Kuoa sio maendeleo acheni kulazimisha watoto kuoa mapema

Kuoa sio maendeleo acheni kulazimisha watoto kuoa mapema

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Imekua ni kawaida kwa Vijana wengi kuoa mapema kuanzia miaka 20-25 tatizo wengi wanaolea nyumbani kwa wazazi unakuta nyumba vyumba vitatu Babu, Bibi, Baba, Mama na Wajukuu wengi mithili ya vifaranga wa Tai.

Wote wanaishi hapo nyumbani. Muda ambao kijana alitakiwa kutafuta maisha ndio analazimishwa kuoa na kulewa hii imeleta sana umasikini haswa mikoa ya Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma na Tanga ndugu zangu acheni vijana wajitafute ndoa sio maendeleo ni hatua tu ya kawaida kwenye maisha.

nigerFP_nigerFPnew.jpg
Fati 3.JPG
 
Unataka watoto waendelee kuzini mkuu. Acha waoane tu. Sema Ndoa nyingi zinavunjika sababu hiyo ya wa2 kuoana wakiwa na umri mdogo.
 
Umeacha usukumani, unyamwezini, uhayani, ukuriani, ukihani, ufipani, umasaini, uarushani, utaturuni, ugogoni ambako vijana wanaoa wakiwa wadogo na bado wapo nyumbani.

By the way ndoa za mapema hudumu kwa kuwa mnazoana katika changamoto za maisha. Familia nyingi za kitanzania walizaliwa wengi.

Hawa modern people ndio wanaona ndoa za mapema ni tatizo, na ndio maana ndoa zao hazidumu kwa sababu wanaoana wakiwa wakubwa kila mwanandoa ni mjuaji na ana kila nyenzo za kumtishia mwenzake ikiwemo ajira, fedha na mali ambazo wanaoana tayari wana hivyo vitu. Waislam wanadumisha mila za dini yao na maadili ya familia
 
Back
Top Bottom