Kuongezeka kwa matukio ya mauaji na mmonyoko wa maadili ni kielelezo cha kushindwa kwa taasisi za dini

Kuongezeka kwa matukio ya mauaji na mmonyoko wa maadili ni kielelezo cha kushindwa kwa taasisi za dini

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa kidini na kimila kuwa chanzo cha kudhibiti mauaji yanayotokea mara kwa mara nchini, kwa kutoa mafunzo ya maadili yatakayosaidia kurejesha utu na hofu ya Mungu.

Ameyasema hayo leo Februari 22 alipohutunia katika maadhimisho ya miaka 25 ya Jubilee ya Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi yaliyofanyika wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.

Amesema wilaya ya Ngara kwa mwaka 2022 kulikuwa na matukio ya kuuawa na kujiua 22 huku mwaka 2021 kukiwa na matukio 21, akisema visababishi ni pamoja na wivu wa mapenzi, tamaa ya mali, imani za kishirikina, msongo wa mawazo na ugomvi wa kifamilia.

"Anayetia uhai na kutoa uhai ni Mungu pekee sasa sina uhakika wanaojiua au kuua wenzao kuwa ni kazi ya Mungu, hivyo viongozi wa dini na mila mna kazi ya kufanya kama ulivyosema Baba Askofu (Niwemugizi) kuwa umeshaianza kuwa kuitisha kikao kati ya viongozi wa dini, mila na serikali katika wilaya yenu," amesema Samia.

Rais Samia amesema serikali itatumia somo la uraia kupandikiza hofu ya Mungu na uzalendo kwa wanafunzi ili wawe mstari wa mbele kupambana na mauaji hayo.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo, Askofu Niwemugizi amesema licha ya kuwepo kwa juhudi za kupambana na mauaji hayo, lakini zimejikita kwenye matokeo ya tatizo badala ya kutafuta chanzo.

Amewataka viongozi wa dini kulaani matukio ya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu huku akiwatahadharisha viongozi wa dini kutonyamaza kwani kufanya hivyo kutaifanya ghazabu ya Mungu kunyanyuka.

Amesema matukio hayo yanatia doa katika taifa hivyo yanatakiwa kulaaniwa na kila mtanzania.

"Viongozi wa dini tukinyamaza, ghadhabu ya Mungu itaamka, mambo ya hovyo yanatendeka na sisi hatusemi, wanaotenda mabaya lazima tuwashauri na tuwaonye ili waishi vizuri," amesema Niwemugizi
 
Dini imeshindwaje, kwa mfano? Asimilia kubwa wanaoporomoka huko kimaadili huwa meikataa dini kwa hiari na bidii yao wenyewe.

What's the difference, na mtu mhalifu anayesingizia kwamba sheria dhidi ya wahalifu ndiyo imeshindwa kazi yake?

Hivi unataka dini iingie mwilini mwako ibadili vinasaba vya DNA ili waikubali dini na kuyafuata maadili by default, au? GIVE RELIGION SOME BREAK!
 
Tungeanza kwenye malezi ngazi za familia, Kuna kipindi nilikuwa naishi sehemu fulani, malezi ya watoto mahali hapo ni ya hovyo sana, Watoto umri chini ya miaka mi5 saa3 usiku wapo nje wa kike kwa wakiume, unategemea nini hapo! Tatizo linanzia chini huku watu wamejizila
 
Chanzo cha kuwepo na dini na hii inahusu dini zote zikiwenu hizi zilizokuja na meli na zile za asili ni
  1. hofu ya kisichojulikana- ukuu wa Mungu
  2. maadili- amri na sheria za dini mfano zile amri 10
  3. kufarijisha hasa wenye vurugu za maono, sonona na msongo wa mawazo
  4. ujira-afanyae kazi hekaluni hulia hekaluni
Angali kabla Yesu hajaondoka hapa alijumuisha amri zote na kupata amri mmoja UPENDO. Na wakati anaondoka alitutuachia amani- AMANI IWE NANYI. Amani ndiyo msingi wa Uislam dini nyingine iliyokUja baada ya Yesu kuondoka.
Kwa kuzingatia hayo hapo juu- dini haziwezi kukwepa kubeba lawana kwa haya yanayotokea kwenye jamii. Wawajibike.
 
Tungeanza kwenye malezi ngazi za familia, Kuna kipindi nilikuwa naishi sehemu fulani, malezi ya watoto mahali hapo ni ya hovyo sana, Watoto umri chini ya miaka mi5 saa3 usiku wapo nje wa kike kwa wakiume, unategemea nini hapo! Tatizo linanzia chini huku watu wamejizila
SAWA NAKUUNGA MKONO
 
Viongozi wa dini wameacha kazi zao asilimia kubwa wamebaki tu kuhubiri sio kujitenga na kuomba

Wengi ukiwauliza mara ya mwisho kuomba Mungu ukiwa peke yako kuombea nchi au waumini wako atakwambia sikumbuki mwisho lini

Yesu alikuwa akiomba sana yeye peke yake

Hawa wa sasa wanachukulia tu kama ajira wapate tu maisha

Raisi yuko sahihi.Maadili yameporomoka kuanzia ndani ya dini.Viongozi wengi hawana maadili na si waombaji ni wapiga mikelele tu makanisani na siasa
 
Mauaji yapo tokea enzi na enzi. Sema enzi hii kupatikana kwa habari kumekuwa rahisi via social media. Tena huenda hata yamepungua.
 
Back
Top Bottom