Kuota ndoto za shule wakati ulishamaliza shule kitambo kabisa ni jambo baya kabisa na linaashiria kurudishwa nyuma katika maisha kwa namna ya kishirikina. Hapa nilipo napambana na jambo hili kwa maombi manake nimekuwa nikiona mipango yangu mingi ikiburugika na kuchelewa. Ndoto hizi huambatana na kuchelewa katika mafanikio ya mtu kwani mtu anakuwa amerudishwa nyuma au kuwekewa stop kichawi. Shughulika sana na jambo hili ni serious problem la sivyo ni vigumu kutoka kimaisha.
Wandugu hivi hii ishu ya kuota mambo ya shule mara kwa mara huwa ina maana gani kiroho!??
Nimekua nikiota ndoto kua nipo shule eidha o'level au advance na mara chache primary na chuo ila za o'level na advance ni kama kila siku tu.
Mwanzo nilikua napuuza lakini naona sasa inakua too much, karibu kila siku naota nipo shule mara nafanya pepa, nasubiri matokeo, nipo class nasoma, napiga story na wana yani zile moments nlizokua nafanya skuli ila zinakua advanced. Kama ni pepa linaweza kua gumu sana au jepesi sana.
Kuna tafsiri yoyote juu ya hizi ndoto??
Personally naonaga kawaida, may be kazi zetu zinahusu mambo innovative, kila muda tunasoma
Hiyo hali hata mimi ninayo sana, kila mara naota nipo shule. Ila kwa muono wangu naona labda kwa sababu tangu nimemaliza shule life langu halijatulia, msoto mkali so pengine subconsciously ubongo unakuwa unajaribu kunipa relief kwa kunikumbusha moments za shule kwa sababu hicho ndo kipindi sikuwa na changamoto nyingi za kimaisha au pengine ubongo kifikra unatamani siku zirudi nyuma ili nibaki kuwa mtoto kama sehemu ya kutafuta solution ya hali ya sasa.
Naona ni kama nafsi ipo kwenye denial state kuhusu hali ya sasa.
Still fighting.
Nasubiri majibu ya hili..or assumptions juu ya ndoto za namna hii
Na mimi huwa naota pia , tena naota nafanya pepa gumu sioni hata swali la kujibu, au naota nimechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani, nilishawahi kuota sina calculator hivo nikashindwa kusolve maswali kabisa na huwa roho inauma hadi nikishtuka hivi kwamba ilikua ni ndoto ndiyo nashukuru na kupata amani, sijui ni nini tafsiri yake 🤔
Mtu unaota
- Umechelewa kwenye chumba cha mtihani na wenzio wameshaanza muda mrefu
- Mtihani hauendi kwako ila kwa wengine wanafanya
- Kufeli au kuchelewa kwenye interview