Kuoa mwanamke bikira hakuwezi kuifanya ndoa yako kuwa bora

Kuoa mwanamke bikira hakuwezi kuifanya ndoa yako kuwa bora

Bi zandile

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
301
Reaction score
856
Kuna wanaume wajinga wajinga hivi wenye akili za kitoto kila uchwao hubweka... "usioe mwanamke asiye bikira." Kiuhalisia hao jamaa hawajui maana ya ndoa ni nini. Wapo walioa mabikira kwa kudhani kuwa ndoa zitadumu kumbe sivyo hivyo. Waliachana na hao mabikira zao.

Wapo wanaojua nini maana ya ndoa walioa wanawake wasio mabikira, hadi leo wanafurahia ndoa za zilizo katika ubora.

Ubikira hauifanyi ndoa kuwa bora. Kinachofanya ndoa iwe bora ni kwa wanandoa kutokuwa na ubinafsi, msamaha, utu wema, uvumilivu na kujitolea. Mimi na mume wangu tusingeoana iwapo tugekosa hizo sifa za kuifanya ndoa iwe bora.

Mnaotafuta mabinti mabikira wa kuoa niwaambie bila kuwaficha.... "bado hamjapata akili ya kuishi na mwanamke - ninyi wenyewe sio mabikira halafu mnatafuta mabikira wa kuoa huo ni ujinga wa kiwango cha kokoto."

Siku mkiacha ujinga mtafanikiwa katika ndoa as couple mliooana huku nyote mkiwa sio mabikira.

Mungu awaondolee ujinga.
 
Tatizo bikra zinauzwa madukani siku hizi.

Kuna binti wa Kidigo nilisoma nae Uganda, ilikuwa tunaishi kama mke na mume na kufanya yote kama wanandoa.

Baada ya kumaliza shule aliambiwa tu kuwa kuna mume katokea na anaolewa.

Moja ya mila za watu wa Tanga ni kuweka shuka nyeupe chumba cha bwana na bibi harusi usiku wa kwanza baada ya ndoa. Wakikuta damu inamaanisha demu alikuwa bikra na wazazi hupewa zawadi.

Kwa yule binti damu ilitoka nyingi na sifa kedekede kwenda kwa wazazi wake kuwa wamemlea vyema.

Baadae kuja kuongea na demu akasema alipewa dawa ya kufunga na mama yake kumfanya awe na utepe tena.

Mumewe mpaka leo anaamini kambikiri mkewe kumbe demu keshabikiriwa toka kinda. Hata mimi sikumkuta na bikra na alishapanch mimba kadhaa.
 
Back
Top Bottom