjwa yako ya tumbo huku ................."

Hiki ni kifungu kwenye biblia. Kwa wajuzi wa bibilia watakubaliana nami.
 
Hahaaaaaa,kupasuka mwili kinoma na kuwa na shavu hiha ni afya!!!!!!...haya bana,we jifariji tu

Kwa kurudia kwa kusisitiza maneno nliyotumia, ''i have done the needful 4 u'' (nakote Chrispin hapa).
 
Kwangu mimi Pombe haina faida(kwa mtu) bana,ina hasara(inakuletea umasikini,ngono zembe,ujasiri wa kijinga unaoweza pelekea upigane/upigwe au kufanya uhalifu wowote ule,magonjwa kama kisukari na matatizo ya ini(gongo)

Sanasana pombe ina faida kwa serikali tu maana inapata kodi nyingi kutoka makampuni yanayotengeneza vilevi...Ni mtizamo tu

Hakuna kisichokuwa na madhara kinapotumika kwa kiwango cha kuzidi. Magari ni mazuri lakini tunalalamikia mwendo kasi! Kadhalika na pombe kama ukifanya mwendo kasi ndio madhara yake. Vingenevyo, pombe ni kinywewa murua na kinachoburudisha kuliko vinywaji vyote. Na ndio maana kinaweza kunywewa kwa muda mrefu kuliko kinywewa kingine. Watu mara nyingi wanaisingizia pombe kwani huwawezesha kuyafanya yale yaujazao moyo wao kwa kisingizio cha pombe!
 
Back
Top Bottom