Kupanua tax base-makanisa, ministries, misikiti vihusike kulipa kodi

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,090
♻️ Kwa kuzingatia wigo mdogo wa walipa kodi ktk nchi yetu dhidi ya idadi kubwa ya wananchi..

♻️ Kufuatia deni la taifa kuongezeka kila leo..
Kufuatia mtikisiko wa thamani wa fedha yetu..

♻️ Kufuatia ukwasi mkubwa wa taasisi za kidini kupitia mapato ya Sadaka,dhaka,mafungu ya kumi..Malimbuko..

♻️ Kufuatia wepesi wa Watanzania kutoa Sadaka kuoitia imani zao mbalimbali..

♻️ Kufuatia utajiri na ukwasi mkubwa wa waendesha huduma za kiroho..Na hili linachagizwa na biashara ya kuuza maji ya upako,Chumvi,Vitambaa,Mafuta,Rangi,etc.

♻️ Ni wakati sasa sheria ya kodi iguse na kutoza kodi kwenye taasisi hizi kuongeza wigo wa mapato kwa nchi.
 
Hata hizo taasisi zikilipa bado zitaishia mikononi mwa wachache kama huna nidhamu kwenye kidogo hata kikubwa kitakushinda tu kwanini 4% ya bajeti inatengwa kwenye anasa (sherehe, vitafunwa, samani za wakubwa, safari nk) huoni ni uzwazwa zaidi ya 600B zinatengwa kwenda kununua magari ya kifahari ya mwaka 2024 kama haitoshi wake za wastaafu wanalipwa nao kiinua mgongo ajabu kabisa.
 
Nadhani haja ya kuimarisha taasisi za udhibiti na ukaguzi ni muhimu kikatiba ili nidhamu na tija viwepo..
 
♻️Kwa kuzingatia wigo mdogo wa walipa kodi ktk nchi yetu dhidi ya idadi kubwa ya wananchi..

♻️Kufuatia deni la taifa kuongezeka kila leo..
Kufuatia mtikisiko wa thamani wa fedha yetu..

♻️Kufuatia ukwasi mkubwa wa taasisi za kidini kupitia mapato ya Sadaka,dhaka,mafungu ya kumi..Malimbuko..

♻️Kufuatia wepesi wa Watanzania kutoa Sadaka kuoitia imani zao mbalimbali..

♻️Kufuatia utajiri na ukwasi mkubwa wa waendesha huduma za kiroho..Na hili linachagizwa na biashara ya kuuza maji ya upako,Chumvi,Vitambaa,Mafuta,Rangi,etc.

♻️Ni wakati sasa sheria ya kodi iguse na kutoza kodi kwenye taasisi hizi kuongeza wigo wa mapato kwa nchi.

Mapatonyasiyokatiwa kodi na Sadaka tuu.ila mengine yote yanatakiwa kukatwa kodi.Mfano hayo ya kuuza vifaa vya kiroho inatakiwa iwepo kodi.yaani itathiminiwe kiasi cha mauzo halafu ikatwe kodi kwenye business income
 
Tax base nakubali,asilimia 45% tatizo nchi imewekeza mno katika anasa,safari za viongozi wajuu wa nchi,warsha, na rushwa hivi vitu vinakula Sana fedha za nchi,Kama nchi hatuna usimamizi madhubuti wa mapato ya nchi,na hatujaimarisha uzalishaji wa ndani Bali tunaendekeza mikopo ndiyo itatuletea maendeleo
 
Hata hizo taasisi zikilipa bado zitaishia mikononi mwa wachache kama huna nidhamu kwenye kidogo hata kikubwa kitakushinda tu kwanini 4% ya bajeti inatengwa kwenye anasa (sherehe, vitafunwa, samani za wakubwa, safari nk) huoni ni uzwazwa zaidi ya 600B zinatengwa kwenda kununua magari ya kifahari ya mwaka 2024 kama haitoshi wake za wastaafu wanalipwa nao kiinua mgongo ajabu kabisa.
Mwambie ukweli huyo chawa hajielewi kabisa!
 
Acheni kuwatengenezea njia zaidi za kupiga hela hawa mafisadi. Rasilimali tulizonazo, zikitumiwa vizuri na kubana matumizi Serikalini, hali itakuwa tofauti.

Nchi inaenda kukopa na inajaza wabunge wa viti maalum, hawana tija ni kuongeza mzigo wa bure. Magari ya viongozi wananunua ya bei kubwa sana bado jinsi ya kuyaendesha.

Safari za nje ni nyingi kwa viongozi. Wajibane na waache ufisadi halafu waone nini kitatokea. Hawataweza sababu kwao kuwa kiongozi, ni kuishi kama Mfalme au Malkia.
 
♻️Kwa kuzingatia wigo mdogo wa walipa kodi ktk nchi yetu dhidi ya idadi kubwa ya wananchi..

