Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kijijini Kila kitu bure kuanzia kuni,maji, chakula unaweza pewa na wanakijiji inategemea na UKARIBU nao, nyumba bure za Serikali au Kodi chini chumba za kisasa hakizidi elf 20,hakuna nauli,mjini mfanyakazi wa chini bila elf 10 ajatoka na kurudi jioni kwake kwa mshahara wa laki 7 wa mjini bila rushwa amalizi mwez wa kijijini mshahara unakutana.
Ulimwengu huu wa internet unakuaje masikini Sasa huku umezungukwa na fursa.
Utakuwa masikini Kama utaki kulink na external world
Punguza maneno mengi, kuna watu kibao wanatafuta watu wakubadirishana nao vituo wapo vijijini, we nenda huko vijijini kwenye fursa na wao waje mjini watakate.
 
Kwahiyo huku ni kilimoo tuuu
Kwa usiyependa kilimo HAKUNA KITU!?

#YNWA
Atapata fursa zingine mfano kujenga godowns za mazao,mashine za kuchakata mazao, usafir,duka la jumla yaani unanunua mjini vitu kwa jumla unaweka home kwako unaanza wasambazia wenye viduka vidogo vijijini mfano mbolea,madawa,mahitaji ya dukani,vifaa vya sola,nk.
Ukitaka starehe unaendaa mjini.
 
Kijijini Kila kitu bure kuanzia kuni,maji, chakula unaweza pewa na wanakijiji inategemea na UKARIBU nao, nyumba bure za Serikali au Kodi chini chumba za kisasa hakizidi elf 20,hakuna nauli,mjini mfanyakazi wa chini bila elf 10 ajatoka na kurudi jioni kwake kwa mshahara wa laki 7 wa mjini bila rushwa amalizi mwez wa kijijini mshahara unakutana.
Ulimwengu huu wa internet unakuaje masikini Sasa huku umezungukwa na fursa.
Utakuwa masikini Kama utaki kulink na external world
Niambie kijiji gani wanapewa nyumba bure hizi slogan huwa mnalishwa na nani? Mara utapewa mashamba bure, mara utapewa chakula na mazao bure nenda sasa kijijini uone hata mchicha wa bure hakuna.
 
Vingi tu, Mimi mwenyewe nampango wa kuanza kuwajengea watumishi nyumba za kukaa bure nazitoa kwa Serikali ya kijiji huko penye fursa
 
Hata mimi nilikua na mawazo ya kuhama kama wewe wakati nipo kijijini.

Baadae nilingundua mawazo ya kuhama yananizuia kujiendeleza na kuwekeza, na pia yanazuia kuziona fursa na kuzitumia.

Mm nilianzia wilayani nikaomba niende kijijini. Huko kwa kweli nilifanikiwa kibiashara kiasi, familia ilinipatia mtaji, na nilibahatika kufanya biashara kutoka Malawi miaka hiyo hasa mbuzi na karanga. Na locally nilikua nanua mpunga kipindi cha mavuno na kuuweka hadi mwisho wa mwaka.

Nilipoondoka, alienipokea alikuja kwa program ya Mkapa foundation, hakuwa na uhakika wa ajira ya kudumu, alikua Msukuma, alianzisha mradi wa ng'ombe wa maziwa, ufugaji kuku, na akatafuta location akaweka pool table. Aliwahi kuniambia hata akikosa ajira, hatohama hapo kijijini.

Kwa sasa nimesikia amewekeza ziwani (ziwa Nyasa) na ana bodaboda kampa kijana, still anapambana, na kwa ujumla anaendelea vyema.

Sometimes it is all about mindsets and priorities.
Kufanikiwa inategemea mtu na mtu sio wote wanatoboa, alafu mafanikio unayapima kwa mizani gani? Huko vijijini hakuna ushindani wa maisha mtu akiwa na kijumba, kaduka ka kuuza mchele na kabodada anaitwa tajiri mkubwa.
 
Kama poa kwanini usiishi na familia yako, hapa kuna uwalakini...
Watoto watadumaa sana kiakili, hawatajua dunia ya sasa ilivyo. Ustawi wa familia kiujumla utakuwa mdogo sana. Ila pesa kijijin ipo kuliko mjini, unanunua kiswaswadu elfu 20 mjin unaenda kuuza 35, wakat wa masika kijijin huwa kunanukaa njaa, unanunua ng'ombe hadi laki 2, wakat wa Kiangaz unapiga lak 8 hadi milion na hapo ni miez 3-4 tu.

Sijui kwenye elimu, upande wa afya utaenda sana semina kwa sababu mpo wachache, mtalipana allowances zote na pesa nzuri kwasababu ya uchache wenu,.

Wanakijiji rahis kukusupport km unaenda nao sawa, wanaweza kukulimia shamba, kukujengea mazizi ya mifugo n.k.
 
Hata mimi nilikua na mawazo ya kuhama kama wewe wakati nipo kijijini.

Baadae nilingundua mawazo ya kuhama yananizuia kujiendeleza na kuwekeza, na pia yanazuia kuziona fursa na kuzitumia.

