Kuondoka kwa mamluki ni faraja kubwa kwa CHADEMA. Zifanyike jitihada waondoke wote

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Siku zote, mamluki au wasaliti ndani ya taasisi yoyote ile ni ufa mbaya, na ni sumu kwa maendeleo ya taasisi hiyo.

Bila shaka, waliofuatilia kikao cha Kigaila na wenzake, na wanahabari tarehe 7 May 2025, alisikia hoja za ajabu za watu hao. Watu hao waliongea uwongo mwingi kama vile hakuna watu wanaojua ukweli.

Watu hawa, waliowadanganya wanaowafanyia kazi kuwa wana uwezo wa kuiparanganisha CHADEMA. Hapo jama walishindwa kuusema ukweli kuwa wao ni kakikundi kadogo sana ndani ya CHADEMA, na hakawakilishi waliokuwa wagombea wa 2020 wala watia nia wa 2025, ambao wote kwa uwingi wao, walihudhuria kikao kilichoandaliwa na chama, na wote kwa umoja wao waliunga mkono azimio na msimamo wa chama wa No Refirms No Election. Hawa wasaliti, walipoitwa na chama ili watoe hoja yao, walikimbia, hakuna hata mmoja aliyejitokeza, badala yake walikimbilia kwa wanahabari.

Hawa watu wamejidhihirisha wazi. Kwa kutambua kuwa walikuwa sehemu ya kamati tendaji ya chama, wanatoa jibu kwa nini CHADEMA, licha ya kuungwa mkono na wananchi wengi, haikuwahi kufanikiwa kuisumbua CCM.

Hii inadhihirisha, kwa kipindi chote, wapinzani wa CHADEMA imewatumia watu hawa wenye uchu na tamaa ya malipo binafsi kuzorotesha kila hatua ya mapambano. Fikiria kuwa, ni hawa watu, ile pesa ya ruzuku ilipotolewa tu, cha kwanza, waligawana wao, eti kufidia kipindi chote cha huko nyuma ambacho hawakupata malipo kamili. Kwa sasa, baada ya kuondolewa kwenye ulaji waliokuwa wakiupata (kwa gharama ya maumivu ya wengi), wanahangaika kutafuta chimbo jingine la mafao.

Kuondoka kwa hawa watu, kwa CHADEMA, ni jambo la faraja kubwa, na ni hatua kubwa kuelekea mafanikio. Siku zote timu ya watu 10 wenye dhamira moja ni imara maradufu kuliko kundi la watu 20 lenye maadui wa ndani 2.

Hawa mamluki, kwa kadiri ya mpango ulioandaliwa hawawezi kwenda CCM, kwa sababu, baada ya kushindwa ndani ya CHADEMA, wanatakiwa kwenda chama bandia kitakachopewa nguvu na dola ili kitumike kwa mambo kadhaa, mojawapo ni kuonesha Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi.

Ukweli Halisi.
Ahadi waliyoambiwa ya kupewa viti vichache vya ubunge, inaweza kuishia hewani, endapo itaonekana wazi kuwa mbinu hiyo haipunguzi nguvu ya CHADEMA. Watatelekezwa, na mwisho wao lazima utakuwa wa aibu kubwa.
 
Hawakuwa na maslahi tena hapo chamani, Siasa ni maslahi, futa hayo maslahi kama hawajabaki wawili.

TAL anajadiliwa na bunge la ulaya. Hayo ni maslahi, ukiyafuta na yeye anaachana na hizo habari.

Wabunge kibao wapo hapo bungeni ni maslahi. Waambie bungeni mshahara ni laki tano bila marupurupu ushuhudie.

Siasa ni maslahi, utofauti ni kiwango cha tamaa.
 
Wenye hoja Mbadala wanasikilizwa au wanaitwa Mamluki?
 
Chama kinasafishika kweli. Hii ni dalili njema kuwa Watanzania wanapata watetezi wao wa kweli na sio madalali wanaotaka kuwatumia kama ngazi kufanikisha malengo yao ya kujineemesha binafsi.
 
Siasa ni maslahi, futa hayo maslahi kama hawajabaki wawili. TAL anajadiliwa na bunge la ulaya. Hayo ni maslahi, ukiyafuta na yeye anaachana na hizo habari, wabunge kibao wapo hapo bungeni ni maslahi. Waambie bungeni mshahara ni laki tano bila marupurupu ushuhudie.
Tundu Lissu angekuwa ana maslahi binafsi asingepigwa risasi na kupata ulemavu wa kudumu.

Mkiongelea siasa zenu za kidalali usimuweke kabisa mkombozi wa kweli wa Watanzania Tundu Lissu.
 
Maslahi si lazima yatoke serikali ya nchi yako. Unaweza pata maslahi nje ili kupigana na serikali ya nchi yako na ukaingia vitani na viongozi wa nchi yako. Bila kujali ni kupigania haki au dhulma ila lazma wanaosapoti mapigano yako wakupe maslahi yako kulinda maslahi yao.

