Utitiri wa Vituo vya Mafuta ni hoja ya KIBIASHARA zaidi kuliko ya KIUSALAMA.
Haiingii akilini kuwa uhitaji wa Petroli na Dizeli umekuwa mkubwa sana kiasi cha kutakiwa uongezekaji wa Vituo, tena karibu karibu kama tunavyoona jijini Dar es Salaam.
Tatizo la usalama kuhofia KULIPUKA MOTO kwenye Vituo vya Mafuta ni dogo sana kwa sababu Mafuta yaliyohifadhiwa chini ardhini ndani ya Matenki ni salama zaidi kuliko Galoni ya Mafuta ya Taa iliyohifadhiwa ndani ya Nyumba zetu.
Chupa ya Mafuta ya Taa nyumbani ni hatari zaidi KIUSALAMA maana Mafuta yanakutana na hewa ya Oksijeni kiurahisi zaidi.
Kama ilivyo kwenye "Sheli za Pikipiki" ambazo zimesambaa sana kwenye maeneo yetu ya Makazi kuhudumia Bodaboda.
Ni vema kufahamu kwamba Petroli na Dizeli, vyenyewe, HAIWAKI/HAILIPUKI mpaka ikutane na hewa ya OXYGEN.
Kama Bomba za Chuma zinazoleta Mafuta kutoka kwenye Matanki chini ya Ardhi kupeleka kwenye Pampu za kujazia Mafuta kwenye Magari HAZIVUJI, uwezekano wa MLIPUKO wa Moto unakuwa haupo.
Lakini kitu muhimu cha kujiuliza ni iwapo kuna umuhimu wa kuwa na Vituo vingi vya Mafuta kwa kiasi tunachoona.
Ni sawa na kujenga Soko kila Mtaa.
Watu wa Mipango Miji wanaoruhusu hali hii wameonyesha UDHAIFU mkubwa wa KITAALUMA.
Na UDHAIFU huo unachochowa na RUSHWA.
Biashara ya Mafuta ni biashara ya pesa nyingi.