Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Hata uwe na solar kama mazingira yanayokuzunguka ni watupori lazima na wewe uwe pori
Pengine hujafika hivyo vijiji ninavyomaanisha unadhani nikisema kijiji namaanisha kijiji cha Makumbusho Dar[emoji1787]
Hawatakuelewa hawa watu, na asilimia kubwa haya watu wa jf wapo mjini.
 
Kwani watumishi wa mijini hawauzi barafu? Haya unayoyasema hapa kwani mjini hayafanyiki? Napenda ujue kuwa ukitoka mjini unajuwa na akili sharp sana lakini ukienda kuishi kijijini kila siku akili yako inapungua na haya mawazo ya kuangalia fursa hutokuwa nayo tena, pia kuna vijijini ni kama jangwa hakuna kulima hakuna kufuga hakuna fursa yoyote.
 
Uwezo wa kufikiri hutegemea na mazingira yanayokuzunguka eg aliekulia New York, dar es salaam na Pangani hawawezi fanana hata kama wote hawajasoma.
Uwezo wa kufikiria na kuziona fursa hutegemea level ya competition ya jamii ndio maana mtu wa kijijini automatic hujikuta ni fursa Kwa yule wa mjini eg unatoka na mazao Yako kuja kuuza mjini utakutana na mtu anaejiita dalali anakupiga
Kama Japan nchi ya Dunia ya kwanza na watu wanakimbia vijijini huku vijiji vyao vikiwa na Kila kitu Barbara za lami,umeme,maji,mawasiliano mpaka ukitaka kuhama mjini kurudi kijijini serikali inakulipa lakini watu hawataki hapo unaweza ona by nature kijijini huwezi fanikiwa

Wewe ona hata hizi jamii za watu weupe zinarundikana kutokana na maendeleo ya sehemu ukiwa dar es salaam ukiambiwa katafute muhindi, machina,mwarabu ni rahisi Sasa nenda Nanyamba huwakuti kwakuwa fursa zinakuwa zimepungua, vijijini hata mzunguko wa pesa ni za msimu.

Watu wa vijijini Bado wanaamini kwenye socialization hivyo wengi huamini huduma ni Bure hivyo huwezi kutumia professional Yako kujipatia kipato Cha ziada mfano nesi wa mjini ukienda kumfuata nyumbani kwake muda sio wa kazi akuchome sindano utamlipa 1000 kijijini mtu atataka Bure,
All in all kijijini utaonekana umefanikiwa ila hujafanikiwa sema kwakuwa unashindana na masikini ni SAWA na wale tunaowaona wamefanikiwa Tanzania ukienda linganisha na wamarekani utawaona wakawaida
 
Unakuta unayoyasema haya upo mjini[emoji16]

Wakurugenzi wenyewe wa vijijini familia zao wameweka mjini

Wabunge wa hivo vijiji wote wanaishi mjini[emoji3]
 
Wamezoea kwenda bar kujirusha kila weekend
 
Kwani open university/other distance learning wana offer kozi zote?

Mfano medicine wanatoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Mapopoma yapo humu kuwalisha wenzao ujinga wakati wao wametulia mijini wakila kiepe yai, na maini roast, bila kusahau kusahau kula mbususu zenye quality...wajinga sana hawa kamanda.
 
Ujue ukiropoka uwe na data

Hujui ni mwaka huu ndiyo serikali imeingia mkataba wa ujenzi wa minara 700 sehemu ambazo hakuna mawasiliano.

Vijiji asilimia 99 havina 4G wala 3G bado wako Edge
Man nimetembea nchi hii sehem pasipo na network labda kwa sababu ya ishu ya population kampuni za simu zimeona hailipi.Hakuna kijiji Cha population zaidi ya watu 100 kikakosa mawasiliano inaweza isiwe ni 24hrs sababu usiku hakuna Sola na pia wapo bondeni lakini mchana wanapata network.
Serikali gani inayojenga minara
 
Wewe haupo vijijini na wala hujawahi kuishi kijijini, nenda kijijini kaishi haya maneno ya taarabu hutosema tena.
Kwamba unayajua zaidi maisha yangu kuliko mimi?

Acha ujuaji.

Kwa sasa sipo kijijini, ila niliishi miaka mitatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…