KERO Kupanda kwa Nauli Njia ya MBEZI-MSUMI, MBEZI-MPIJI MAGOE, MBEZI-MSAKUZI

KERO Kupanda kwa Nauli Njia ya MBEZI-MSUMI, MBEZI-MPIJI MAGOE, MBEZI-MSAKUZI

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kabla ya kupanda kwa mafuta nauli za daladala ilikuwa shilingi mia saba 700/= kwa abiria lakini kila ikifika jioni kuanzia saa 1 na kuendelea hupanda mpaka shilingi elfu moja 1000/=, kila abiria atakaye uliza majibu watakayopewa ni kuwa usiku usafiri wa shida gari chache pia barabara za maeneo hayo hazipitiki vizuri hasa wakati wa usiku.

Screenshot_20260509-193726_Google.jpg
Utaratibu huo uliendelea mpaka pale bei ya mafuta ilipopanda Tanzani nzima na kufanya madereva na makondakta wa magari hayo kupandisha bei ya nauli hata nyakati za mchana kuwa elfu moja 1000/=, kabla ya LATRA kutangaza bei mpya ya nauli za daladala.

Pia soma ~ LATRA: Tumeanza kufunga ving'amuzi vya VTS kufuatilia Daladala zinazokatisha ruti na kuzidisha nauli

Kulingana na bei mpya za nauli kutoka LATRA umbali usiozidi kilomita 10 ni shilingi 700/= sawa na umbali kutoka mbezi stendi ya daladala mpaka msumi mwisho sawa na mpiji magoe na msakuzi lakini bado nauli zinazotozwa na daladala zinazoelekea maeneo hayo ni shilingi elfu moja 1000/= hata akitokea abiria analipa shilingi mia nane 800/= kwa makadirio ya kuzidi kilometa 10 za usafiri kwa mujibu wa LATRA ugomvi wa abiria na kondakta unakuwa mkubwa na makondakta baadhi wamesikika wakisema njia hizo hazina nauli ya mia nane 800/=.

20260516_162325.jpg

Pia, kuna baadhi ya wamiliki wa daladala za maeneo hayo hubadilisha usajili wa daladala hizo kwenda ruti nyengine kisha baada ya mda fulani huzirudisha na kutoza abiria nauli ya elfu moja 1000/= na kusema kuwa wanatoa msaada kwa kuwasafirisha abiria hao kwani daladala hizo hazina usajili wa ruti za maeneo hayo.

20260516_162320.jpg

Tunaomba mamlaka zitusaidie kuongea na wamiliki wa magari nakuhakikisha nauli za daladala za kwenda Msumi, Msakuzi na Mpiji magoe haizipandi kiholela kutokana na hali ya uchumi wa sasa, pia wahakikishe daladala zote zinazofanya safari zake kwenda maeneo hayo zimesajiliwa ili kuepusha mchezo wa kuhamisha usajili wa daladala lakink bado zinafanya kazi kwenye maeneo hayo maana kila senti inayotumika ina thamani kubwa ila watu wachache wanatumia mwanya kuwanyonya wengine.

Soma pia:
 
Mitano tena si ndio.... vijana wa huko daslam si ndio mlikuwa mnafanya press kila siku mkisema mtatiki , ? Na mpo na mama, mara anaupiga mwingi? Mara boda boda na bajaji mkasema hamdanganyiki ?

Kuleni chuma hicho
 
Kweli kabisa ..Taifa limejaa malofa kila kona....Mzee Mkapa alitamka waziwazi...
Na mwezi ujao mafuta buku tano ....
 
Jamaa wakishashiba vipande vya viazi mbatata vilivyochemshwa au kukaangwa na akili huwatoroka kabisa.Ni wa kutandikwa viboko vya shingoni hadi waimbe hallelujah!
 
Kweli kabisa ..Taifa limejaa malofa kila kona....Mzee Mkapa alitamka waziwazi...
Na mwezi ujao mafuta buku tano ....

Mwezi ujao mafuta yatakuwa hayapo sokoni, hiyo bei ya elfu 5 ndio inatumika kwa sasa. Pengne vita vikianza tena bei itafika elfu !0
 
Kweli kabisa ..Taifa limejaa malofa kila kona....Mzee Mkapa alitamka waziwazi...
Na mwezi ujao mafuta buku tano ....
Sasa hivi kila kona ni kilio ....mkapa hakosea kusema taifa limejaa malofa
 
Mitano tena si ndio.... vijana wa huko daslam si ndio mlikuwa mnafanya press kila siku mkisema mtatiki , ? Na mpo na mama, mara anaupiga mwingi? Mara boda boda na bajaji mkasema hamdanganyiki ?

Kuleni chuma hicho
Kwa hiyo wasingetiki ndio wangezuia bei za mafuta zisipande duniani?
 
Hiyo ya kilometa 10 kwa mia 7 si ni barabara ya lami?
 
Hiyo ya kilometa 10 kwa mia 7 si ni barabara ya lami?
Ukisoma vizuri hapo utaona hata kabla ya mafuta jamaa walikuwa wanatozwa nauli ya barabara ya lami ambayo ndio ilikuwa official na mpaka saiv inabid iwe ivyo kama mwanzo ila sijui kama kuna taratibu zimebadilika
 
Hili taifa ni daraja la wazenji kujitajilisha bila kumtetea mtanganyika kwa lolote lile. Kila sehemu ni kilio n watawala hawajali kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom