Kupanda kwa Mafuta na Hatari ya Migomo na Maandamano Nchi Nzima

Sijajua ila leo nimeletewa kale kamtung kadogo ka gesi kg 6 elf 30 ba usafir buku.imekuaje kuaje sijui. Mara ya mwisho nilibadilisha kwa elf 23
Duu mkuu unaishi mkoa Gani , kagera ?
Hali inatisha kwa kweli
 
Duuh elf 7?
Kama una ndugu umasaini huko Ngorongoro muulize atakuambia maana wale wananunua mafuta Karatu then wanayasafirisha na penyewe ni magendo maana mafuta hayatakiwi kusafirishwa kwenye madumu na kila dumu ni elfu 20 au zaidi, imqgine mfuko wa kilo 25 wa sukari unalipia elfu 15.

Kuna sehemu kule Loliondo vijijini kbs lita mafuta ni Tz 7,500.
 
Mungu wangu!, inakuwaje watu wanaishi kwa shida hivi na watu tuko
 
D yetu ya kiswahili lazima itupeleke kwenye sh 8,000/L kufikia Julai. hapa nilipo sh 5,000 inatupa 1.18L

Huko nyuma Februari, sh 3174 ilitupa lita 1.18
 
Hili ni jambo hatari, sarafu ikishuka gharama ya kuagiza mafuta inakuwa ghali
 
Tanzania imebaki kidogo maandamano kama ya Sudan yatokee
 
Ukienda kununua mafuta hauoneshi kadi ya CCM wala hausemi, Samia mitano tena. Badala yake unatakiwa ulipe kulingana na EWURA walivosema au zaidi.

Angalia mwenendo wa bei Dar:
  • Petroli: Feb TZS 2,788 → Mei TZS 4,115
  • Dizeli: Feb TZS 2,701 → Mei TZS 4,248
Ndani ya miezi mitatu petroli imepanda ~48%, dizeli ~57%.

Vita vya Mashariki ya Kati na kufungwa kwa Hormuz vimechangia, lakini tozo na kodi za serikali ndizo zinabeba mzigo mkubwa wa bei yetu. kuna tozo na kodi zaidi ya 19 zenye thamani ya zaidi ya TZS 1,113 kwa kila lita — Fuel Levy, Excise Duty, Petroleum Development Levy, Railway Development Levy, VAT, Import Declaration Fee, n.k, karibu asilimia 40 ya bei ya pampu ni tozo za serikali. Linganisha: Uganda ~26%, Ethiopia hawatozi kabisa. Ndiyo maana mwananchi anabeba mzigo wa pande mbili, bei ya dunia pamoja na tozo za nyumbani.

Mafuta yamepanda haraka kuliko nauli, hii ndio hatari zaidi na tumeshaona Wasafirashaji wakigoma na kupanga migomo na hakuna kitu rahisi kama kugoma kwenye usafirishaji.

Mgomo wa nchi nzima hauhitaji tangazo. Wamiliki wanaweza kulemaza usafiri kwa njia ngumu kuzishika kisheria:
  1. Kupunguza safari (badala ya 8, wanafanya 4)
  2. Kupunguza saa za kazi (kutoa magari asubuhi tu, au kuchelewa kuingiza magari)
  3. Kutotoa magari kwa mzunguko — nusu ya magari yanapumzika kila siku, kila baada ya siku moja
90%+ ya wakazi wa miji wanategemea usafiri wa umma, hata punguzo la nusu kwa wiki linaweza kusimamisha jiji.

Hatari kubwa zaidi — kusambaa sekta nyingine. Hapa ndipo jambo linakuwa la taifa zima. Mgomo wa usafiri ni "kibiriti" tu; mfumuko wa bei ndio "petroli."
  • Wafanyakazi wa umma (walimu, wauguzi, polisi wa chini): mishahara ni ileile, lakini nauli + chakula vimepanda. Mtumishi wa mshahara mdogo anaposhindwa kufika kazini na mshahara hauwezi kumudu maisha → madai ya nyongeza ya mshahara → migomo ya kisekta.
  • Madereva wa malori/mizigo (cargo): wakijiunga, bandari na usambazaji wa bidhaa unaganda → uhaba → bei zaidi → hasira zaidi. Hii inageuza tatizo la "mijini" kuwa la kitaifa.
  • Wakulima: dizeli ya matrekta, umwagiliaji na kusafirisha mazao sokoni inapanda → gharama za uzalishaji wa chakula zinaongezeka → mfumuko unazidi.
  • Machinga na biashara ndogo: abiria wakipungua, wateja wanapungua; pembejeo zinapanda. Hawa ni wengi na wepesi kuingia mitaani.
  • Boda boda na bajaji: tayari ni sekta ya usafiri — wakijiunga na daladala, hakuna njia mbadala iliyobaki.

