Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?

Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?

Sijui ni nn mm mwenyewe mpaka nimejiuliza mfano ni mdogo tu kutoka kigamboni ferry pale mpaka kigamboni darajani kuna vituo vya mafuta hata kumi na usheee sehem ambayo si zaid ya km 8 lakini ina vituo kumi na ushee na eneo hilo ndio kuna makazi ya watu pia matank ya reserv ila ndo kuna vituo vya mafuta km vyote.
Watu wana tktish pesa tu
We fungua kituo mambo mengine
Jiongeze

Ova
 
Kama sababu ni za kibiashara then inatakiwa waachwe soko litaamua. Huwezi kumzuia mtu kuanzisha biashara eti kwa kigezi kuwa tayari kuna biashara kama hiyo pembeni yake. Acha wapambani kibiashara soko litaamua nani atasurvive.
Hoja ya kupinga nafikiri iwe ya kiusalama zaidi kuliko kibiashara.
Kama vile ukitaka kufingua hotel mtaa fulani, manispaa haipaswi kukuzuia kwa kigezo kuwa tayari kuna hotel nyingine ipo mtaa huo. Soko huria.
Hoja iwe ya KITAALUMA zaidi.
Mpangilio wa Miji, TOWN PLANNING, uliisha fanyika na kuidhinishwa na Mamlaka husika, kwa nini Wafanyakazi wa Idara/Wizara ya Ardhi wanarudi kuubadilisha?
Hili ndilo tatizo.
Na kichocheo ni RUSHWA.
Suluhu ni kuyafuta MABADILIKO yote yanayofanywa na Idara ya Ardhi.
Ramani za awali ziheshimiwe.
 
ni kuombea kusitokee mlipuko mana kupambana na uwo moto itakuwa ngumu.

bongo hapa mipango miji tunafeli pakubwa.. bado najiuliza ata wale waliojenga ile DART main depot pale jangwani ;walikuwa wanawaza nini vichwani mwao!
 
Vp kile cha jkt mlalakuwa vepe

Ova
Kile kiko sawa kabisa kuanzia eneo hadi position maana hakuna kituo hadi Mikocheni Nyerere, Hakuna Kituo hadi Stendi ya Kawe, Hakuna kituo hadi Total MbeziBeach
 
Kile kiko sawa kabisa kuanzia eneo hadi position maana hakuna kituo hadi Mikocheni Nyerere, Hakuna Kituo hadi Stendi ya Kawe, Hakuna kituo hadi Total MbeziBeach
Maringo pale kona vp hakuna kituo kinachojengwa pale
Ila pale jkt majirani walitaka kuanza kupinga uwepo wa kituo hicho anyway
Sjui walimalizana vp

Ova
 
ni kuombea kusitokee mlipuko mana kupambana na uwo moto itakuwa ngumu.

bongo hapa mipango miji tunafeli pakubwa.. bado najiuliza ata wale waliojenga ile DART main depot pale jangwani ;walikuwa wanawaza nini vichwani mwao!
Maafa makubwa yakitokea ndiyo akili
Huwa inakaaa sawa

Ova
 
Hivi vituo vilitakiwa vijengwe nje ya mji vijitenge na makazi ya watu. Kuna mji mmoja barabara kuu vituo vya mafuta vimejengwa vinakaribiana mita chachache kutoka kimoja hadi kingina na vyote vipo kwenye makazi ya watu
Hiyo ni energy source, huwezi kujitenga nayo, mwenye hii mada haelewi Dunia inakwenda wapi, kinachotakiwa ni safety standards na Sio kuzuia makazi ya Watu na Watu SI ndio watumiaji!? Fikiria maduka ya gesi Si ndio hatarishi Zaidi ila yapo vyumbani mwa Watu
 
Hivi vituo vilitakiwa vijengwe nje ya mji vijitenge na makazi ya watu. Kuna mji mmoja barabara kuu vituo vya mafuta vimejengwa vinakaribiana mita chachache kutoka kimoja hadi kingina na vyote vipo kwenye makazi ya watu
Wenye magari tupo mjini sasa kwanini kituo kijengwe nje ya mji? Kufa kupo tuu acha uoga.
 
