Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Punguza maneno mengi, kuna watu kibao wanatafuta watu wakubadirishana nao vituo wapo vijijini, we nenda huko vijijini kwenye fursa na wao waje mjini watakate.
 
Kwahiyo huku ni kilimoo tuuu
Kwa usiyependa kilimo HAKUNA KITU!?

#YNWA
Atapata fursa zingine mfano kujenga godowns za mazao,mashine za kuchakata mazao, usafir,duka la jumla yaani unanunua mjini vitu kwa jumla unaweka home kwako unaanza wasambazia wenye viduka vidogo vijijini mfano mbolea,madawa,mahitaji ya dukani,vifaa vya sola,nk.
Ukitaka starehe unaendaa mjini.
 
Niambie kijiji gani wanapewa nyumba bure hizi slogan huwa mnalishwa na nani? Mara utapewa mashamba bure, mara utapewa chakula na mazao bure nenda sasa kijijini uone hata mchicha wa bure hakuna.
 
Niambie kijiji gani wanapewa nyumba bure hizi slogan huwa mnalishwa na nani? Mara utapewa mashamba bure, mara utapewa chakula na mazao bure nenda sasa kijijini uone hata mchicha wa bure hakuna.
Vingi tu, Mimi mwenyewe nampango wa kuanza kuwajengea watumishi nyumba za kukaa bure nazitoa kwa Serikali ya kijiji huko penye fursa
 
Kufanikiwa inategemea mtu na mtu sio wote wanatoboa, alafu mafanikio unayapima kwa mizani gani? Huko vijijini hakuna ushindani wa maisha mtu akiwa na kijumba, kaduka ka kuuza mchele na kabodada anaitwa tajiri mkubwa.
 
Kama poa kwanini usiishi na familia yako, hapa kuna uwalakini...
Watoto watadumaa sana kiakili, hawatajua dunia ya sasa ilivyo. Ustawi wa familia kiujumla utakuwa mdogo sana. Ila pesa kijijin ipo kuliko mjini, unanunua kiswaswadu elfu 20 mjin unaenda kuuza 35, wakat wa masika kijijin huwa kunanukaa njaa, unanunua ng'ombe hadi laki 2, wakat wa Kiangaz unapiga lak 8 hadi milion na hapo ni miez 3-4 tu.

Sijui kwenye elimu, upande wa afya utaenda sana semina kwa sababu mpo wachache, mtalipana allowances zote na pesa nzuri kwasababu ya uchache wenu,.

Wanakijiji rahis kukusupport km unaenda nao sawa, wanaweza kukulimia shamba, kukujengea mazizi ya mifugo n.k.
 
Wewe haupo vijijini na wala hujawahi kuishi kijijini, nenda kijijini kaishi haya maneno ya taarabu hutosema tena.
 
Upo sahihi kaka, kwa mtu aliyetoka Mwanza mjini au Dar, umpeleke vijijini huyu baada ya miaka mitano mtamzika, vijijini unapata mshahara na pesa hujui unaitimia vipi hakuna sehemu ya kuspend, upo tu unapigwa vumbi na upepo mkali, hakuna pisi kali, hakuna kupiga pamba na mwendo wa kufukuzana na mbuzi na wanyama.....
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
 
Motivational speaker kwenye ubora wenu, nenda field kafanye haya.
 
Zaidi ya kutakata mjini kuna maisha gani fainal ukistaafu ndo utajua
Unawazia kustahafu, yaani niishi kwa kujitesa na tabu za vijijini eti nikisubiria uzeeni ndio niishi vizuri, vunja mifupa ingali meno ipo, kwa mijini huwa hawana akili ya kufatuta, nyie wa mijini huwa mnadharau sana... Unasema hayo na hapo upo mjini.
 
Nashukuru sana kwa kutambua kuwa ukiwa kijijini lazima udumae kiakili na mwili na ukishadumaa kiakili hata haya mawazo ya hizo fursa hutokuwa nayo, asante sana kiongozi.
 
Wanafiki waliopata zali ya kuajiriwa mjini watajifanya hawaoni.
 
Nashukuru sana kwa kutambua kuwa ukiwa kijijini lazima udumae kiakili na mwili na ukishadumaa kiakili hata haya mawazo ya hizo fursa hutokuwa nayo, asante sana kiongozi.
Ndo maana nikasema familia iwe mjin, kila baada ya miez 2 hivi nenda mjin bila hivyo kuishi na familia kijijin lazima uwe bogus kias fulan
 
Kuna halmashauri inaitwa Rombo.
  • Huwezi kulima
  • Huwezi kufuga
  • Huwezi kufanya biashara
  • Huwerzi kujenga, utapanga mpaka siku unastaafu

kudadadeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…