Kuoa au Kuoana na Mtu msiyeendana nyota

Unajua nanii.. vijana wengi kabla hawajaoa hua wanadhani kwamba wana hela. Hii ni kwasababu matumizi binafsi yanakua madogo hivyo mtu kuweza kumudu maisha kirahisi. Hata akiwa na kabiashara anaanza kuona kama kanalipa ananunua na kausafiri.

Ukishaoa sasa ndio unashangaa kama kwa mwezi ulikua unatumia laki 2, sasa unaanza kutumia laki 7, kodi ulikua unalipa 80,000 chumba kimoja sasa inabidi ukodi nyumba nzima 400,000 maana mna msichana, mara wageni, mara wadogo zake.. Hapo hujaanza kutuma hela ukweni, mara kuna mgonjwa, mara misiba, mara sijui mdogo ake kaishiwa ada, huku mke anataka saluni, nguo, nywele, kutolewa out...

Weee.. lazima uanze kutafuta mchawi.
 
Nyota kwani wanaishi angani?. Shehe Yahya ameharibu sana watu.
 
Ujinga mwengine huu mtu hamiliki ata baskeli ila ana nyota zilizopo angani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…