Sijui ni nn mm mwenyewe mpaka nimejiuliza mfano ni mdogo tu kutoka kigamboni ferry pale mpaka kigamboni darajani kuna vituo vya mafuta hata kumi na usheee sehem ambayo si zaid ya km 8 lakini ina vituo kumi na ushee na eneo hilo ndio kuna makazi ya watu pia matank ya reserv ila ndo kuna vituo vya mafuta km vyote.
Wewe shida Yako ni nini, tra hawachukua Kodi huko!? Acha wivu na biashara za Watu
 
Hilo la Moro ulishuhudia au ulihadithiwa mbona hatujawahi kulisikia, usiwe umechanganya tukio la lori la mafuta lililopata ajali na moto ukasababishwa na bodaboda wezi wa mafuta, na ajali kama hiyo ilitokea Mbeya pia.
Naona umekurupuka kujibu bila kusoma, kuelewa na kutafakari. Uhusiano hapo ni idadi ya vifo vinavyoweza kutokea kwenye majanga ya mafuta na moto.

Soma elewa, urikurupuke na kuropoka Mkuu
 
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?

Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani? Sijui kwanini haifikirii?

Nakumbuka Septemba 2022, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula aliagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa majengo yanayojengwa kinyume cha sheria na kuondolewa vituo vya mafuta vilivyojengwa kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kutozingatia umbali. Alitaka wabadilishe umbali wa kutoka mita 200 hadi mita 500 wa kituo kimoja kwenda kingine.

Aidha, Novemba 10, 2022, Waziri Mabula alisema Serikali imesitisha ujenzi wa vituo vya mafuta ili kutoa nafasi ya kufanya tathimini ya ujenzi wa vituo hivyo kufuatia ongezeko la ujenzi holela wa vituo hivyo

Lakini pia, mnamo Aprili 2023, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango aliagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kufanya ukaguzi wa kina juu ya vituo vya mafuta vinavyojengwa kwa wingi kwenye makazi ya watu mkoani Dar es Salaam ili kunusuru kusitokee majanga ya moto.

Pamoja na matamko yote hayo, Serikali imedhiirisha kuwa ya matamko kwani hakuna kilichoendelea wala kufanyika

Mfano Kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe pale Tanganyika Packers ni hatarishi kweli kweli iwapo kutatokea mlipuko au madhara ni makubwa sana

Bado kuna Kituo kingine kimejengwa Mikochenk karibu na makazi ya Watu ambacho kimelamikiwa hadi na Mwanasiasa nguli, Prof. Anna Tibaijuka ila bado Serikali hii ipo kimya.

Huenda inangoja yatokee yale ya ajali ya moto wa mafuta kama kule Morogoro ndio wanashughulikia na kuweka sana pale ambapo Watanzania watakuwa na huzuni kubwa ya kupoteza Ndugu, Jamaa na Marafiki.

View attachment 2850297
Ramani kuonesha Kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe

Je, Serikali inasubiri hadi majanga yatokee na tupate maafa kama ya Morogoro kwenye ajali ya mafuta ili kuchukua hatua?

Natambua Waziri wa Ardhi wa sasa, Jerry Silaa amechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa maendeleo ya makazi, Deogratius Kaliminze ila hiyo haitoshi kabisa, mara nyingi sana hii hutokea na hakuna cha maana kinafanyika. Inadaiwa huyu mtu vituo kadhaa ni vyake kupitia syndicate aliyoitengeneza.

Soma: Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi
Hivyo vituo vingi vya mafuta vina mkono wa viongozi wa serekali, fedha hizi ni zile fedha zetu za miradi kama hospital, shule nk.
 
Back
Top Bottom