Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Naomba ufafanuzi wa hili, ...kuna mlokole mmoja naishi nae nyumba moja katika kuongea yeye kila siku anataka tuongelee masuala ya kiimani tu yani ukija na mada nyingine hataki, hili limefanya vijana wote mtaani kumkimbia (kumtenga) ni mimi pekee ndo huwa najaribu kukaa nae,sasa katika mazungumzo yetu ya kiimani nikimbana vizur huwa anakuja na jibu jepesi kwamba hayo ni mambo ya ROHONI mimi siyajui, sasa swali langu ni kwamba huko ROHONI ni kweli papo na kama papo je ni WALOKOLE pekee ndo wanafika maana sijawahi sikia waumini wa madhehebu mengine wanausemea huo ulimwengu wa ROHONI tofauti na WALOKOLE.
Huyo naona yuko vizuri. Nuru yake ndiyo inayowakimbiza hao wengine wnaopenda kuongea mambo ya gizani. Nuru na giza haviwezi kukaa pamoja. Wewe naona hauko mbali na wokovu.

Kuhusu mambo ya rohoni, yuko sahihi. Kuna mambo huwezi kuyaelewa bila kuwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anaingia kwa watu waliookoka tu.
1 Wakorintho 2:14
Mtu ambaye hana Roho Mtakatifu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni.

Ukiokoka, ndio utajua ukweli huo
 
Kuokoka ni series of practices of a saint. Kunaanza na kuamini then kubatizwa then kuishi maisha ya utakatifu then kuvumilia changamoto zote za kuuishi utakatifu mpaka mwisho; hauwezi kuruka stage ili kufikia hali ya kuokoka. Hii ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

NB:
Aliezaliwa mara ya pili {Born Again} na Alieokoka {The Saved} sio sawa kimaandiko.
 
Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiyo atakayeokoka (Mathayo 24:13 SUV)
 
Huyo naona yuko vizuri. Nuru yake ndiyo inayowakimbiza hao wengine wnaopenda kuongea mambo ya gizani. Nuru na giza haviwezi kukaa pamoja. Wewe naona hauko mbali na wokovu.

Kuhusu mambo ya rohoni, yuko sahihi. Kuna mambo huwezi kuyaelewa bila kuwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anaingia kwa watu waliookoka tu.
1 Wakorintho 2:14
Mtu ambaye hana Roho Mtakatifu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni.

Ukiokoka, ndio utajua ukweli huo
Sio mnateteana nyie?kama ni hivyo kwa nini iwe kwa WALOKOLE tu na sio waumini wa madhehebu mengine?
 
Walokole nyinyi ni wanafiki tu. Tusidanganyane hapa. Hakuna dhambi mnaifanya kwa kiwango cha juu kama dhambi ya kuzini/uasherati wa kimya kimya! Hamna wokovu wowote ule, zaidi ya unafiki.
ndo maana tunamuhitaji Yesu ili atuokoe hakuna ambaye anajiokoa kwa matendo yake

na baada ya kuokolewa tunapokea usaidizi wa roho mtakatifu kubafili mienendo yetu huku tukisoma neno na maombi bila kuacha kutangaza injili na wengine waokolewe
 
Yeyote anaedai ameokoka basi IQ yake ipo chini sana.
haya mambo walifichwa watu wenye akili wakafunuliwa watu wajinga

18 For the message about the cross is foolishness to those who are perishing, but to us who are being saved it is the power of God.
 
Ni kwa nini mtu asome Biblia? Je kutenda matendo mema na kuacha dhambi hakutoshi pasipo kusoma biblia?
ili ujue hayo matendo mema na hizo dhambi za kuziacha ni lazima usome neno na pia ili uweze kuwahubiria wengine habari za wokovu

Yesu mwenyewe alitumia neno la maandiko kuhubiri
 
Ni kwa nini mtu asome Biblia? Je kutenda matendo mema na kuacha dhambi hakutoshi pasipo kusoma biblia?
Matendo yote mema utayajuaje usiposoma Biblia? Yako mengi sana, mkuu.

