Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Mi nilichokinyaka hapa ni kua hizi ndoto hutokea kukukumbusha ukamilishe jambo.

Nahisi kwa mimi hili ni kweli coz maisha yangu mpaka sasa yana viporo sana. Mipango kibao utekelezaji kiduchu mwisho unaacha viporo tu.

Kuhusu vita ya kurudishwa nyuma sidhani kwakweli.
 
Maisha ya elimu katika mazingira yetu ni mateso sana. Zile nyakati ngumu mtu anazopitia hujirudia kupitia ndoto. Ndio maana huwa tunatamani hizo ndoto zisiwe za kweli, hata mtu ashtukapo kutoka ndotoni hujawa na furaha pale aonapo kumbe si tukio halisi.
 
Hili tumeshalijadili sana hapa na lina tafsiri ya moja kwa moja kiroho kwamba kuna jambo/mambo uliyaanza na hujayamaliza hivyo unakumbushwa kiroho kuyamaliza

Mengine huwa ni ahadi ulizoshindwa kuzitimiza ama kumaliza, nadhiri, madeni, mipango ya maendeleo, mipango ya maisha na sometimes hata visasi
kuuuu jibu lipo hapa
 
hizi ni ndoto za kufeli maisha ukiota unashindwa kufanya mtihani mara umechelewa ujue kabisa kwamba mbele kuna vigingi vya kutosha katika maisha yako inabidi uvunje hizo ndoto kwa sala.
 
Kiongozi samahani Na pale unapoota upo njiani unaelekea shule ghafla unajikuta unamkimbiza mtu anaendesha baiskeli unajikuta umepoteza kiatu kimoja katika harakat za kumkimbiza huyo mtu basi unaghaili kwenda shule kwakua Hauna kiatu je hii inamaana Gani kiongozi?
 
Mie pia nimeota ndoto hiyo asubuhi ya leo na huwa naota mara kwa mara...... ila nilisikia kuwa ndoto za hivo zina maana ya kuwa kuna vita kubwa sana ili kusonga mbele kimaisha, yaani unarudishwa nyuma.
Ukiota umemaliza shule
 
Ondoa hofu.. Kawaida akili ya mwanadamu ina tabia ya kujikumbushia yale mambo yaliyopita wakati ukiwa umelala.

Tena inapenda kujikumbushia matukio ambayo uliyaishi kwa muda mrefu au yale uliyoyapenda sana
Sawa
 
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho!??

Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.

Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.

Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto??
Utaja kuwa Profesa.
 
Aloo ndoto hii nimeiota nimepata nipo level za juu kielimu nimepata marks za juu zaidi darasa zima linanisifia yaan weee aloo acha kabisa naogopeka km ningebaki ndotoni yaan pepa lilikua gumuuu mi ndio nimepiga gepu vibaya sana wengine wote chali

-Tafasiri ya kuona matokeo ya mtihani umepigwa mweleka au umepasua
Screenshot_20240926-063804.png


-Tafasiri ya hii ndoto wanasema anaeota atakua anayakaribia mafanikio
Screenshot_20240926-063718.png


Ninakumbuka wazee wangu waliwahi kunifundisha hata iweje ukiota ndoto yoyote iwayo ile usimwambie mtu yoyote yaan usimsimulie mtu ndoto yako uliyoota Jana kwa maana haujui yupi ni yupi na yupi ni yupi (ndoto ni siri yako wewe na Mungu wako) isipokua fanya tafasiri mwenyewe taratibu taratibu maisha ni siri usiwe mtu wa kumwambia kila mtu kila kitu na kila kitu kila mtu itakula kwako

Signature
Ambivert88
 
Naongezea kitu kidogo kuhusu ndoto ndugu yangu ukiota umelala kisha ukawa unacheka maana yake mbele yako kuna kilioo yaan aidha utaumia kwa ajali mbaya nusura kupoteza uhai wako, utagombana na mtu nusura kuua/kuuwawa au utafanya jambo lolote baya ila utaumia/utaumizwa sana

Nakushauri ukilala na mtu kisha ukamuona anacheka kwa kumsaidia mtie kofi aamke atoke kwenye hio ndoto usimuache aendelee kucheka anaota ndoto mbaya sana

Signature
Ambivert88
 
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho!??

Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.

Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.

Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto??

Mtafute Mwamposa au kuhani Mussa akupe tafsiri yake.
 
Mtu unaota
  • Umechelewa kwenye chumba cha mtihani na wenzio wameshaanza muda mrefu
  • Mtihani hauendi kwako ila kwa wengine wanafanya
  • Kufeli au kuchelewa kwenye interview
Maana yake umeshindwa au kuna jambo linakuja mbele utashindwa yaan utapigwa za uso
 
Back
Top Bottom