Kuongeza bei za data, lengo ni kuibana internet isifikie wengi au ni kuota ndoto kwamba wananchi wana pesa za mchezo kununua mabando

Kuongeza bei za data, lengo ni kuibana internet isifikie wengi au ni kuota ndoto kwamba wananchi wana pesa za mchezo kununua mabando

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Miezi michahe iliyopita hili jambo lilipigiwa kelele sana pale mitandao yote kwa mpigo iliposhinikizwa kubadili bei zao kutokana na mabadiliko kadhaa ya sheria.

Kiukweli kisu kiligonga mfupa na wananchi kelele zao zilikita kila kona na mpaka raisi akaingilia kati.

kwa sasa ndani ya miezi miwili hii tumesuhudia mitandao ilikuwa inapokezana vijiti kupandisha bei, wakipandisha huku wananchi tulihamia kule na huku, haikuwa kwa mpigo ila haba na haba hujaza kibaba na sasa lengo limetimia huku waanchi tukiwa hatuna mbadala.

sasa nashindwa kuelewa hapa, je lngo ni kuibana internet isifikie watu wengi au labda kuna kikao cha mameneja wa wizara husika wanaolipwa mamilioni wakadhani kwamba kwa kuwa wao wana uweo wa kumudu vifurshi basu wakachukuia na wananchi wana pesa za mchezo kulipia haya mabando?

Aibu ilioje hii.
 
Halotel nao wahuni sana😏
Kile kifurushi cha Royal Week ilopita ulikua ukijiunga unapata GB 7 per 30days ila sasa hvi unapata GB 6, bado sms n dk wamezipunguza😏
 
Nasikia kuna mtandao wa Azam wenye bando za kitanzania, hivi umeishia wapi ?
 
Halafu mbona kama wote bei ziko sawa, ni kama wameplan iwe hivyo, naona mpaka sasa serikali iko kimya
 
Hat kifurushi cha usiku jamani tulichokuwa tuna download na kesho yake kuamka macho mekundu nacho kimefumuliwa vibaya vibaya...haya majitu ya v -8 yana roho mbaya sana , hkayamungu
 
Ni kuminya watu wasitumie internet kujifunz mambo. Wabaki wajinga
 
Data Tanzania bado ni cheap.

Ndio mana utakuta page instagram imeandikwa wema sepetu fans ina wafuasi milioni.

Hii ni kuonyesha kwamba data ziko cheap na watu hawana shughuli ya kufanya wanashinda mtandaoni wanapiga umbea.

Nashauri GB 1 ya data iwe angalau kuanzia 5k au zaidi.
 
Back
Top Bottom