Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Kuokoka ni nini? Walokole wanaposema wameokoka, wanamaanisha nini?

Kama umekuwa ukijiuliza maswali kama hayo, leo ni siku yako ya kujua maana ya kuokoka na pengine ndiyo siku yako na wewe ya kuokoka.

Kuokoka ni neno tu la kawaida la Kiswahili lenye maana ya kusalimika au kunusurika kutoka katika janga, maafa makubwa au hatari yoyote inayokuijia. Mfano mzuri ni ile ndege iliyoangukia katika ziwa Victoria. Abiria katika ndege ile walikuwa katika hatari ya kufa maji; lakini alitokea kijana mmoja fundi sana wa kuogelea, akawasalimisha abiria wengi. Hapo tunasema fundi huyo wa kuogelea, aliwaokoa abiria; wakanusurika kufa maji. Kwahiyo abiria waliokolewa au waliokoka.

Kwanini sasa “walokole” wanasema wameokoka? Wamenusurika kutoka katika maafa gani?

Iko hivi: Baada ya Adam na Eva kufanya dhambi, wanadamu wote wanazaliwa wakiwa na asili ya dhambi na hivyo kujikuta wanatenda dhambi(Rum 5:12). Ndiyo sababu kwa mfano, mama akimnyima ziwa mtoto wake mchanga, anakasirika na kumpiga kofi mama. Jiulize hasira hiyo ameitoa wapi mtoto? Au je ni nani aliyemfundisha kupiga? Hiyo ni dhambi ya asili. Kwa asili hiyo kila mtu anahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi hata kama hafanyi uzinzi, haibi, au kusema uongo. Kwa sababu hiyohiyo mtu hata akijitahidi kutenda mema, bado tu anahesabiwa mkosaji, kutokana na asili yake ya dhambi(Ayu 9:29-31).

Mshahara wa dhambi ni kutupwa katika ziwa la moto milele (Rum 6:23; Ufu 21:8). Kuwapa maskini sadaka, kusali mara saba kwa siku, kipaimara, au tendo lolote jema la kidini, haliwezi kumfanya mtu anusurike kupata adhabu hiyo ya moto wa milele kwa sababu ya dhambi ya asili iliyomo ndani yake.

Ili unusurike au uokoke kutoka katika adhabu hiyo ya moto wa milele, ni lazima uhesabiwe haki na Mungu mwenyewe. Haki hiyo haipatikani kwa kushika sabato, kufanya sakramenti au kushika nguzo za kidini.

Haki hiyo inapatikana kwa kutubu dhambi zako na kuamua kuziacha kabisa na kumpokea Yesu Kristo moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukifanya hivyo, unasamehewa dhambi zako na kuokolewa (Mit 28:13; Mdo 3:19, Rum 10:10).

Kwahiyo ukitubu dhambi zako sasa hivi na kumwamini Yesu, utasamehewa na hapo tutasema umeokoka; yaani umenusurika kutupwa motoni na badala yake, umepata neema ya kuingia mbinguni. Kwa lugha nyingine tutasema “umezaliwa mara ya pili.”

Naamini umeelewa sasa kuokoka ni nini.
Mimi nimeokoka. Je, na wewe unapenda kuokoka leo? Naamini unapenda kwa sababu hakuna mtu anayependa kwenda jehanam, katika moto wa milele. Basi, kama unapenda kuokoka, omba(fuatisha) sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kukuokoa sasa hivi:

Omba hivi:, “Mungu Baba, asante kwa kunifundisha maana ya kuokoka. Nimetambua mimi ni mwenye dhambi kwa asili. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo, ili ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya katika maisha ya wokovu. Ubarikiwe sana!
Nenda katafute elimu ya maana maana hiyo ya kufikirika haitakusaidia wala kutusaidia zaidi ya kutupoteza na kutupotezea muda.
 
Kutomberner, kutudanganya una $15000
Hizo sio dhambi na kuhusu $ hizo kweli ninazo, nilikwambia na wewe nenda bank kaokote slip km rahisi..!!
Halafu sio kuweka hata kuzishika nazishika sana 😹😹😹
Sasa mkinga nakosaje pesa na nipo kkoo??
 
Kuokoka ni kuacha dhambi na kumrudia Bwana
Nani aliye hai hatendi dhambi? Hakuna dhambi mbaya kama kuwadanganya wengine nawe ukajidanganya. Wanatenda dhambi mbaya binadamu wanaojiita walokole kwani hawajaokoka kitu zaidi ya kudanganya wakajidanganya wenyewe.
 
Japo sijasoma mada yote wala sijaokoka, ila wanamaanisha "kumpokea yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yako"
 
Japo sijasoma mada yote wala sijaokoka, ila wanamaanisha "kumpokea yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yako"
Yesu mwenyewe yuko wapi na kwanini ukubali kuwa mtumwa au kondoo ili wachunaji wajiitao wachungaji wakuchune na kukula nyama washushie na damu yako na ya Yesu?
 
Hizo sio dhambi na kuhusu $ hizo kweli ninazo, nilikwambia na wewe nenda bank kaokote slip km rahisi..!!
Halafu sio kuweka hata kuzishika nazishika sana 😹😹😹
Sasa mkinga nakosaje pesa na nipo kkoo??
Kumbe mke watu😲😲😲
 
Hizo sio dhambi na kuhusu $ hizo kweli ninazo, nilikwambia na wewe nenda bank kaokote slip km rahisi..!!
Halafu sio kuweka hata kuzishika nazishika sana 😹😹😹
Sasa mkinga nakosaje pesa na nipo kkoo??
Nahitaji boxer toka happ kkooo bei zikoke boxer za ukweli?
 
Yesu mwenyewe yuko wapi na kwanini ukubali kuwa mtumwa au kondoo ili wachunaji wajiitao wachungaji wakuchune na kukula nyama washushie na damu yako na ya Yesu?
Kutoa sadaka sio lazima utoe madhabauni. Unaweza hata kuwapa chochote masikini na wasio jiweza. Na hakuna mchungaji anae lazimisha uweke sadaka kwenye madhabau yake
 
Back
Top Bottom