♻️Kufuatia deni la taifa kuongezeka kila leo..
Kufuatia mtikisiko wa thamani wa fedha yetu..

♻️Kufuatia ukwasi mkubwa wa taasisi za kidini kupitia mapato ya Sadaka,dhaka,mafungu ya kumi..Malimbuko..

♻️Kufuatia wepesi wa Watanzania kutoa Sadaka kuoitia imani zao mbalimbali..

♻️Kufuatia utajiri na ukwasi mkubwa wa waendesha huduma za kiroho..Na hili linachagizwa na biashara ya kuuza maji ya upako,Chumvi,Vitambaa,Mafuta,Rangi,etc.

♻️Ni wakati sasa sheria ya kodi iguse na kutoza kodi kwenye taasisi hizi kuongeza wigo wa mapato kwa nchi.
Kodi ipi vilipe?
 
Ni wazo zuri, naongezea kwa kushauri na kupendekeza yafuatayo ili kukuza hiyo TAX BASE

1. Iwe ni sheria kila nyumba iwe na umeme ili kulipa kodi ya majengo, imagine kuna nyumba ngapi kuanzia Bukoba mpaka Tanga, kuna nyumba ngapi kuanzia Mara mpaka Mtwara vipi kuhusu nyumba kuanzia Katavi mpaka Manyara na je kuna nyumba ngapi kuanzia Arusha hadi Kigoma.

Ni maelfu ya nyumba hata wakilipa 1000 tu kwa mwezi ambayo hata haiumizi ni pesa kiasi gani utakusanya na nipesa ya uhakika kila mwezi maana lazima anunue umeme.

Pili kuwepo na mipango miji yenye tija ili kubaini wafanyabiashara wote, kuwepo na sheria ya maeneo maalumu ya kufanyia biashara ili kubaini idadi yao, siyo kama ilivyo kwa sasa wanafanyabiashara wanaotambulika ni wale tu waliopo cente ya kijiji au wilaya, lakini huko vichochoroni nje na cente kunawatu wanabiashara na hawalipi kodi mfano mtu amegeuza chumba kimoja kimejaa bidhaa na kufanya dirisha moja kuwa sehemu ya kutolea huduma ya dukani lakini halipi kodi je ni mapato kiasi gani yanapotea??

Badala yake unabebesha mzigo kwa watu wachache. Na hii ni Wizara moja tu ya ardhi sijagusa Wizara ya kilimo.
 
Kweli walipe kodi sasa, haya si Makanisa ni makampuni, Yesu aliwapiga na kuwafukuza wafanyabiashara ndani ya kanisa... Leo wamerudi kwa nguvu na ari mpya.... Elisha alikataa zawadi ya Naamani, hebu Naamani aje leo atashangaa..... yaani Wanadai michango Hadi kama vichaa....
 
Makanisa ni makampuni ya biashara ya consultants za kiroho na wanapiga fedha na ukwasi mwingi Sana usiotozwa Kodi,serikali geukieni huko pia,lakini shaka yangu kubwa,ni kuwa serikali hii imetopea mno kwenye matumizi ya anasa na rushwa.hata Kama tungelipa Kodi Hadi ya nguo za ndani ,bado Kodi haitatosha kwani viongozi wa Tanzania mentality zao ni kupata nafasi na kuanzisha kutengeneza mianya ya ufujaji wa fedha
 
Tax base nakubali,asilimia 45% tatizo nchi imewekeza mno katika anasa,safari za viongozi wajuu wa nchi,warsha, na rushwa hivi vitu vinakula Sana fedha za nchi,Kama nchi hatuna usimamizi madhubuti wa mapato ya nchi,na hatujaimarisha uzalishaji wa ndani Bali tunaendekeza mikopo ndiyo itatuletea maendeleo

Kupanga ni kuchagua

Nchi tajiri wapo sensitive sana ktk matumizi yao..

Nasi ni wakati tukafanya maamuzi ya kujibana kwa dhati..Tudhibiti matumizi yasio ya lazima sana..Tupunguze misafara,warsha,Makongamano,Maadhimishoyanayoepukika au yasio na tija kwenye ukuaji wa uchumi..
 
Nadhani haja ya kuimarisha taasisi za udhibiti na ukaguzi ni muhimu kikatiba ili nidhamu na tija viwepo..
CAG kila mwaka anakuja na report yenye ubadhirifu lakini hakuna kinachofanyika ila mwizi wa kuku na mchoma picha kesi ni harakq na mvua inamnyeshea
 
Acheni kuwatengenezea njia zaidi za kupiga hela hawa mafisadi. Rasilimali tulizonazo, zikitumiwa vizuri na kubana matumizi Serikalini, hali itakuwa tofauti.

