Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2019
Posts
15,954
Reaction score
35,415
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho?

Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.

Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.

Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto?
 
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho!??

Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.

Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.

Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto??

Jana tu nimeota hii ndogo
 
MALIPO ni hapa hapa duniani watafute uliwaibia 🖋️ , kifutio, kichongeo shule ya msingi kisha waombe msamaha usipofanga hivyo vyeti vyako vyote vitaungua mizimu ya kwenu insongea na wewe 🤪
😀😀😀 Mkuu mi sikua mwizi wa peni tu advance nikwida sana vitabu.

Wacha niwatafute niwalipe aisee.
 
Hiyo hali hata mimi ninayo sana, kila mara naota nipo shule. Ila kwa muono wangu naona labda kwa sababu tangu nimemaliza shule life langu halijatulia, msoto mkali so pengine subconsciously ubongo unakuwa unajaribu kunipa relief kwa kunikumbusha moments za shule kwa sababu hicho ndo kipindi sikuwa na changamoto nyingi za kimaisha au pengine ubongo kifikra unatamani siku zirudi nyuma ili nibaki kuwa mtoto kama sehemu ya kutafuta solution ya hali ya sasa.

Naona ni kama nafsi ipo kwenye denial state kuhusu hali ya sasa.

Still fighting.
 
I feel you bro, Keep the fight On [emoji123]
 
Na mimi huwa naota pia , tena naota nafanya pepa gumu sioni hata swali la kujibu, au naota nimechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani, nilishawahi kuota sina calculator hivo nikashindwa kusolve maswali kabisa na huwa roho inauma hadi nikishtuka hivi kwamba ilikua ni ndoto ndiyo nashukuru na kupata amani, sijui ni nini tafsiri yake 🤔
 
Back
Top Bottom