Lakini Yesu alisema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokokaKuokoka kunahusiana na kumwamini Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yako.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele(Yohana 3:16).
Hivi mkuu maisha ya dhambi ndiyo maisha gani hayo ?Kuokoka ni kuachana na dhambi
Mtu aliyeokoka anaacha kabisa maisha ya dhambi na kuanza kutembea katika utakatifu.
"Basi tubuni, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana." (Matendo 3:19)
Maisha ya dhambi ni maisha yanayofuata matakwa au tamaa za mwili badala ya kufuata mapenzi ya Mungu. Yaani, ni maisha ambayo mtu anaishi bila kujali sheria na mapenzi ya Mungu. Mtu ambaye haoni tatizo kusema uongo, kuzini, kunywa pombe... huyo anaishi masha ya dhambi.Hivi mkuu maisha ya dhambi ndiyo maisha gani hayo ?
Unapotubu dhambi unakiri kwamba umekosea na hutarudia tena dhambi. Kwa maana hiyo ukitubu na kuokoka, dhambi ulizotenda nyuma zote zinafutwa. Kuanzia hapo hupaswi kurudia tena matendo ya dhambi uliyoyaacha. Ndio sababu Paulo anawaambia waliokuwa wezi kabla hawajaokoka, wasiibe tena:Nieleweshe na hii ,hivi tunaacha dhambi au dhambi zinafutwa tu ?
Leta ushahidi. Umeniona wapi nafanya uzinzi.Walokole nyinyi ni wanafiki tu. Tusidanganyane hapa. Hakuna dhambi mnaifanya kwa kiwango cha juu kama dhambi ya kuzini/uasherati wa kimya kimya!
Ni kweli Mathayo 24:13 inasema, ‘mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.’ Lakini andiko hilo halimaanishi kwamba hakuna kuokoka sasa, bali linaonyesha umuhimu wa kudumu katika imani hadi mwisho wa maisha au hadi Yesu atakaporudi. Ukikata tamaa njiani badala ya kuvumilia mateso na udhia, unapoteza wokovu.Lakini Yesu alisema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka
Mathayo 24v13
Au mwisho umekwishafika?
🤝Amen. Asante kwa kusoma; ubarikiwe pia wewe sanaaa
Hizo kauli ni janjajanja tu ya shetani kuwashawishi watu wasiokoke na kufaidi baraka za wokovu.Mlokole Ni Mtu aliyethirika akili kutokana na uraibu WA dini ya kikristo
Mtu akiujua ukweli hawezi kubaki kwenye kanisa ambalo anaona lina matapeli wauza chumvi na mafutaCharacteristics za mlokole
(Ana hamahama makanisa ovyo)
Sio dhambi kuabudu kwa sauti kubwa. Mungu aliyetuumba ndiye aliyetupa uwezo wa kuongea kwa sauti kubwa. So, kama mtu anajisikia vizuri akiabudu kwa sauti kubwa usimzuie.2. Anatabia ya kufoka foka sana anapoabudu.
Nani amekudanganya. Hakuna mchawi anayeweza kumroga mtu aliyeokoka kwelikweli.3. Anaamini matatzo yake yote yanasababishwa na KUROGWA.
Walokole mnaposeema mmeokoka maana yake ni kwamba hakikisha unatenda dhambi na mtu asijue hasa dhambi ya kuzini.Kuokoka ni kuzaliwa upya kiroho.
"Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu." (Yohana 3:3)
Ulishawahi kuwa mlokole ukawa mzinzi? Au umeamua kuropoka tuu?Walokole nyinyi ni wanafiki tu. Tusidanganyane hapa. Hakuna dhambi mnaifanya kwa kiwango cha juu kama dhambi ya kuzini/uasherati wa kimya kimya! Hamna wokovu wowote ule, zaidi ya unafiki.
Hayo ni mawazo yako. Ukimficha mtu utamficha na Mungu asijue?Walokole mnaposeema mmeokoka maana yake ni kwamba hakikisha unatenda dhambi na mtu asijue hasa dhambi ya kuzini.
Hao wanaoshindana hawajui MaandikoZaidi ya yote, hasa kwa wanawake na vijana, kuokoka siku hizi ni katrend maana ulokole siku hizi unakwenda na fashion na mapastor wanashidnana kuonyesha nani mwenye fedha na nayekula bata kuliko mwenzake, ova.