Kwa ufahamu wangu: Ndoto za shule ni ndoto zinazosignify Retrogression Spirit. Roho ya kurudishwa nyuma, kunakuwa hakuna progress katika eneo flani la maisha yako au pia maisha yako kwa ujumla. Unakuta unaanza hili mara linakufa, mara aumwe mtu ile hela uitoe ikamtibie, mara msiba, mara kaja mcheps ukahonga au akakuibia, mara uibiwe na majambazi. Au ni kazini mara ufukuzwe, usimamishwe. Au ni kiwanja chako mara kiuzwe mara mbili basi ilimradi ukwame.
Na hii spirit inaoriginate from various places, mojawapo being generational curses. Baadhi yetu tunapenda sana kufanya ibada kwa mizimu tunasema tunaona wazee au kuaga kwenu kumbe unakabidhiwa huko kwenye hizo madhabahu. Mara ya kwanza utaona unafanikiwa and all but kiuhalisia kiroho ndo umedidimia sana. Na mafanikio ya kweli huanzia mtu kufanikiwa rohoni kwanza ndo mwilini. Lakini kuna cases pia kwamba yumkini kuna watu ulisoma nao way back hawakuwa wazuri as in wachawi au maagent wa kuzimu. Wakakamata nyota yako, destiny yako. Na kama ulikula nao, ulishare nao chochote, ama waliiba peni yako..hili nalo ni very possible. Na pia kuna baadhi ni ardhi ulikosomea. Kuna shule zimewekewa mambo yake kwenye ardhi.
Juzi hapa kuna mtu alileta uzi wa shule za watoto wa single sex kuwa na roho za uchafuzi (tafsida). Sasa pia ardhi za shule hizi mara nyingi zinadai haya maagano yatimizwe. Uwe na uhakika watu watafanya haya. Kwanini: unakuta mtu katoka na tabia mbaya kwao huko, anaenda shule anafanya hayo madude, tayari ardhi inabeba hiyo laana. Wewe unampeleka mwanao, huombei ardhi ya shule.
Kila uchafu, laana zilizopo zitamkumba very likely. Somo ni refu sana, ninaongea from personal experience, nilikuwa affected pia. Mpaka leo ninajifanyia maombi ya deliverance. Mifungo ya kavu, Daniel fast ihusike. Its not easy but utapona tu ukiamua. Pray and mean it kuchomoka hapo.