Binadamu ni binadamu. TAL hajadiliwi na bunge la ulaya sababu ulaya wanampenda sana, ni maslahi ya watu wa ulaya waliyonayo Tanzania. Na sio jambo jipya, Nyerere mwenyewe aliwahi kuwa na maslahi na nchi za ulaya na wamewahi kumlinda.
 
Siku zote, mamluki au wasaliti ndani ya taasisi yoyote ile ni ufa mbaya, na ni sumu kwa maendeleo ya taasisi hiyo.

Bila shaka, waliofuatilia kikao cha Kigaila na wenzake, na wanahabari tarehe 7 May 2025, alisikia hoja za ajabu za watu hao. Watu hao waliongea uwongo mwingi kama vile hakuna watu wanaojua ukweli.

Watu hawa, waliowadanganya wanaowafanyia kazi kuwa wana uwezo wa kuiparanganisha CHADEMA. Hapo jama walishindwa kuusema ukweli kuwa wao ni kakikundi kadogo sana ndani ya CHADEMA, na hakawakilishi waliokuwa wagombea wa 2020 wala watia nia wa 2025, ambao wote kwa uwingi wao, walihudhuria kikao kilichoandaliwa na chama, na wote kwa umoja wao waliunga mkono azimio na msimamo wa chama wa No Refirms No Election. Hawa wasaliti, walipoitwa na chama ili watoe hoja yao, walikimbia, hakuna hata mmoja aliyejitokeza, badala yake walikimbilia kwa wanahabari.

Hawa watu wamejidhihirisha wazi. Kwa kutambua kuwa walikuwa sehemu ya kamati tendaji ya chama, wanatoa jibu kwa nini CHADEMA, licha ya kuungwa mkono na wananchi wengi, haikuwahi kufanikiwa kuisumbua CCM.

Hii inadhihirisha, kwa kipindi chote, wapinzani wa CHADEMA imewatumia watu hawa wenye uchu na tamaa ya malipo binafsi kuzorotesha kila hatua ya mapambano. Fikiria kuwa, ni hawa watu, ile pesa ya ruzuku ilipotolewa tu, cha kwanza, waligawana wao, eti kufidia kipindi chote cha huko nyuma ambacho hawakupata malipo kamili. Kwa sasa, baada ya kuondolewa kwenye ulaji waliokuwa wakiupata (kwa gharama ya maumivu ya wengi), wanahangaika kutafuta chimbo jingine la mafao.

Kuondoka kwa hawa watu, kwa CHADEMA, ni jambo la faraja kubwa, na ni hatua kubwa kuelekea mafanikio. Siku zote timu ya watu 10 wenye dhamira moja ni imara maradufu kuliko kundi la watu 20 lenye maadui wa ndani 2.

Hawa mamluki, kwa kadiri ya mpango ulioandaliwa hawawezi kwenda CCM, kwa sababu, baada ya kushindwa ndani ya CHADEMA, wanatakiwa kwenda chama bandia kitakachopewa nguvu na dola ili kitumike kwa mambo kadhaa, mojawapo ni kuonesha Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi.

Ukweli Halisi.
Ahadi waliyoambiwa ya kupewa viti vichache vya ubunge, inaweza kuishia hewani, endapo itaonekana wazi kuwa mbinu hiyo haipunguzi nguvu ya CHADEMA. Watatelekezwa, na mwisho wao lazima utakuwa wa aibu kubwa.
CHADEMA bado liko imara ebu wamwachie Lissu uone vumbi lake na dola ikae pembeni. Hawa jamaa walikwisha aminika na wananchi na wanaendelea kuaminika wanaoondoka ni sehemu ndogo ya kujisafisha na kujenga kuaminika zaidi. wako vizuri
 
Maslahi si lazima yatoke serikali ya nchi yako. Unaweza pata maslahi nje ili kupigana na serikali ya nchi yako na ukaingia vitani na viongozi wa nchi yako. Bila kujali ni kupigania haki au dhulma ila lazma wanaosapoti mapigano yako wakupe maslahi yako kulinda maslahi yao.

Binadamu ni binadamu. TAL hajadiliwi na bunge la ulaya sababu ulaya wanampenda sana, ni maslahi ya watu wa ulaya waliyonayo Tanzania. Na sio jambo jipya, Nyerere mwenyewe aliwahi kuwa na maslahi na nchi za ulaya na wamewahi kumlinda.
Hizo propaganda za kijinga jilishe wewe na wajinga wenzako huko CCM
 
U
Hawakuwa na maslahi tena hapo chamani, Siasa ni maslahi, futa hayo maslahi kama hawajabaki wawili.

TAL anajadiliwa na bunge la ulaya. Hayo ni maslahi, ukiyafuta na yeye anaachana na hizo habari.

Wabunge kibao wapo hapo bungeni ni maslahi. Waambie bungeni mshahara ni laki tano bila marupurupu ushuhudie.

Siasa ni maslahi, utofauti ni kiwango cha tamaa.
Umejibu vyema sana. Uzalendo wanao wananchi wa kawaida ila mwanasiasa ni maslahi ndo anatafuta.
 
Back
Top Bottom