Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Kuokoka kunahusiana na kumwamini Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yako.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele(Yohana 3:16).
Lakini Yesu alisema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka
Mathayo 24v13
Au mwisho umekwishafika?
 
Kuokoka ni kuachana na dhambi
Mtu aliyeokoka anaacha kabisa maisha ya dhambi na kuanza kutembea katika utakatifu.
"Basi tubuni, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana." (Matendo 3:19)
Hivi mkuu maisha ya dhambi ndiyo maisha gani hayo ?

Nieleweshe na hii ,hivi tunaacha dhambi au dhambi zinafutwa tu ?
 
Hivi mkuu maisha ya dhambi ndiyo maisha gani hayo ?
Maisha ya dhambi ni maisha yanayofuata matakwa au tamaa za mwili badala ya kufuata mapenzi ya Mungu. Yaani, ni maisha ambayo mtu anaishi bila kujali sheria na mapenzi ya Mungu. Mtu ambaye haoni tatizo kusema uongo, kuzini, kunywa pombe... huyo anaishi masha ya dhambi.

Wakolosai 3:7-10 inatuambia:
Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo[ya dhambi]. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu. Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake. (Kol 3:7-10).
Nieleweshe na hii ,hivi tunaacha dhambi au dhambi zinafutwa tu ?
Unapotubu dhambi unakiri kwamba umekosea na hutarudia tena dhambi. Kwa maana hiyo ukitubu na kuokoka, dhambi ulizotenda nyuma zote zinafutwa. Kuanzia hapo hupaswi kurudia tena matendo ya dhambi uliyoyaacha. Ndio sababu Paulo anawaambia waliokuwa wezi kabla hawajaokoka, wasiibe tena:
Waefeso 4:28
Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.

Kama sijaeleweka usisite kuuliza
 
okay naona umetaja matendo ya dhambi, sawa
kwani dhambi ni nini mkuu
 
Walokole nyinyi ni wanafiki tu. Tusidanganyane hapa. Hakuna dhambi mnaifanya kwa kiwango cha juu kama dhambi ya kuzini/uasherati wa kimya kimya!
Leta ushahidi. Umeniona wapi nafanya uzinzi.
Nikose kuingia mbinguni kwenye raha ya milele kwa ajili ya uchafu huo?
Halafu ujue, sio kila mtu anayejiita mlokole ameokoka kweli. Inawezekana hao uliowaona wakifanya uzinzi ni "magugu" Siku ya mwisho, ngano na magugu vitatenganishwa. Magugu yatachomwa moto
 
Lakini Yesu alisema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka
Mathayo 24v13
Au mwisho umekwishafika?
Ni kweli Mathayo 24:13 inasema, ‘mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.’ Lakini andiko hilo halimaanishi kwamba hakuna kuokoka sasa, bali linaonyesha umuhimu wa kudumu katika imani hadi mwisho wa maisha au hadi Yesu atakaporudi. Ukikata tamaa njiani badala ya kuvumilia mateso na udhia, unapoteza wokovu.

Maandiko yafuatayo yanaeleza wazi kwamba mtu anaweza kuokoka sasa.

Waefeso 2:8 – ‘Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.’

Tito 3:5 – ‘Alituokoa, si kwa matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake...’

Luka 7:50 – Yesu akamwambia yule mwanamke: ‘Imani yako imekuokoa; enenda zako kwa amani.’

2 Timotheo 1:9 – ‘Yeye alituokoa na kutuita kwa mwito mtakatifu...’
 
By definition,
Mlokole Ni Mtu aliyethirika akili kutokana na uraibu WA dini ya kikristo

Characteristics za mlokole
1. Hana kanisa maalum la kuabudu,
(Ana hamahama makanisa ovyo)

