Kuogopana kwa Watanzania nchini Marekani

Kuogopana kwa Watanzania nchini Marekani

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
WaTanzania tuna asili ya undugu na ukarimu kwa hapa nyumbani........ lakini kwa Marekani ni tofauti kabisa...wabongo huogopana sana.

Maisha na michongo hupatikana kwa waKenya yaani Mtanzania na Mkenya kwa Marekani ni zaidi ya ndugu.

Sasa katika pitapita zangu kuna sehemu huwa naenda kupata ''gahwa'' na kitu kama kashata za karanga wenyewe wanaita 'peanut butter cookies',,,{hii hunifanya nijisikie niko kwenye vijiwe vya kahawa vya nyumbani}

Wakati napooza baridi na kahawa nikasikia mtu anazungumza kiswahili kwenye simu....na kiswahili chake ni cha kibongo haswa.....basi mara baada ya kumaliza kuzungumza nikaona vyema nimsabahi,,,,,dooh mwanangu jamaa alipaniki mpaka nikaona huu mtihani lakini hata hivyo nikazidi kuzungumza nae kiungwana na kiundugu.......

Kwa kifupi jamaa akawa mpole na baada ya kumkaribisha gahwa akaanza kufunguka yeye bongo anatoka sehemu gani na yupo marekani kwa muda mrefu sana sana....akazidi kunijuza visa mbalimbali vya wabongo kufanyiana roho mbaya.........

WAbongo wengi waliokuja miaka ya 80 themanini na tisini wazazi wao walikuwa aidha ni viongozi au wafanyabiashara wakubwa....na watoto wengi maisha yao ya nyumbani yalikuwa na hali nzuri sana,

Pia kuna wabongo wachache ambao wametoka kwenye familia za kimasikini ambao wao hukumbuka kufanya hili na lile kwa nyumbani,,,

Sasa wale watoto wa wakubwa hakuna la maana walilofanya aidha nyumbani au huku marekani wengi ni walevi wengine ni mateja na wengine wako jela ama wametoka jela kurudi nyumbani wanaona noma....kazi yao kubwa ni kuwafanya wabongo wengine waharibikiwe,,,,,,,

Wazazi wao huko bongo wengi wamekwisha fariki na wengine wamestaafu kazi na hali zao kiujumla si nzuri,,,,,,Hapa ndipo nikamkumbuka mzee fulani maeneo ya Mbezi beach watoto wake wote wako marekani lakini yeye maisha yake ya kinyonge sana,,,,angalau jumba analokaa linaonyesha hapo kabla alikuwa MTU lakini.........
 

Attachments

  • 20250123_132933.jpg
    20250123_132933.jpg
    401.6 KB · Views: 7
  • 20250123_143714.jpg
    20250123_143714.jpg
    1,013.9 KB · Views: 5
  • 20250123_143549.jpg
    20250123_143549.jpg
    553.5 KB · Views: 5
  • 20250123_143650.jpg
    20250123_143650.jpg
    1.4 MB · Views: 6
Heeee! Kwa nini waogopane sasa
Swali zuri.....
Zipo sababu mbalimbali....
Lakini kubwa linalozungumzwa ni 'MAKARATASI'
NA kingine ni roho mbaya tu.....kwa mfano mtu yupo huku marekani miaka 20 lakini hana kitu....iwe bongo au hapa USA
Sasa wengine wamekuja wana miaka miwili au mitatu tayari nyumbani wameshajenga na kufanya maendeleo.......sasa chuki na wivu kwa hawa 'wakongwe'iwapo watajua huna karatasi....mwanangu wanakuchoma.....
 
Sio marekani tuu hata kwa madiba, ngozi nyeusi ni tuna chuki mbaya sana, japo kuna baadhi wenyewe roho njema husaidia wengine

Wengi wameogopa kusaidia wengine kwa kuhofia u- snitch
Watu wanaogopa kuambukizana "dhambi". We mtu hujui ameingiaje nchi ya watu, ukiwa naye , akikamatwa na wewe umo.
 
Kuna mwanamke mmoja wa kichaga anaduka la bidhaa x.,. London unadhani kwa tabia zetu anaweza kumsaidia yoyote..?
Binafsi, nilishapewaga stori za mambo yetu mabaya tukiwa nje ya nchi. Pale Durban kwa Madiba, nilishawhi ingia duka moja, nikakutana na watu wanaongea kiswahili cha ki-Tanzania. Nikaogopa sana kuongea nao, maana nilikumbuka niliyoambiwa. Na bahati mbaya stori zao zilikuwa na kidilidili chafu..!!!
 
Back
Top Bottom