Tofauti na migomo ya Madaktari Serikali imewahi kuingiza Madaktari kutoka Jeshini, ila safari hii hakuna idadi ya magari ya jeshi inaweza kupunguza aina ya mgomo huu, zaidi ni kwamba hayo magari hayatumii maji yanatumia mafuta ambayo yamepanda, hata Serikali ikisema ipunguze gharama ya mafuta kwa magari ya Jeshi bado watachochea mgomo wa Wauzaji wa mafuta, kiufupi hili swala la mafuta ni sehemu nzuri ya kuhakikisha utawala wa Samia hautawali.

Tutarajie migomo na mdororo mkubwa wa Uchumi
Hakuna mbuzi inagoma, mmeshasahau
 
Fee kwenye petrol zilikuwepo hata wakati wa Kikwete..
VAT inamsaidia muuzaji sio mnunuzi
Maana yake ni kwamba wenye vituo ndo wanafaidika zaidi
sio mwananchi kwa hiyo hakuna kilichopungua waondoe au wapunguze hizo tozo kwa miezi kadhaa ili gharama na ukali wq maisha kwa watu maskini /wanyonge upungue.
Mwanangu alienda mwezi Machi nauli ikiwa elfu 10 leo ni elfu 25. Kuna sehemu lita ya petrol inauzwa elfu 7.
Bolded text
Are you sure of what you're talking about? Course coordinator hapo umetulisha matango pori.
 
Why are you saying I'm feeding you false information?
Do your research first, then come back and prove me wrong, kama una ndugu yupo maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro hayo muulize lita ya mafuta wanauziwaje ?
Nitakutajia vijiji hapa (Iltulele, Naiyobi, Bulati, Masamburai, Osinoni, Esere, Kapenjiro)
Then utamuuliza nauli kutoka Karatu kwenda Esere,Osinoni mwezi Februari na Machi ilikua shilingi ngapi na kwa sasa Mei kwenda Juni ni shilingi ngapi?

If the information mentioned above is not true, call me the best lucifer himself.
 
Na hivi wana kisingizio mkondo wa Hormuz kazi ipo, mwizi kapata justification sababu ya mkondo tutegemee vilio zaidi
 
Why are you saying I'm feeding you false information?
Do your research first, then come back and prove me wrong, kama una ndugu yupo maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro hayo muulize lita ya mafuta wanauziwaje ?
Nitakutajia vijiji hapa (Iltulele, Naiyobi, Bulati, Masamburai, Osinoni, Esere, Kapenjiro)
Then utamuuliza nauli kutoka Karatu kwenda Esere,Osinoni mwezi Februari na Machi ilikua shilingi ngapi na kwa sasa Mei kwenda Juni ni shilingi ngapi?

If the information mentioned above is not true, call me the best lucifer himself.
Swali kwako; unawafundisha hivi huko vyuoni? Kwa ID yako inashabiana na mhadhiri wa chuo. Siko hapa kuonyesha nani ni nani zaidi kuhusu mambo ya kodi; nipo kukusahihisha tu kuwa uliyoyasema hayana ukweli wowote.

* Wauzaji hawahifadhi VAT wanayotoza. Kwa mujibu wa sheria, biashara hufanya kazi kama mawakala wa kodi kwa serikali.

* Mmiliki wa duka anapouza bidhaa, hukusanya VAT kutoka kwa mnunuzi; Kisha wanalazimika kisheria kuwasilisha (kulipa) iliyokusanya VAT kwa mamlaka ya kodi ya taifa (TRA)

* Kuweka pesa hizo kwa faida binafsi au ya biashara ni kukwepa kodi, ambayo ni kosa kubwa la jinai. Kwa hivyo, mmiliki wa duka/biashara hafaidiki na fedha kutokana na kodi hiyo.

* VAT ni kodi ya matumizi. Imeundwa ili ichukuliwe na mtumiaji wa mwisho (mnunuzi). Kila wakati mtu anaponunua bidhaa au huduma inayojumuisha VAT, analipa asilimia 18% ya ziada ambayo
huenda moja kwa moja kwenye mapato ya serikali.

* Kuendesha biashara iliyosajiliwa na VAT kunahitaji:
Kuweka mfumo wa rekodi za kiuhasibu.

Kutoa risiti rasmi za kodi za kielektroniki (kama vile risiti za EFD).

Kuwasilisha VAT return ya kila mwezi.
N.B Kuna ukaguzi mkali na adhabu ikiwa hesabu haiendani.

* Output Tax: The VAT the shop charges you (buyer)

* Input Tax: The VAT the shop paid when buying stock from wholesalers.

When filing returns, the shop owner deducts the Input Tax from the Output Tax and pays the net difference to the government.
 
Hii Elimu imekaa poa sana, kumbe Kodi sio hela zetu watu waache kulalamika.

