Kuondoka kwa Majeshi ya Marekani Nchi Afghanistan kumewaachia maafa makubwa wananchi

Kuondoka kwa Majeshi ya Marekani Nchi Afghanistan kumewaachia maafa makubwa wananchi

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Ni huzuni kweli kweli,nimeona taarifa ya BBC ikionesha mateso wanayopata Raia wa Afghanistan kutokana na vita Kati ya Taleban na Majeshi ya Serikali.

Watu Wana njaa,wanauwawa na Wana majeraha ya risasi na mabomu.Marekani wamekosea Sana kuondoka huku wakijua jeshi la Nchi ni dhaifu.Matokeo yake ni ombwe la kugombea madaraka huku Taleban wakionekana kuizidi serikali.

Ni vyema Umoja wa Mataifa uangalie jinsi ya kuwasidia Hawa watu hasa watoto, wanawake, wazee na walemavu. Ukizaliwa kwenye amani hadi ukazeeka na kufa kwenye amani mshukuru Mungu maana unaweza kutana na janga ukiwa Mzee, mgonjwa au mtoto.
 
Ni huzuni kweli kweli,nimeona taarifa ya BBC ikionesha mateso wanayopata Raia wa Afghanistan kutokana na vita Kati ya Taleban na Majeshi ya Serikali...

Humvee za jeshi ya USA zilizotekwa na wa TALEBAN, zinatumika kusafirisha abiria wa ki AFGHAN huko vijijini.

FB_IMG_1625714875845.jpg
 
Waafghan ni wapenda vita. Namna pekee ya kupata amani ni kuwaacha Wataleban watawale ili Shariah itamalaki maana ndicho wanachotaka. Wenye kukatwa miguu au mkono wakatwe na wenye kupigwa mawe wapigwe.

Hakika Shariah ikitamalaki Afganistan itatulia tuli kama mtungi wa maji na wale wenye kupenda utawala wa kidini wanaweza hata kuhamia huko ili kujitenga na watenda dhambi wa dunia. Afghanistan chini ya Taleban itakuwa kama Peponi.
 
Marekani hata wakiweka majeshi yao milele huko Afghanistan hawataweza kuwamaliza au kuwazima Wataliban wala amani haiwezi kupatikana. Miaka 20 ni mingi sana kwa malengo ya kivita. Imebidi waondoke tu wawaachie wenye nchi watimize “wajibu wao”.

Taliban ni movement kubwa. Wanadai wanapigana vita ya kidini ya jihad ili kuifanya Afghanistan kuwa Islamic Emirate. Huwezi kuua movement kama hiyo kwa vita. Kwao kifo si lolote wala chochote. Wapiganaji wao wako tayari kufa hata 100 na zaidi ili kuua askari 1 tu wa Marekani! Asymmetrical warfare!

Ukweli ni kuwa Wanashamiri Afghanistan kwa vile wana support kubwa ya ndani na nje ya nchi; ya kitaifa na kidini. Awali Warusi walijaribu kuwang’oa watangulizi wao, MUJAHIDEEN, lakini walinyosha mikono juu na kukimbia. Hata ukiua laki ngapi hawaishi na moto ni ule ule. Labda mje nchi nzima.

Marekani wamekuwa na hali ngumu. Wanaonekana zaidi kama wavamizi tena makafiri. Nayo serikali ya kisekula ya Kabul inaonekana kama kibaraka wa Marekani. Wamekuwa wakihangaika kuzima hujuma muda mwingi. Tabu yote ya nini? Walishatahadharishwa na Warusi tangu awali wasithubutu kuweka lengo la kuikalia Afghanistan kwa muda mrefu eti ili “kuinyoosha”; wataondoka kwa aibu. Labda uue watu wote nchi nzima.

Afghanistan lazima ipitie moto ndipo ijielewe kama ni taifa moja au vipi; kama inataka kuwa taifa la kidini au kisekula; n.k. Dunia nzima mataifa imara huko Ulaya, Marekani na Asia yamepitia moto hadi kujibainisha kitaifa. Mengine bado moto unaendelea. Hakuna shortcut. Ndio asili ya kusikitisha ya binadamu. Heshima huja baada ya upanga. Ukitaka amani ya kweli jiandae kwa vita. Majeshi ya kigeni hayawezi kuwajengea utaifa.

Lengo rasmi la Marekani lilikuwa kuwafurusha Al Qaeda toka Afghanistan na kumuangamiza Osama bin Laden. Walitakiwa wawe wameondoka siku nyingi lakini kwa ujinga wakajidai watakaa kuinyoosha nchi hiyo wakifikiri wanakubalika sana kwa Waafghanistan wengi. Hatimaye, wameondoka kwa aibu kama walivyosema Warusi. Imagine siku ya mwisho kuondoka Bagram Air Base walitimka usiku bila kuaga.
 
Back
Top Bottom