TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,767
- 20,869
Unajua nanii.. vijana wengi kabla hawajaoa hua wanadhani kwamba wana hela. Hii ni kwasababu matumizi binafsi yanakua madogo hivyo mtu kuweza kumudu maisha kirahisi. Hata akiwa na kabiashara anaanza kuona kama kanalipa ananunua na kausafiri.Habarini za wakati huu Wazee!
Kama maada inavyojieleza, kuna mshikaji wangu wa karibu sana alinishirikisha Jambo ambalo likanifikirisha sana na kuwa shauku kufuatilia zaidi. Huyu mshikaji wangu yupo Dsm kwa sasa na mimi nipo Dsm kwa muda, jana tukapata muda wa kukutana kupata moja baridi moja moto. Katika stori, jamaa yangu akawa analalamika kuwa maisha yake yamekua hovyo na uchumi wake unazidi kudhiofika siku hadi siku.
Na Changamoto na majanga yalianza kuonekana. Alinisimulia mengi, Changamoto za Uzazi uchumi na maisha kiujumla imekua shida. Ni mwaka wa Sita sasa, Hawajapata mtoto ili hali kabla ya kuoa alipataga mtoto na Alipooa tu alitaka mtoto lakini imekua ngumu. Lakini pia Kila Biashara anayoanzisha inakufa anakula hasara na Kuna Biashara juzi hapa amefunga baada ya mfululizo wa hasara tu kwa Sababu ya mauzo mabovu lakini eneo ambalo Biashara ilikuwepo ni Biashara ni Eneo ambalo lina mishe mishe na Biashara zinafanyika. Maduka yanafunguliwa na yakua ila Biashara yake imekufa.
Kabla ya Kumuoa huyu Mwanamke Mishe mishe zilikua zinalipa. Biashara zake zilikuwa zinaenda vizuri na alikuwa na kausafiri. Sasa hivi amerudi nyuma kiuchumi kwakweli, maana hata mwili wake umepungua na anaonekana mwenye mawazo.
Swali langu kwenu wadau, Je kuna ukweli kwenye haya anayosema huyu Jamaa na Kama ni kweli, Njia ya kutokea hapo hua ni nini ? Kwa wazee wetu mliokula Chumvi Nisaidieni kujua kama kuna namna anaweza kufanya kuondoa hiyo hali ya kutokupatana Damu.
Ukishaoa sasa ndio unashangaa kama kwa mwezi ulikua unatumia laki 2, sasa unaanza kutumia laki 7, kodi ulikua unalipa 80,000 chumba kimoja sasa inabidi ukodi nyumba nzima 400,000 maana mna msichana, mara wageni, mara wadogo zake.. Hapo hujaanza kutuma hela ukweni, mara kuna mgonjwa, mara misiba, mara sijui mdogo ake kaishiwa ada, huku mke anataka saluni, nguo, nywele, kutolewa out...
Weee.. lazima uanze kutafuta mchawi.