Kuongea kilugha jukwaani ni kutamani ukabila

Kuongea kilugha jukwaani ni kutamani ukabila

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Sikumbuki ni lini Mwl. Nyerere alihutubia taifa kwenye jukwaa na mbele ya kamera kwa kuchanganya na Kizanaki, na wala sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi wala Mkapa wakifanya hivyo wala watu wao. Waliamini kuwa kwa kufanya hivyo ni kutamani siasa za ukabila na kufukua hisia za kikabila nchini.

Nimewahi kumuona Mh. Shibuda juzijuzi akiongea Kisukuma kitupu wakati alipopewa nafasi ya kusalimia kwenye mkutano ambao ulikuwa wa public ambao pia ulikuwa unafuatiliwa na hata watu wasiofahamu lugha ya Kisukuma na bila kupewa onyo.

Wasiwasi wangu ni watu kuutamani mtaji wa kikabila ambao Nyerere alisema ni dalili za mtu kufilisika kisiasa.

Hebu turudini kwenye mstari aliouacha baba wa taifa.
 
Magufuli amefika mbali zaidi sio tu kuongea kisukuma bali kuwatukana wapiga kura wake kwa kisukuma majuzi akiwa Tabora alisikika akisema 'Mkatolwe' akimanisha watu wote wakaolewe waume kwa wake ili waepuke maisha magumu ilikuwa ni kauli ya ovyo sana kutoka kwa JPM.
 
Ukabila sasa rasmi tz kutokana na kuongozwa na mtu mkabila kwa mawazo, maneno na vitendo
 
Sikumbuki ni lini Mwl. Nyerere alihutubia taifa kwenye jukwaa na mbele ya kamera kwa kuchanganya na Kizanaki, na wala sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi wala Mkapa wakifanya hivyo wala watu wao. WAliamini kuwa kwa kufanya hivyo ni kutamani siasa za ukabila na kufukua hisia za kikabila nchini.

Nimewahi kumuona Mh. Shibuda juzijuzi akiongea Kisukuma kitupu wakati alipopewa nafasi ya kusalimia kwenye mkutano ambao ulikuwa wa public ambao pia ulikuwa unafuatiliwa na hata watu wasiofahamu lugha ya Kisukuma na bila kupewa onyo.

Wasiwasi wangu ni watu kuutamani mtaji wa kikabila ambao Nyerere alisema ni dalili za mtu kufilisika kisiasa.

Hebu turudini kwenye mstari aliouacha baba wa taifa.
I'd like to disagree, or to differ, kuongea kilugha ni kudumisha mila!.

Tena kwa kukusaidia tuu, kanuni za kampeni zinakataza kuhutubia kwa lugha za kikabila.
Tembelea hapa ushuhudie wakabila wakihutubia kikabila tena kwenye kampeni rasmi ambapo kukampeni kikabila hakuruhusiwi na watu walikampeni kikabila and no one said anything.


Hivyo msitake kumlaumu Shibuda, Wasukuma when exited, ili kuonyesha furaha yao, huongea Kisukuma. Pale Shibuda was exited so much!.

P
 
..hakuanza akiwa raisi.

..alianza akiwa waziri ktk kampeni za uchaguzi mdogo nadhani ilikuwa jimbo la busanda.

..sasa wako radhi kuvunja mwiko wowote ule ili mradi kupata kura.

..kama UKABILA utawasaidia kupata kura watautumia.

..kama UDINI utawasaidia kushinda uchaguzi watautumia.

..hata UKATILI/ MAUAJI / UNYAMA kwao ni ruksa ili mradi washinde uchaguzi.
 
Huhuru. Kenyata mwenyewe Akiwa anahutubia kwao huwa anaongea kiruga ivyo si jambo geni

Sent using Jamii Forums mobile app
Je,huyo Uhuru Kenyatta ndiyo rode model wenu?Ukabila wa nchi yetu unatengenezwa kimkakati kama sehemu ya kampeni.Wameshasema kura za Kanda ya Ziwa zinatosha kumpa Urais wa Tanzania,ndiyo maana wanalazimisha miradi mikubwa isiyo na tija kanda pendwa.
 
Hawa watu wanataka tuwaelewe kwamba ni wakabila na hivyo ndivyo wanavyojipambanua kuwa ndivyo walivyo.

Uzuri ni kwamba hawawezi tena kututumbukiza kwenye athari za ukabila, kwa sababu uwezo huo hawana.

Wapinzani inafaa waanze kulisemea hili jambo watu walielewe vizuri.
 
Sio CCM, hata Wapinzani nao kuna saa wanaanguka kwenye hili, inakera sana
Hawa watu wanataka tuwaelewe kwamba ni wakabila na hivyo ndivyo wanavyojipambanua kuwa ndivyo walivyo.

Uzuri ni kwamba hawawezi tena kututumbukiza kwenye athari za ukabila, kwa sababu uwezo huo hawana.

Wapinzani inafaa waanze kulisemea hili jambo watu walielewe vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani alikwambia mtu kuongea kilugha ni ukabila? Wewe una makamasi kichwani siyo bure.Hakuna raha kama kuongea kilugha,kama Cha kwenu hukijui piga chini kaa kimya.Kuna kikabila fulani Cha kaskazini utakuta watu wake hawajui hata kilugha Cha kwao lakini wanakumbatia sana ukabila na kila mtanzania anawajua na hata wenyewe wanalijua hilo.Acha watu waongee cha kwao,*****
 
Huhuru. Kenyata mwenyewe Akiwa anahutubia kwao huwa anaongea kiruga ivyo si jambo geni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kenya wanatafunwa na ukabila, mtaji wa Uhuru ni kura za wakikuyu. Je na sisi ndio tuelekee huko? Wasukuma ni wakikuyu wa Kenya Kwa wingi. Hivyo ukipata kura za wasukuma wote lazima utawashinda wapinzani wako
 
Kwani lugha ziliumbwa za nini kama haturuhusiwi kuzitumia, halafu Magufuli huongea lugha nyingi za Tanzania, ni genius.
 
Back
Top Bottom