Mm nilianzia wilayani nikaomba niende kijijini. Huko kwa kweli nilifanikiwa kibiashara kiasi, familia ilinipatia mtaji, na nilibahatika kufanya biashara kutoka Malawi miaka hiyo hasa mbuzi na karanga. Na locally nilikua nanua mpunga kipindi cha mavuno na kuuweka hadi mwisho wa mwaka.

Nilipoondoka, alienipokea alikuja kwa program ya Mkapa foundation, hakuwa na uhakika wa ajira ya kudumu, alikua Msukuma, alianzisha mradi wa ng'ombe wa maziwa, ufugaji kuku, na akatafuta location akaweka pool table. Aliwahi kuniambia hata akikosa ajira, hatohama hapo kijijini.

Kwa sasa nimesikia amewekeza ziwani (ziwa Nyasa) na ana bodaboda kampa kijana, still anapambana, na kwa ujumla anaendelea vyema.

Sometimes it is all about mindsets and priorities.
Wewe haupo vijijini na wala hujawahi kuishi kijijini, nenda kijijini kaishi haya maneno ya taarabu hutosema tena.
 
Kwa wapenda bata vijijini hakuwafai.
Ishu ya internet ni vijiji vichache havina labda vile vidogo ambavyo Serikali haijapeleka uhitaji wa huduma za kijamii sababu hakuna watu, kampuni za simu zinashindana kupeleka minara hata pasipo na umeme wanatumia sola.
Popote penye watu Pana pesa ni wewe kichwan mwako tu hata mjini watumishi wengi wanapigika maisha ni Ile tu kusafisha macho mjini at the end wengi uishia kuwa masikini mbwa baada ya kusataafu
Upo sahihi kaka, kwa mtu aliyetoka Mwanza mjini au Dar, umpeleke vijijini huyu baada ya miaka mitano mtamzika, vijijini unapata mshahara na pesa hujui unaitimia vipi hakuna sehemu ya kuspend, upo tu unapigwa vumbi na upepo mkali, hakuna pisi kali, hakuna kupiga pamba na mwendo wa kufukuzana na mbuzi na wanyama.....
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
 
Atapata fursa zingine mfano kujenga godowns za mazao,mashine za kuchakata mazao, usafir,duka la jumla yaani unanunua mjini vitu kwa jumla unaweka home kwako unaanza wasambazia wenye viduka vidogo vijijini mfano mbolea,madawa,mahitaji ya dukani,vifaa vya sola,nk.
Ukitaka starehe unaendaa mjini.
Motivational speaker kwenye ubora wenu, nenda field kafanye haya.
 
Zaidi ya kutakata mjini kuna maisha gani fainal ukistaafu ndo utajua
Unawazia kustahafu, yaani niishi kwa kujitesa na tabu za vijijini eti nikisubiria uzeeni ndio niishi vizuri, vunja mifupa ingali meno ipo, kwa mijini huwa hawana akili ya kufatuta, nyie wa mijini huwa mnadharau sana... Unasema hayo na hapo upo mjini.
 
Watoto watadumaa sana kiakili, hawatajua dunia ya sasa ilivyo. Ustawi wa familia kiujumla utakuwa mdogo sana. Ila pesa kijijin ipo kuliko mjini, unanunua kiswaswadu elfu 20 mjin unaenda kuuza 35, wakat wa masika kijijin huwa kunanukaa njaa, unanunua ng'ombe hadi laki 2, wakat wa Kiangaz unapiga lak 8 hadi milion na hapo ni miez 3-4 tu.

Sijui kwenye elimu, upande wa afya utaenda sana semina kwa sababu mpo wachache, mtalipana allowances zote na pesa nzuri kwasababu ya uchache wenu,.

Wanakijiji rahis kukusupport km unaenda nao sawa, wanaweza kukulimia shamba, kukujengea mazizi ya mifugo n.k.
Nashukuru sana kwa kutambua kuwa ukiwa kijijini lazima udumae kiakili na mwili na ukishadumaa kiakili hata haya mawazo ya hizo fursa hutokuwa nayo, asante sana kiongozi.
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.
Wanafiki waliopata zali ya kuajiriwa mjini watajifanya hawaoni.
 
Nashukuru sana kwa kutambua kuwa ukiwa kijijini lazima udumae kiakili na mwili na ukishadumaa kiakili hata haya mawazo ya hizo fursa hutokuwa nayo, asante sana kiongozi.
Ndo maana nikasema familia iwe mjin, kila baada ya miez 2 hivi nenda mjin bila hivyo kuishi na familia kijijin lazima uwe bogus kias fulan
 
Upo sahihi kabisaaa

Wale wa Halmashauri za Wilaya zile ngumuuu kama

1. Ukerewe
2. Momba
3. Mpimbwe
4. Mlele
5. Tanganyika

Watakuelewa vizuri sanaaa. Ukiwa halmashauri hizi Kutoboa ki exporure, academic na financially ni taabu sanaaaaaa.

Raia wa humo huwaza kulima na kufuga tu.

#YNWA
Kuna halmashauri inaitwa Rombo.
  • Huwezi kulima
  • Huwezi kufuga
  • Huwezi kufanya biashara
  • Huwerzi kujenga, utapanga mpaka siku unastaafu

kudadadeki
 
Back
Top Bottom