Mathayo 7:21-23Unauliza swali kama uko dunia nyingine vile! Kwani nyinyi manojiita walokole mnaishi wapi mpaka tushindwe kuyaona matendo yenu ya uzinzi?
sheri zipi hizo ?Kwa kifupi: Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu – ni kuvunja au kupuuza sheria au mapenzi ya Mungu.
1 Yohana 3:4
"Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria."
Biblia inaeleza vizuri Mungu anapenda tufanye nini katika maisha yetu. Tuenende namna gani ili tumpendeze. Tukienda kinyume na anavyotaka, Mungu anahesabu tumefanya dhambi.
nasoma ila wewe sikuelewi maana unaongea tofauti kabisa na kilicho ongelewa humoUsiibe, usizini, usiue, usiseme uongo...hizo ni baadhi tu ya sheria. Ina maana wewe husomi kabisa Biblia?
Hawana jipya hawa wameshiba mahindi mabichi hawawez kukujibHii inamtofautisha vp mlokole na Mroma wa kawaida ambae jana alienda kuungama dhambi zake na anamkriri Yesu kuwa ndo mwokozi wake?
Pia ili mtu aweze kuyafanya hayo maana yake ni kwamba awe amaefikia umri wa kuanza kutambua jema na baya, kutambua uwepo wa Mungu n.k mtoto chini ya miaka miwili (just mfano) hana sifa hizo za utambuzi, je akifa katika umri huo mafikio yake yanakuwa ni wapi? Jehanamu ama?
Mkuu Yesu alikuja kwa kazi gani duniani?Kihalisia tu huwezi kuokoka ukiwa hapa duniani, acha kujihesabia haki subiri upite kwenye chujio
Hakuna kuokoka. Ni uzwazwa tu. Huwezi kuokoka ukaendelea kuomba. Waliokoka wapo makaburini hawa ni bangi tu.Kama umekuwa ukijiuliza maswali kama hayo, leo ni siku yako ya kujua maana ya kuokoka na pengine ndiyo siku yako na wewe ya kuokoka.
Kuokoka ni neno tu la kawaida la Kiswahili lenye maana ya kusalimika au kunusurika kutoka katika janga, maafa makubwa au hatari yoyote inayokuijia. Mfano mzuri ni ile ndege iliyoangukia katika ziwa Victoria. Abiria katika ndege ile walikuwa katika hatari ya kufa maji; lakini alitokea kijana mmoja fundi sana wa kuogelea, akawasalimisha abiria wengi. Hapo tunasema fundi huyo wa kuogelea, aliwaokoa abiria; wakanusurika kufa maji. Kwahiyo abiria waliokolewa au waliokoka.
Kwanini sasa “walokole” wanasema wameokoka? Wamenusurika kutoka katika maafa gani?
Iko hivi: Baada ya Adam na Eva kufanya dhambi, wanadamu wote wanazaliwa wakiwa na asili ya dhambi na hivyo kujikuta wanatenda dhambi(Rum 5:12). Ndiyo sababu kwa mfano, mama akimnyima ziwa mtoto wake mchanga, anakasirika na kumpiga kofi mama. Jiulize hasira hiyo ameitoa wapi mtoto? Au je ni nani aliyemfundisha kupiga? Hiyo ni dhambi ya asili. Kwa asili hiyo kila mtu anahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi hata kama hafanyi uzinzi, haibi, au kusema uongo. Kwa sababu hiyohiyo mtu hata akijitahidi kutenda mema, bado tu anahesabiwa mkosaji, kutokana na asili yake ya dhambi(Ayu 9:29-31).
Mshahara wa dhambi ni kutupwa katika ziwa la moto milele (Rum 6:23; Ufu 21:8). Kuwapa maskini sadaka, kusali mara saba kwa siku, kipaimara, au tendo lolote jema la kidini, haliwezi kumfanya mtu anusurike kupata adhabu hiyo ya moto wa milele kwa sababu ya dhambi ya asili iliyomo ndani yake.
Ili unusurike au uokoke kutoka katika adhabu hiyo ya moto wa milele, ni lazima uhesabiwe haki na Mungu mwenyewe. Haki hiyo haipatikani kwa kushika sabato, kufanya sakramenti au kushika nguzo za kidini.
Haki hiyo inapatikana kwa kutubu dhambi zako na kuamua kuziacha kabisa na kumpokea Yesu Kristo moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukifanya hivyo, unasamehewa dhambi zako na kuokolewa (Mit 28:13; Mdo 3:19, Rum 10:10).
Kwahiyo ukitubu dhambi zako sasa hivi na kumwamini Yesu, utasamehewa na hapo tutasema umeokoka; yaani umenusurika kutupwa motoni na badala yake, umepata neema ya kuingia mbinguni. Kwa lugha nyingine tutasema “umezaliwa mara ya pili.”
Naamini umeelewa sasa kuokoka ni nini.
Mimi nimeokoka. Je, na wewe unapenda kuokoka leo? Naamini unapenda kwa sababu hakuna mtu anayependa kwenda jehanam, katika moto wa milele. Basi, kama unapenda kuokoka, omba(fuatisha) sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kukuokoa sasa hivi:
Omba hivi:, “Mungu Baba, asante kwa kunifundisha maana ya kuokoka. Nimetambua mimi ni mwenye dhambi kwa asili. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo, ili ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya katika maisha ya wokovu. Ubarikiwe sana!
Wewe unajitofautisha vipi na magugu ikiwa wote mnaishi katika dunia iliyojaa vishawishi vya kutenda dhambi?Leta ushahidi. Umeniona wapi nafanya uzinzi.
Nikose kuingia mbinguni kwenye raha ya milele kwa ajili ya uchafu huo?