Nchi inaenda kukopa na inajaza wabunge wa viti maalum, hawana tija ni kuongeza mzigo wa bure. Magari ya viongozi wananunua ya bei kubwa sana bado jinsi ya kuyaendesha.

Safari za nje ni nyingi kwa viongozi. Wajibane na waache ufisadi halafu waone nini kitatokea. Hawataweza sababu kwao kuwa kiongozi, ni kuishi kama Mfalme au Malkia.
Mambo ya ajabu lukuki eti viti maalumu upuuzi mtupu wanakula mishahara na posho bure tu kwanza mishara na posho za wabunge ingepunguzwa nayo. Leo/jana PM yupo/alikuwa Njombe eti anakataa makadilio ya ujenzi wa nyumba za walimu kwa kiasi cha 100m anasema haipaswi kuzidi 30m wakati wao wanapitisha bajeti ya kununua magari yao zaidi ya 600B gari moja la PM linafika 500m msafara wake unayo ya kutosha​
 
Kupanga ni kuchagua

Nchi tajiri wapo sensitive sana ktk matumizi yao..

Nasi ni wakati tukafanya maamuzi ya kujibana kwa dhati..Tudhibiti matumizi yasio ya lazima sana..Tupunguze misafara,warsha,Makongamano,Maadhimishoyanayoepukika au yasio na tija kwenye ukuaji wa uchumi..
Nani wa kufanya hayo maamuzi ya kujibana namba 1, Tulia au Mwigulu hiyo nidhamu inatoka wapi ikiwa VOTE 20 haiguswi​
 
Ni wazo zuri, naongezea kwa kushauri na kupendekeza yafuatayo ili kukuza hiyo TAX BASE

1. Iwe ni sheria kila nyumba iwe na umeme ili kulipa kodi ya majengo, imagine kuna nyumba ngapi kuanzia Bukoba mpaka Tanga, kuna nyumba ngapi kuanzia Mara mpaka Mtwara vipi kuhusu nyumba kuanzia Katavi mpaka Manyara na je kuna nyumba ngapi kuanzia Arusha hadi Kigoma.

Ni maelfu ya nyumba hata wakilipa 1000 tu kwa mwezi ambayo hata haiumizi ni pesa kiasi gani utakusanya na nipesa ya uhakika kila mwezi maana lazima anunue umeme.

Pili kuwepo na mipango miji yenye tija ili kubaini wafanyabiashara wote, kuwepo na sheria ya maeneo maalumu ya kufanyia biashara ili kubaini idadi yao, siyo kama ilivyo kwa sasa wanafanyabiashara wanaotambulika ni wale tu waliopo cente ya kijiji au wilaya, lakini huko vichochoroni nje na cente kunawatu wanabiashara na hawalipi kodi mfano mtu amegeuza chumba kimoja kimejaa bidhaa na kufanya dirisha moja kuwa sehemu ya kutolea huduma ya dukani lakini halipi kodi je ni mapato kiasi gani yanapotea??

Badala yake unabebesha mzigo kwa watu wachache. Na hii ni Wizara moja tu ya ardhi sijagusa Wizara ya kilimo.
Hata yote hayo yafanyike na pesa ziongezeke watakwiba na kufuja safari za nje zitaongezeka mara dufu na watataka watembelee range rover za kisasa zaidi ama defender zile za kisasa​
 
Shida ya taifa hili,sio kulipa Kodi,bali matumizi sahihi ya Kodi,ndo shida kubwa.
JamiiForums-1176904024.jpg
 
Ili taifa au nchi iwe tajiri haitakiwi kuwaza au kuongeza kodi.
Kodi haiongezi utajiri wa nchi.
Ili uwe tajiri lazima ukusanye kutoka kwa wengine, lazima wengine wakuhitaji ili wakulipe (wahitaji na kununua maliasili, ujuzi/teknolojia, bidhaa,.... kutoka kwako). Huko nyuma nguvu ilitumika (utumwa na ukoloni au njia za kutafuta utajiri kijima kama uvamizi/vita).
Kodi kwa utajiri wa nchi ni kama kuhamisha pesa yako mfuko mmoja wa suruali au shati na kuweka mwingine, haiongezeki.
Mataifa yaliyoendelea yote yanatafuta utajiri nje na siyo kunyonya wananchi wao kwa kodi (kunyonya kwani huhudumia viongozi zaidi na hata huiba kuficha nje ya nchi).
Tukijenga barabara zetu kwa kutumia makampuni ya kichina moja kwa moja tumeongeza utajiri wa China, vivyo hivyo tunaponunua bidhaa kwao.
Hata hivyo, kodi ni muhimu kwa uendeshaji wa shughuli za serikali na utoaji huruma za kimaendeleo kwa wananchi.
Tunatakiwa kuwaza nje ya sanduku la Kodi ili tuendelee zaidi na nchi yetu au taifa liwe tajiri.
 
Back
Top Bottom