Mkuu,Ndiyo maana huwa nakwambiaga kwamba, kuvunjiana heshima sio Jambo la Afya hata kidogo, Hadi naamua kujiunga humu, awali nilikuwa ni msomaji mzuri wa michango ya watu hapa JF, na tayari Hadi najiunga Jf, kuna watu ambao tayari nilikuwa nawakubali na kuwaheshimu, ni pamoja na wewe mkuu,
Mfano hapo ulichoongea ni umeamua kuinyima nafs yako ukweli,
Hembu nikuulize, unaposema kwamba,Lisu aliongea ki Lugha kule kwao eti si Wakati wa kuomba Kura na hakuvunja Kanuni za uchaguzi, Je Kanuni za uchaguzi huanzia kipindi kipi, ni kipindi chote tangu kuomba wadhamini au ni Wakati wa Kampeni pekee?