Halafu ujue, sio kila mtu anayejiita mlokole ameokoka kweli. Inawezekana hao uliowaona wakifanya uzinzi ni "magugu" Siku ya mwisho, ngano na magugu vitatenganishwa. Magugu yatachomwa moto
Amina, ubarikiwe sana.Kama umekuwa ukijiuliza maswali kama hayo, leo ni siku yako ya kujua maana ya kuokoka na pengine ndiyo siku yako na wewe ya kuokoka.
Kuokoka ni neno tu la kawaida la Kiswahili lenye maana ya kusalimika au kunusurika kutoka katika janga, maafa makubwa au hatari yoyote inayokuijia. Mfano mzuri ni ile ndege iliyoangukia katika ziwa Victoria. Abiria katika ndege ile walikuwa katika hatari ya kufa maji; lakini alitokea kijana mmoja fundi sana wa kuogelea, akawasalimisha abiria wengi. Hapo tunasema fundi huyo wa kuogelea, aliwaokoa abiria; wakanusurika kufa maji. Kwahiyo abiria waliokolewa au waliokoka.
Kwanini sasa “walokole” wanasema wameokoka? Wamenusurika kutoka katika maafa gani?
Iko hivi: Baada ya Adam na Eva kufanya dhambi, wanadamu wote wanazaliwa wakiwa na asili ya dhambi na hivyo kujikuta wanatenda dhambi(Rum 5:12). Ndiyo sababu kwa mfano, mama akimnyima ziwa mtoto wake mchanga, anakasirika na kumpiga kofi mama. Jiulize hasira hiyo ameitoa wapi mtoto? Au je ni nani aliyemfundisha kupiga? Hiyo ni dhambi ya asili. Kwa asili hiyo kila mtu anahesabiwa kuwa ni mwenye dhambi hata kama hafanyi uzinzi, haibi, au kusema uongo. Kwa sababu hiyohiyo mtu hata akijitahidi kutenda mema, bado tu anahesabiwa mkosaji, kutokana na asili yake ya dhambi(Ayu 9:29-31).
Mshahara wa dhambi ni kutupwa katika ziwa la moto milele (Rum 6:23; Ufu 21:8). Kuwapa maskini sadaka, kusali mara saba kwa siku, kipaimara, au tendo lolote jema la kidini, haliwezi kumfanya mtu anusurike kupata adhabu hiyo ya moto wa milele kwa sababu ya dhambi ya asili iliyomo ndani yake.
Ili unusurike au uokoke kutoka katika adhabu hiyo ya moto wa milele, ni lazima uhesabiwe haki na Mungu mwenyewe. Haki hiyo haipatikani kwa kushika sabato, kufanya sakramenti au kushika nguzo za kidini.
Haki hiyo inapatikana kwa kutubu dhambi zako na kuamua kuziacha kabisa na kumpokea Yesu Kristo moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukifanya hivyo, unasamehewa dhambi zako na kuokolewa (Mit 28:13; Mdo 3:19, Rum 10:10).
Kwahiyo ukitubu dhambi zako sasa hivi na kumwamini Yesu, utasamehewa na hapo tutasema umeokoka; yaani umenusurika kutupwa motoni na badala yake, umepata neema ya kuingia mbinguni. Kwa lugha nyingine tutasema “umezaliwa mara ya pili.”
Naamini umeelewa sasa kuokoka ni nini.
Mimi nimeokoka. Je, na wewe unapenda kuokoka leo? Naamini unapenda kwa sababu hakuna mtu anayependa kwenda jehanam, katika moto wa milele. Basi, kama unapenda kuokoka, omba(fuatisha) sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kukuokoa sasa hivi:
Omba hivi:, “Mungu Baba, asante kwa kunifundisha maana ya kuokoka. Nimetambua mimi ni mwenye dhambi kwa asili. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo, ili ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya katika maisha ya wokovu. Ubarikiwe sana!
Yesu pia pamoja na kwamba hajawahi kutenda dhambi, aliomba, kila siku, na alituasa tusiache kuomba. Mungu akusaidie kwa sababu background yako inaonyesha haukukuzwa kwenye mambo ya Mungu kabisa kama haujui hata hili. nadhani ushakuwa mtu mzima sasa, jipambanie, fanya uamuzi binafsi wa kutafuta kumjua Mungu na njia zake sahihi, kwani usipofanya hivyo ni wewe binafsi utakuja kuhukumiwa. Mungu akusaidie.Hakuna kuokoka. Ni uzwazwa tu. Huwezi kuokoka ukaendelea kuomba. Waliokoka wapo makaburini hawa ni bangi tu.
ajabu yake wewe unayeamini hakuna kuokoka, akili yako imetekwa na shetani, hata hiyo IQ haipo kabisa na haujuikama haipo kwako.Yeyote anaedai ameokoka basi IQ yake ipo chini sana.
hujaelewa alichoandika. pia, ulishawahi kusoma sehemu inayosema aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa? pia MATENDO 2:47 inayosema "Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa" have you ever read those areas?Hakuna wokovu hapa duniani. Hivyo tuache kudanganyana.
kwa hiyo ukiambiwa ukweli kwamba uache dhambi uokoke, hupendi kukosolewa, unakimbilia kusema unahukumiwa? hata Yesu alitukanwa hivyo hivyo na alikosoa hivyohivyo, na watu kama wewe walikuwepo tangu zamani, na waliangamia hata baada ya kuambiwa ukweli na kushupaza shingo zao. Mungu akusaidie ujue ukweli pengine utapona.Unafiki mtupu!
Hakuna watu wanafiki na wanaopenda kuhukumu watu wengine kama hawa.