2. Anatabia ya kufoka foka sana anapoabudu.
(Akiabudu Kwa saiti ya chini, anahisi Mungu hamsikii)

3. Anaamini matatzo yake yote yanasababishwa na KUROGWA.
 
Mlokole Ni Mtu aliyethirika akili kutokana na uraibu WA dini ya kikristo
Hizo kauli ni janjajanja tu ya shetani kuwashawishi watu wasiokoke na kufaidi baraka za wokovu.
Hata Yesu walisema amerukwa na akili:
Marko 3:21:
"Jamaa zake walipopata habari walitoka kwenda kumkamata, kwa maana walisema, Amerukwa na akili." (Marko 3:21, SUV)
Characteristics za mlokole
(Ana hamahama makanisa ovyo)
Mtu akiujua ukweli hawezi kubaki kwenye kanisa ambalo anaona lina matapeli wauza chumvi na mafuta
2. Anatabia ya kufoka foka sana anapoabudu.
Sio dhambi kuabudu kwa sauti kubwa. Mungu aliyetuumba ndiye aliyetupa uwezo wa kuongea kwa sauti kubwa. So, kama mtu anajisikia vizuri akiabudu kwa sauti kubwa usimzuie.
Hata Zaburi 98:4 inatuhimiza kumpazia Mungu sauti wakati wa kumwabudu
"Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda."
3. Anaamini matatzo yake yote yanasababishwa na KUROGWA.
Nani amekudanganya. Hakuna mchawi anayeweza kumroga mtu aliyeokoka kwelikweli.
Hesabu 23:23
Kwa maana hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli...
 
Kuokoka ni kuzaliwa upya kiroho.
"Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu." (Yohana 3:3)
Walokole mnaposeema mmeokoka maana yake ni kwamba hakikisha unatenda dhambi na mtu asijue hasa dhambi ya kuzini.
Zaidi ya yote, hasa kwa wanawake na vijana, kuokoka siku hizi ni katrend maana ulokole siku hizi unakwenda na fashion na mapastor wanashidnana kuonyesha nani mwenye fedha na nayekula bata kuliko mwenzake, ova.
 
Walokole nyinyi ni wanafiki tu. Tusidanganyane hapa. Hakuna dhambi mnaifanya kwa kiwango cha juu kama dhambi ya kuzini/uasherati wa kimya kimya! Hamna wokovu wowote ule, zaidi ya unafiki.
Ulishawahi kuwa mlokole ukawa mzinzi? Au umeamua kuropoka tuu?
 
Kihalisia tu huwezi kuokoka ukiwa hapa duniani, acha kujihesabia haki subiri upite kwenye chujio
 
Walokole mnaposeema mmeokoka maana yake ni kwamba hakikisha unatenda dhambi na mtu asijue hasa dhambi ya kuzini.
Hayo ni mawazo yako. Ukimficha mtu utamficha na Mungu asijue?
Methali 6:32
Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa; huyo hujiangamiza yeye mwenyewe
Zaidi ya yote, hasa kwa wanawake na vijana, kuokoka siku hizi ni katrend maana ulokole siku hizi unakwenda na fashion na mapastor wanashidnana kuonyesha nani mwenye fedha na nayekula bata kuliko mwenzake, ova.
Hao wanaoshindana hawajui Maandiko
Wafilipi 2:3
"Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."

Halafu ni vizuri ujue kuwa sio wote wanaojiita mapastor ni watumishi wa kweli wa Mungu. Kuna wengine mungu wao ni tumbo.
Wafilipi 3:18-19
Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: Watu wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo. Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.
 
Naomba ufafanuzi wa hili, ...kuna mlokole mmoja naishi nae nyumba moja katika kuongea yeye kila siku anataka tuongelee masuala ya kiimani tu yani ukija na mada nyingine hataki, hili limefanya vijana wote mtaani kumkimbia (kumtenga) ni mimi pekee ndo huwa najaribu kukaa nae,sasa katika mazungumzo yetu ya kiimani nikimbana vizur huwa anakuja na jibu jepesi kwamba hayo ni mambo ya ROHONI mimi siyajui, sasa swali langu ni kwamba huko ROHONI ni kweli papo na kama papo je ni WALOKOLE pekee ndo wanafika maana sijawahi sikia waumini wa madhehebu mengine wanausemea huo ulimwengu wa ROHONI tofauti na WALOKOLE.
 
Back
Top Bottom