Uchaguzi 2020 Kuomba kura kwa ukabila CCM hii imezidi. Msukuma awaambia wana Geita kwa kisukuma mnamwachaje mtoto wenu mnachagua asiye wa kwenu

Ukisikia kubomoa paa la nyumba ili ujenge mlango ndiko huku...., tunapandikiza chuki na ukabila...

Kazi kubwa aliyofanya Mwalimu ya kutuunganisha inaharibiwa leo...., kwa manufaa ya nani... (who knows); ila definitely not Tanzania...
Mwl Nyerere alisha sema kabisa kuwa ukiona mwana siasa anatumia kigezo cha ukabila basi jua kuwa as mefilisika kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waache wapande tu hiyo mbegu, watakuja kuvuna wanachokipanda
 
Endelea kutetea wasukhuma wenzako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuanzia sasa na kuendelea, nimejilidhisha pasipo Shaka kuwa, wewe ni miongoni mwa watu wajingawajinga Sana hapa, nimekuwa nikifuatilia namna ya hoja na michango yako, mingine ni ya kijinga mno

Labda huwa unaazimwa kiandikio anatumia mwingine, lakini kama ni wewe mwenyewe, ni mtu mjinga Sana wewe
 
Ni kawaida, kule nimewahi kuishi, kuna wazee kule hawajiu Kiswahili hata cha kuombea maji tu,
Acha Tu mkuu waombwe Kura Kwa lugha Yao ileile!! Na nadhani hakuna ubaya Ila tu mtizamo tu ulionao wewe
Unamaanisha watangulizi wake hawakwenda kuomba kura uko kisa lugha gongana!?
 
Hao wavuvi wanapaswa kukumbuka kuwa mwasisi wa tabia za kuchoma nyavu zao ndiye huyohuyo anayewaomba kura hadi kwa kilugha! Nakumbuka alimwambia waziri wa uvuvi na mifugo Luaga Mpina akasema .....Mpina wewe ni kichaa mwenzangu endelea! Hii ilikuwa kumtaka Mpina kuendelea kuchoma nyavu za wavuvi hao bila kujali wanazipata kwa jasho kiasi gani na je ni changamoto zipi zinafanya washindwe kupata vibali vya kuvulia hao samaki!
 
Hotuba zote zipitiwe ili kwa kutumia wasukuma walioko upinzani tafsiri ya chochote kilichosemwa kwa kisukuma ipatikane na kuwekwa hadharani
 
Kilichofanyikaga pale singida mh Lisu akiongea na Wanyaturu kilikuwa ni Kiswahili kweli kile?

Sheria za uchaguzi zinataka kiswahili tu ndio kitumike. Hiyo siku Lisu alikuwa kwenye kampeni? Isitoshe hata kama Lisu aliongea kinyaturu, nani alimsifia kwa huo upuuzi?
 
Sheria za uchaguzi zinataka kiswahili tu ndio kitumike. Hiyo siku Lisu alikuwa kwenye kampeni? Isitoshe hata kama Lisu aliongea kinyaturu, nani alimsifia kwa huo upuuzi?
Mkuu,Ndiyo maana huwa nakwambiaga kwamba, kuvunjiana heshima sio Jambo la Afya hata kidogo, Hadi naamua kujiunga humu, awali nilikuwa ni msomaji mzuri wa michango ya watu hapa JF, na tayari Hadi najiunga Jf, kuna watu ambao tayari nilikuwa nawakubali na kuwaheshimu, ni pamoja na wewe mkuu,

Mfano hapo ulichoongea ni umeamua kuinyima nafs yako ukweli,

Hembu nikuulize, unaposema kwamba,Lisu aliongea ki Lugha kule kwao eti si Wakati wa kuomba Kura na hakuvunja Kanuni za uchaguzi, Je Kanuni za uchaguzi huanzia kipindi kipi, ni kipindi chote tangu kuomba wadhamini au ni Wakati wa Kampeni pekee?
 
Wasukuma tunachafuliwa na upumbavu wa watu wachache
 
Haya ndiyo baadhi ya mambo ambayo Mwalimu aliyakataa kabisa!!
 
Ni Kanuni ngapi mpaka sasa zimevunjwa na wagombea mkuu na bado wanaachwa?
Kwa hiyo kimsingi unakubali kuvunjwa kwa kanuni ila unashangaa kuwa kanuni nyingi zimevunjwa na wagombea na hatua hazijachukuliwa?
 
Nyerere:"Hatumchagui mtu kuwa Rais kwa kabila lake wala dini yake"!

Magufuli:"Nichagueni mimi msukuma mwenzenu,mtoto wa nyumbani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…