Sidhani kama unachofurahia kinaweza kupunguza maumivu yako,,Fei toto kuondoka sio big issue kwa yanga hii,,inategemea ameondokaje,,kama ameondoka vizuri kiroho safi ataenda kufanikiwa uko alikoenda lakini kama ameondoka vibaya kwa kuwavimbia viongozi na kujiona amefikia kilele cha utukufu basi safari yake ya mafanikio inakwenda kuishia Azam,,siongei hiki kwa kubahatisha bali naongea kwa mifano hai,,Mnamkumbuka mchezaji alikuwa anaitwa Frank domayo,uyu aliondoka yanga akiwa on fire na yanga awakutaka kumuachia lakini aliwagomea kusaini mkataba mpya licha ya juhudi kubwa kufanyika akaenda kusaini Azam akiwaacha viongozi wa yanga midomo wazi kwa kiwango alichokuwa nacho kipindi icho alikuwa tegemeo,,lakini alivyoondoka kilichofata kinajulikana habari yake iliishia Azam, Mwingine aliyeondoka vibaya ni gadiel michael na sasa kinachomkuta uko alipo kila mtu ni shahidi, Mwingine ni Ibrahim ajibu anachokipitia kila mtu anakijua, kwaiyo suala sio fei toto anaenda azam suala ni ameondokaje, kwa sababu pamoja na umuhimu wake kwenye kikosi lakini yanga haiwezi kutetereka sababu ya fei toto kutokana na kikosi walichonacho kwa sasa sio wa kutegemea mchezaji mmoja,,ishu ni namna ya uondokaji wa mlengwa na ninachoona ameondoka kibabe kwa kuvunja mkataba wake wakati klabu bado ina mkataba nae na bado inamhitaji,,Yanga ni Taasisi kubwa haiwezi kuyumba sababu ya mchezaji mmoja na kama anaondoka basi viongozi watakuja na tamko rasmi