Kuongea kilugha jukwaani ni kutamani ukabila

Kuongea kilugha jukwaani ni kutamani ukabila

Wasukuma ni wakikuyu wa Kenya Kwa wingi. Hivyo ukipata kura za wasukuma wote lazima utawashinda wapinzani wako

Kuna profesori juzi kati amesema kura za kiongozi mnene zipo ziwa kubwa kwingine kote wanajaziajazia, huyo ni msomi wa ngazi ya juu kabisa ama kweli bora njaa ya tumbo kuliko njaa ya kichwa!!!
 
Kasoro ki English ndio kinapita kushoto tuu!!!

Cha nini hicho, ki English ni lugha ya watu wa mataifa ya mbali, tukomae kwenye lugha zetu za hapa hapa, piga Kisukuma, Kinyamwezi, Kiswahili kwa raha zako.
Mchina, Mwarabu au hata Muingereza akija mpe mkalimani, mbona mtaendana tu.
 
Kwani lugha ziliumbwa za nini kama haturuhusiwi kuzitumia, halafu Magufuli huongea lugha nyingi za Tanzania, ni genius.
Kama tunamheshimu Nyerere basi tumheshimu kabisa. Unapozungunza na
Hawa watu wanataka tuwaelewe kwamba ni wakabila na hivyo ndivyo wanavyojipambanua kuwa ndivyo walivyo.

Uzuri ni kwamba hawawezi tena kututumbukiza kwenye athari za ukabila, kwa sababu uwezo huo hawana.

Wapinzani inafaa waanze kulisemea hili jambo watu walielewe vizuri.
Kwani sababu hasa za wao kuongoea kilugha ilihali wakijua kuwa sio wote wanaowasikiliza ni kabila moja ni nini?

Wanataka kupata faida/maslahi gani kwa wao kuongea kilugha mahali pale?

Wanataka kupeleka ujumbe gani ambao hautafika kwa lugha ya kiswahili (cha wote)?

Wanataka kuwaficha nini wengine?

Je, wanaowahutubia hawajui Kiswahili?
Je, wanaohutubia hawajui Kiswahili?

Dhamira yao ni nini?

Je, na viongozi wengine pia waongee kilugha wanapowahutubia na kuwahudumia watu wa vitongoji, vijiji, kata, tarafa, wilaya, majimbo, mikoa na hata wizara zao? Tunaelekea wapi?

Mwl Nyerere (RIP) hakulipenda hili pamoja na udini, na rushwa kwa viongozi wetu.
 
Kuna profesori juzi kati amesema kura za kiongozi mnene zipo ziwa kubwa kwingine kote wanajaziajazia, huyo ni msomi wa ngazi ya juu kabisa ama kweli bora njaa ya tumbo kuliko njaa ya kichwa!!!
Nyerere kuna watu ambao hakutamani wawe viongozi hasa kutokana na hurka na mila zao
 
Sikumbuki ni lini Mwl. Nyerere alihutubia taifa kwenye jukwaa na mbele ya kamera kwa kuchanganya na Kizanaki, na wala sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi wala Mkapa wakifanya hivyo wala watu wao. WAliamini kuwa kwa kufanya hivyo ni kutamani siasa za ukabila na kufukua hisia za kikabila nchini.

Nimewahi kumuona Mh. Shibuda juzijuzi akiongea Kisukuma kitupu wakati alipopewa nafasi ya kusalimia kwenye mkutano ambao ulikuwa wa public ambao pia ulikuwa unafuatiliwa na hata watu wasiofahamu lugha ya Kisukuma na bila kupewa onyo.

Wasiwasi wangu ni watu kuutamani mtaji wa kikabila ambao Nyerere alisema ni dalili za mtu kufilisika kisiasa.

Hebu turudini kwenye mstari aliouacha baba wa taifa.
Tuna Rais wa ajabu haijawahi tokea by TL
 
Pascal Mayalla,
kati ya watu wa jf wanaojielewa nilizani na wewe umo, hivi kila kiongozi akitaka kuongea kilugha chake wakati anasikilizwa na makabila mbalimbali hali itakuwaje? unasema wasukuma uonyesha furaha yao kwa kuongea kisukuma, kwani alikuwa anaongea na familia yake?
 
I'd like to disagree, or to differ, kuongea kilugha ni kudumisha mila!.

Tena kwa kukusaidia tuu, kanuni za kampeni zinakataza kuhutubia kwa lugha za kikabila.
Tembelea hapa ushuhudie wakabila wakihutubia kikabila tena kwenye kampeni rasmi ambapo kukampeni kikabila hakuruhusiwi na watu walikampeni kikabila and no one said anything.


Hivyo msitake kumlaumu Shibuda, Wasukuma when exited, ili kuonyesha furaha yao, huongea Kisukuma. Pale Shibuda was exited so much!.