Kuna faida nyingi za kusoma Biblia. Hizi hapa baadhi yake:
1. Inatufundisha mapenzi ya Mungu
Biblia ni Neno la Mungu. Ukiisoma, utajua yaliyo sawa machoni pa Mungu. Ni mwongozo wa maisha, unaotusaidia kuelewa kusudi la Mungu juu yetu.
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” – Zaburi 119:105

2. Hutulinda dhidi ya dhambi
Ukisoma Biblia dhamiri yako itakuwa safi. Maandiko ya Biblia yatakufundisha jinsi ya kuiepuka dhambi.
“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.” – Zaburi 119:11

3. Hutuimarisha kiroho
Biblia inatuwezesha kukua kiroho kama watoto wa Mungu, na kujua jinsi ya kuishi maisha ya utakatifu na imani.
“Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu.” – 1 Petro 2:2

4. Huongeza hekima na maarifa
Biblia inatupatia hekima – kwa ajili ya maisha yetu, maamuzi, mahusiano, kazi, nk.
“Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa.” – Mithali 1:7

5. Hutoa faraja na tumaini
Katika maisha kuna nyakati za huzuni, majaribu, na msongo wa mawazo. Biblia hutupatia faraja ya kweli.
“Kwa kuwa yote yaliyoandikwa zamani yaliandikwa ili kutufundisha sisi, ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.” – Warumi 15:4

6. Hujenga uhusiano wa karibu na Mungu
Kwa kusoma Neno la Mungu, tunazidi kumjua Yesu Kristo na kuimarisha mahusiano yetu naye kwa maombi na utiifu.

7. Hutuwezesha kuwahubiria wengine kwa usahihi
Tunapojua Biblia vizuri, tunaweza kuwa mashahidi wa kweli wa Kristo na kuwasaidia wengine katika imani.

8. Ina ahadi nyingi nzuri za Mungu kwa ajili yetu
Bila kuisoma huwezi kuzijua ahadi hizo. Na usipozijua huwezi kuomba Mungu azitimize kwako.

9. Biblia ina nyimbo nzuri za kumsifu Mungu
Kila aliyeokoka anapaswa kumsifu Mungu kwa nyimbo, Zaburi na Tenzi za Rohoni. Bila kusoma Biblia huwezi kuwa na maneno mazuri ya kumwimbia Mungu,

10. Biblia ina....
ANZA KUISOMA LEO UTAONA FAIDA NYINGINE NYINGI ZAIDI YA HIZO
 
Yeyote anaedai ameokoka basi IQ yake ipo chini sana.
To assert that the ontological affirmation of soteriological transformation is concomitant with a diminution of intellectual acumen is a paradigmatic manifestation of epistemic reductionism and philosophical myopia. Such a conjecture egregiously neglects the nuanced interplay between noetic faculties and transcendent metaphysical intuitions, erroneously presupposing that axiological adherence to the divine necessarily negates cerebral sophistication. On the contrary, the annals of intellectual history are replete with polymaths and erudite luminaries whose assent to theological verities coexisted symbiotically with formidable rational prowess. Hence, to impute diminished intelligence to those professing salvific conviction is not merely an ad hominem oversimplification but a categorical error grounded in an empiricist hegemony that fails to apprehend the legitimacy of non-material epistemologies.
 
Mimi ninavyojua kuokoka sio kuacha dhambi, bali ni kuzaliwa upya, unaweza kuwa mtu mwema na ukazaliwa upya kuwa mtu katili, yote ni kuokoka, maana umetoka kwenye hali ya zamani usiyoitaka (ya wema), na umezalliwa upya kwenda kwenye hali mpya unayoitaka na kuipenda (kuwa katili).

Na kuokoka ni kitendo kinachoanzia kwenye mawazo yako (meditation), na unaweza kuokoka katika nyanja mbali mbali (Tabia, muonekano, kiuchumi nk.., ) kila wiki kama unataka..


