Kuongea kilugha jukwaani ni kutamani ukabila

Cha nini hicho, ki English ni lugha ya watu wa mataifa ya mbali, tukomae kwenye lugha zetu za hapa hapa, piga Kisukuma, Kinyamwezi, Kiswahili kwa raha zako.
Mchina, Mwarabu au hata Muingereza akija mpe mkalimani, mbona mtaendana tu.
Halafu kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu ni kiingereza, inaelekea ulipofika darasa la saba ukagoma kuendelea na masomo maana huko ni kimombo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huhuru. Kenyata mwenyewe Akiwa anahutubia kwao huwa anaongea kiruga ivyo si jambo geni

Sent using Jamii Forums mobile app
Bw Ibrahim, kenya wanapiga kura kikabila, hata ukiwa kiziwi na kipofu lakini kabila lako likiamrishwa na wazee na machifu basi watakupifia kura. Jee tunakaribisha kura za kilabila?

Kenya Governor wa Central hawezi kuwa Mjaluo lazima awe mkikuyu , Ridt Valley Mkalenjin, Nyanza Mjaluo, North Eastern Msomalo, Ukambani Mkamba nk...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
One should not correct a mistake with a mistake
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alitumia maneno mengi ya kabila - kung'atuka, Nyabusabusa burwero ne kiriro kirimbura! Na mengine mengi. Ni kwamba wewe umekuwa kiziwi na kipofu kwa chuki binafsi kwa Raisi wetu.
 
Nyerere alitumia maneno mengi ya kabila - kung'atuka, Nyabusabusa burwero ne kiriro kirimbura! Na mengine mengi. Ni kwamba wewe umekuwa kiziwi na kipofu kwa chuki binafsi kwa Raisi wetu.
Nyerere alikuwa anatumia au ku quote maneno ya lugha za kienyeji ili kukoleza na kusisitiza uzuri au ubaya wa kitu au taarifa kwenye sentensi za kiswahili baada ya kukosa neno lenye uzito sawa na kile anachokimaanisha kwenye kiswali, lakini alikuwa haongei Kizanaki
 
Mwl. Nyerere: "....Na tuliweka sheria. Tukasema, mtoa rushwa na mpokea rushwa; Wazanaki tunasema; wote maziganyanga....!" Mwisho wa kunukuu.
 
Mwl. Nyerere: "....Na tuliweka sheria. Tukasema, mtoa rushwa na mpokea rushwa; Wazanaki tunasema; wote maziganyanga....!" Mwisho wa kunukuu.
Yaani ameazima neno la kizanaki kwenye hotuba yake kwakuwa neno maziganyanga lilikuwa na uzito wa kipekee kwake, na pia akafafanua maana ya neno hilo akasema wote wako kwenye msukosuko
 
Hata hii ya kusalimia kidini mara sijui Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristu, huu ni udini tu!
 
Yaani ameazima neno la kizanaki kwenye hotuba yake kwakuwa neno maziganyanga lilikuwa na uzito wa kipekee kwake, na pia akafafanua maana ya neno hilo akasema wote wako kwenye msukosuko
Na alitoa tafsiri palepale.
Mwenzetu huyu mwingine analonga kisukuma tu, wakielewa wasukuma inatosha!
 
Yaani ameazima neno la kizanaki kwenye hotuba yake kwakuwa neno maziganyanga lilikuwa na uzito wa kipekee kwake, na pia akafafanua maana ya neno hilo akasema wote wako kwenye msukosuko
Dogo unaatoa hoja halafu unajaribu kuitetea bila mafanikio. Tanzania hatuna ukabila. Kuongea kilugha kwa namna yoyote ni kunogesha stori tu. Wataalamu wa 'Public Speech' wanalijua hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…