Kuoa kwenye Familia Tajiri ni taabu sana

Kuoa kwenye Familia Tajiri ni taabu sana

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kuoa kwenye Familia Tajiri ni taabu sana, mkikosana siku ya kesi uwanja mzima unajaa magari ya nyumbani kwao, alafu ukute kuna ndugu zake wengine wapo Nje ya nchi wanafatilia kesi Online, wanatishia kama umeshindwa kulea mtoto wetu tuletee huku Australia tutamlea wenyewe🥱🥱
 

Attachments

  • 1727879602090.jpg
    1727879602090.jpg
    97.5 KB · Views: 4
Tena usiombe wakawa watani zangu wahaya utajuta
Dogo mmoja dereva wangu wa Bajaj akataka kwenda kuoa kwa hawa watu,hakutaka mbwembwe sijui za magari na nini yeye akachukua kijiweni kwake vijana wenzake kumpa kampan ya kumbebea ndugu zake kwenda ukweni kujitambulisha,Bajaj zilikuwa kama sita hivi.

Kufika gate lilipo na ilipo nyumba ya wakwe (ndani ya fence) ni zaidi ya 100 mt sasa ule muongozano wa vile vibajaj mule ndani wale wahaya wakaona ajabu nikasikia mmoja wao(baadae kwenye mazungumzo nilikuja kugundua ni mjomba mtu) akisema kwa lafudhi yao “iih bhojo,hutu tudude twa walemavu tumefuata nini humu ndani,we mujuni ka-press alarm switch pale watu wajiandae kwa mapambano,raabda tumevamiwa”,mwengine akadaki “ina maana ndugu yetu anaolewa na mulemavu” mi nilivyosikia tu ile lafudhi na yale maneno nikamwambia oya dogo hapa mke hamna.
 
Hawa jamaa wanaweza kukufanya ujute kukosa hela na kuoa ndugu yao .

Hawana neno tafsida katika kumwambia mtu ,hawashindwi kukuambia Sasa bila ndugu yetu wewe si ungekuwa umekufa na maisha magumu ?
Nawapiga konzi na kohozi sipendag ujinga mm😂😂
 
Back
Top Bottom