View: https://www.instagram.com/p/DG2uz1cqsRM/?igsh=MWRxcjVqYjUxYTBndg==

Duh, huo mtazamo wako hauendani kabisa na mafundisho ya Kikristo (Biblical Evangelical Christianity). Inaonekana umechanganya na falsafa ya New Age.

Unasema kwamba
“Kuokoka sio kuacha dhambi, bali ni kuzaliwa upya”
Katika Ukristo, kuzaliwa upya ni kuacha dhambi
“Basi mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! yamekuwa mapya.” – 2 Wakorintho 5:17
“Kila mtu azaliwaye na Mungu hatendi dhambi...” – 1 Yohana 3:9


Umesema pia kwamba
“Unaweza kuwa mtu mwema na ukazaliwa upya kuwa mtu katili”
Hii ni kinyume kabisa na mafundisho ya wokovu ya Kikristo. Kuzaliwa upya kunamgeuza mtu kuwa kama Kristo – siyo kutoka wema kwenda katika uovu.
“Kwa maana Mungu alituchagua sisi... tupate kuwa watakatifu, wasio na mawaa mbele zake katika upendo.” – Waefeso 1:4

Umesema tena kwamba
“Kuokoka ni kitendo kinachoanzia kwenye mawazo yako (meditation)”
Hii ni falsafa ya New Age au humanistic self-transformation, ambapo mtu hujibadilisha mwenyewe kwa kutafakari. Katika Biblia, kuokoka sio matokeo ya kutafakari, bali ni tendo la neema ya Mungu kwa imani:
“Kwa maana mnaokolewa kwa neema kwa njia ya imani... si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” – Waefeso 2:8-9

Sikubaliani na wewe unaposema kwamba
“Unaweza kuokoka katika nyanja mbali mbali... kila wiki kama unataka”
Huo ni mtazamo wa wokovu wa kimwili, sio wa kiroho kwa mujibu wa Biblia. Biblia haizungumzii “kuokoka kila wiki” bali unaokoka mara moja kwa njia ya imani katika Yesu, na kisha unatembea katika utakaso kila siku.
“Kwa kuwa kwa sadaka moja amewafanya wakamilifu hata milele wale wanaotakaswa.” – Waebrania 10:14.

Angalia sana ndugu, naona umepotea njia.
 
Biblia imesema mshahara wa dhambi ni mauti na sio moto
Soma Biblia yako kwa makini, ndugu.
Mathayo 25:41
“Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, enyi mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.”

Marko 9:43
“Mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia Jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki.”

Ufunuo 20:15
“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.”

Hii ndiyo "mauti ya pili," yaani, kutupwa kwenye moto wa milele baada ya hukumu ya mwisho.
 
okay naona umetaja matendo ya dhambi, sawa
kwani dhambi ni nini mkuu
Kwa kifupi: Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu – ni kuvunja au kupuuza sheria au mapenzi ya Mungu.
1 Yohana 3:4
"Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria."


Biblia inaeleza vizuri Mungu anapenda tufanye nini katika maisha yetu. Tuenende namna gani ili tumpendeze. Tukienda kinyume na anavyotaka, Mungu anahesabu tumefanya dhambi.
 
Kuokoka ni series of practices of a saint. Kunaanza na kuamini then kubatizwa then kuishi maisha ya utakatifu then kuvumilia changamoto zote za kuuishi utakatifu mpaka mwisho; hauwezi kuruka stage ili kufikia hali ya kuokoka. Hii ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

NB:
Aliezaliwa mara ya pili {Born Again) na Alieokoka (The Saved) sio sawa kimaandiko.
Kwa sehemu uko sahihi, ila naona kama unachanganya masomo. Yule mwizi msalabani mbona aliruka hiyo stage ya ubatizo? Ubatizo ni muhimu sana ila na-challenge tu hiyo kauli yako ya "huwezi kuruka stage."
 
Ulishawahi kuwa mlokole ukawa mzinzi? Au umeamua kuropoka tuu?
Unauliza swali kama uko dunia nyingine vile! Kwani nyinyi manojiita walokole mnaishi wapi mpaka tushindwe kuyaona matendo yenu ya uzinzi?
 
Back
Top Bottom