Mkuu asante kwa Elimu hii.
Nisaidie pia kujua na sisi tunaolipa PAYE
 
Kama mtu anaongeza magari ya misafara , bado hawa madogo wa Serengeti wamepew mil 500.. na bado wataongezewa..

Nchi hela ipo..

Nawaza inawezakuw hizi bei ni mambo ya SIASA.. ikifika 5k atokee Jamaaa mmoja aseme nakemea hizi bei nashusha mpk 2800. usikie maneno ya Machawa... na kujipa maujiko ya kisiasa maana itamgusa kila raia.
 
Mafuta yakipanda yanapandisha Budhaa zingine
 
Ukienda kununua mafuta hauoneshi kadi ya CCM wala hausemi, Samia mitano tena. Badala yake unatakiwa ulipe kulingana na EWURA walivosema au zaidi.

Angalia mwenendo wa bei Dar:
  • Petroli: Feb TZS 2,788 → Mei TZS 4,115
  • Dizeli: Feb TZS 2,701 → Mei TZS 4,248
Ndani ya miezi mitatu petroli imepanda ~48%, dizeli ~57%.

Vita vya Mashariki ya Kati na kufungwa kwa Hormuz vimechangia, lakini tozo na kodi za serikali ndizo zinabeba mzigo mkubwa wa bei yetu. kuna tozo na kodi zaidi ya 19 zenye thamani ya zaidi ya TZS 1,113 kwa kila lita — Fuel Levy, Excise Duty, Petroleum Development Levy, Railway Development Levy, VAT, Import Declaration Fee, n.k, karibu asilimia 40 ya bei ya pampu ni tozo za serikali. Linganisha: Uganda ~26%, Ethiopia hawatozi kabisa. Ndiyo maana mwananchi anabeba mzigo wa pande mbili, bei ya dunia pamoja na tozo za nyumbani.

Mafuta yamepanda haraka kuliko nauli, hii ndio hatari zaidi na tumeshaona Wasafirashaji wakigoma na kupanga migomo na hakuna kitu rahisi kama kugoma kwenye usafirishaji.

Mgomo wa nchi nzima hauhitaji tangazo. Wamiliki wanaweza kulemaza usafiri kwa njia ngumu kuzishika kisheria:
  1. Kupunguza safari (badala ya 8, wanafanya 4)
  2. Kupunguza saa za kazi (kutoa magari asubuhi tu, au kuchelewa kuingiza magari)
  3. Kutotoa magari kwa mzunguko — nusu ya magari yanapumzika kila siku, kila baada ya siku moja
90%+ ya wakazi wa miji wanategemea usafiri wa umma, hata punguzo la nusu kwa wiki linaweza kusimamisha jiji.

Hatari kubwa zaidi — kusambaa sekta nyingine. Hapa ndipo jambo linakuwa la taifa zima. Mgomo wa usafiri ni "kibiriti" tu; mfumuko wa bei ndio "petroli."
  • Wafanyakazi wa umma (walimu, wauguzi, polisi wa chini): mishahara ni ileile, lakini nauli + chakula vimepanda. Mtumishi wa mshahara mdogo anaposhindwa kufika kazini na mshahara hauwezi kumudu maisha → madai ya nyongeza ya mshahara → migomo ya kisekta.
  • Madereva wa malori/mizigo (cargo): wakijiunga, bandari na usambazaji wa bidhaa unaganda → uhaba → bei zaidi → hasira zaidi. Hii inageuza tatizo la "mijini" kuwa la kitaifa.
  • Wakulima: dizeli ya matrekta, umwagiliaji na kusafirisha mazao sokoni inapanda → gharama za uzalishaji wa chakula zinaongezeka → mfumuko unazidi.
  • Machinga na biashara ndogo: abiria wakipungua, wateja wanapungua; pembejeo zinapanda. Hawa ni wengi na wepesi kuingia mitaani.
  • Boda boda na bajaji: tayari ni sekta ya usafiri — wakijiunga na daladala, hakuna njia mbadala iliyobaki.

Tofauti na migomo ya Madaktari Serikali imewahi kuingiza Madaktari kutoka Jeshini, ila safari hii hakuna idadi ya magari ya jeshi inaweza kupunguza aina ya mgomo huu, zaidi ni kwamba hayo magari hayatumii maji yanatumia mafuta ambayo yamepanda, hata Serikali ikisema ipunguze gharama ya mafuta kwa magari ya Jeshi bado watachochea mgomo wa Wauzaji wa mafuta, kiufupi hili swala la mafuta ni sehemu nzuri ya kuhakikisha utawala wa Samia hautawali.

Tutarajie migomo na mdororo mkubwa wa Uchumi
Nchi hii siku wananchi wakigundua kuwa kugoma ni rahisi kama kukataa kwenda shule, basi tutatoka haraka sana.
 
Back
Top Bottom