Thibitisha kwa Maandiko hiyo kauli
Kuzaliwa mara ya pili ni baada ya kuliamini neno, kubatizwa na kuanza kuishi maisha ya utakatifu.
1. 1 Petro 1:23
[23]Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
Being born again, not of corruptible seed, but of incorruptible, by the word of God, which liveth and abideth for ever.
Kwa kulisikia na kulitii lile neno la Mungu mtu huzaliwa mara ya pili.
2. Yohana 3:2-5
[2]Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
The same came to Jesus by night, and said unto him, Rabbi, we know that thou art a teacher come from God: for no man can do these miracles that thou doest, except God be with him.
[3]Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Jesus answered and said unto him, Verily, verily, I say unto thee, Except a man be born again, he cannot see the kingdom of God.
[4]Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
Nicodemus saith unto him, How can a man be born when he is old? can he enter the second time into his mother's womb, and be born?
[5]Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Jesus answered, Verily, verily, I say unto thee, Except a man be born of water and of the Spirit, he cannot enter into the kingdom of God.
Kwa kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu mtu huzaliwa mara ya pili.
Alieokoka ni aliyefanya yote yapasayo kuokoka. Kivipi nifuatishe hapo chini.
Maandiko yanaposema "ataokoka" yanamaanisha kuwa kile ulichokifanya kinakupa tiketi ya kufikia hali fulani ila unatakiwa kuendelea au kufanya kitu zaidi ili ufike huko.
1. Marko 16:16
[16]Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
He that believeth and is baptized shall be saved; but he that believeth not shall be damned.
Ukiamini ukabatizwa unapata tu tiketi ya kuokoka kwa maana ya kuwa bado una jukumu la kufanya ili ufike hali ya kuitwa umeokoka thats why maandiko hayajasema. Aaminiye na kubatizwa ameokoka.
2. Yohana 10:9
[9]Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
I am the door: by me if any man enter in, he shall be saved, and shall go in and out, and find pasture.
Kupitia kujifunza kutoka kwa Yesu Kristo/kukaa katika uwepo wake/ndani yake mtu ataokoka ila haiguarantee kuwa ameshaokoka kwakuwa bado ana wajibu wa kufanya ili kuitwa "ameokoka"; that's why andiko halisemi ukiingia kwa mimi umeokoka.
3. Warumi 10:13
[13]kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
For whosoever shall call upon the name of the Lord shall be saved.
Kuliitia Jina la Yesu Kristo kunakupa tiketi ila hakuguarantee kuokoka pasipo kutimiza wajibu mwingine that's why andiko halisemi "Kila atakayeliitia Jina la Bwana atakuwa ameokoka."
4. Mathayo 10:22
[22]Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
And ye shall be hated of all men for my name's sake: but he that endureth to the end shall be saved.
Unaweza ukayafanya yote kuanzia 1-3 ila ukikata tamaa njiani hauwezi kuokoka maana una wajibu wa kuvumilia mpaka mwisho ili uwe umeokoka.
Kuokoka = Kuiepuka ile hukumu ya Shetani na wafuasi wake = Kupata nafasi katika ufalme wa Mbinguni baada ya Kukamilisha 1-4
Kwa summary ni kuwa mtu anakuwa Born Again (Anazaliwa mara ya pili) angali hai katika maisha; na anakuwa Saved (Anaokoka) baada ya kutimiza wajibu wake katika wokovu ile sekunde yake ya mwisho ya kufa.