P
Hiki ni kingereza au sijaelewa mh p mayala,na siku hz unavyokula makombo,sishangai,yaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tunamheshimu Nyerere basi tumheshimu kabisa. Unapozungunza na

Kwani sababu hasa za wao kuongoea kilugha ilihali wakijua kuwa sio wote wanaowasikiliza ni kabila moja ni nini?

Wanataka kupata faida/maslahi gani kwa wao kuongea kilugha mahali pale?

Wanataka kupeleka ujumbe gani ambao hautafika kwa lugha ya kiswahili (cha wote)?

Wanataka kuwaficha nini wengine?

Je, wanaowahutubia hawajui Kiswahili?
Je, wanaohutubia hawajui Kiswahili?

Dhamira yao ni nini?

Je, na viongozi wengine pia waongee kilugha wanapowahutubia na kuwahudumia watu wa vitongoji, vijiji, kata, tarafa, wilaya, majimbo, mikoa na hata wizara zao? Tunaelekea wapi?

Mwl Nyerere (RIP) hakulipenda hili pamoja na udini, na rushwa kwa viongozi wetu.
Kati ya vitu ambavyo Mwl.Nyerere alitukosea ni kukataza watu kuenzi kabila lao ,utamaduni wao la lugha zao. Ili alikua tofauti na mawazo ya wakoloni. Mimi nafurai sana kutumia lugha mama aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani alikwambia mtu kuongea kilugha ni ukabila? Wewe una makamasi kichwani siyo bure.Hakuna raha kama kuongea kilugha,kama Cha kwenu hukijui piga chini kaa kimya.Kuna kikabila fulani Cha kaskazini utakuta watu wake hawajui hata kilugha Cha kwao lakini wanakumbatia sana ukabila na kila mtanzania anawajua na hata wenyewe wanalijua hilo.Acha watu waongee cha kwao,*****
Nchi imekabidhiwa washamba wala haishangazi. Waliosema maneno hayo walikuwa sahihi.
 
Nani alikwambia mtu kuongea kilugha ni ukabila? Wewe una makamasi kichwani siyo bure.Hakuna raha kama kuongea kilugha,kama Cha kwenu hukijui piga chini kaa kimya.Kuna kikabila fulani Cha kaskazini utakuta watu wake hawajui hata kilugha Cha kwao lakini wanakumbatia sana ukabila na kila mtanzania anawajua na hata wenyewe wanalijua hilo.Acha watu waongee cha kwao,*****
Wa Kaskazini waliamka wakati wewe umelala. Wivu hautakusaidia. Nape mwenyewe anajua kuwa washamba na malimbukeni ndio wamekabidhiwa nchi.
 
Yako makabila ambayo yangetamani lugha yao ingekuwa ndiyo lugha ya Taifa, huwa wanamlaumu Nyerere kwa kukikumbatia Kiswahili.

Na huo ndio ugomvi wa Ethiopia kumlaum HaileRas kuifanya Amharic lugha ya kikabila kidogo (Amhara) kilichostaarabika kuwa Lugha ya Taifa na kuziacha lugha za makabila makubwa Ethiopia.
 
Kama tunamheshimu Nyerere basi tumheshimu kabisa. Unapozungunza na

Kwani sababu hasa za wao kuongoea kilugha ilihali wakijua kuwa sio wote wanaowasikiliza ni kabila moja ni nini?

Wanataka kupata faida/maslahi gani kwa wao kuongea kilugha mahali pale?

Wanataka kupeleka ujumbe gani ambao hautafika kwa lugha ya kiswahili (cha wote)?

Wanataka kuwaficha nini wengine?

Je, wanaowahutubia hawajui Kiswahili?
Je, wanaohutubia hawajui Kiswahili?

Dhamira yao ni nini?

Je, na viongozi wengine pia waongee kilugha wanapowahutubia na kuwahudumia watu wa vitongoji, vijiji, kata, tarafa, wilaya, majimbo, mikoa na hata wizara zao? Tunaelekea wapi?

Mwl Nyerere (RIP) hakulipenda hili pamoja na udini, na rushwa kwa viongozi wetu.
Hii ni dalili moja iliyo wazi, pamoja na mengine kwamba tuna 'mtawala' mbovu kabisa.
 
Je,huyo Uhuru Kenyatta ndiyo rode model wenu?Ukabila wa nchi yetu unatengenezwa kimkakati kama sehemu ya kampeni.Wameshasema kura za Kanda ya Ziwa zinatosha kumpa Urais wa Tanzania,ndiyo maana wanalazimisha miradi mikubwa isiyo na tija kanda pendwa.
Mradi upi hauna tija? Sababu unaongea vapours tu.
 
Back
Top Bottom