Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nina ardhi yangu iko mkoa wa Dar es Salaam haijapimwa bado.
Je, process za wizara ya ardhi kukupimia zikoje?
Umetisha sana mkuu. Mi pia nipo kwenye hatua ya kupata hati mbezi goba ila muda nimekua sina so namtumia jamaa wa kampuni ya upimaji ambae juzi tu kanilamba 150k kwa ajili ya kuweka mawe halafu next step apate plot number maana tayari vilikua vilishapimwa. Ila nahisi mchakato utawahi sababu wilaya ya ubungo kitengo Cha ardhi wamepiga kambi pale kimara stopover wameweka kama clinic ya ardhi kusaidia kuharakisha michakato yote ya mambo ardhi wilaya ya ubungo. Ila nishatenga kama 1.5 pembeni kuhakikisha napata hati maana viwanja vimeungana viwiliOption 1
Tafuta kampuni ya upimaji iliyoidhinishwa ikupimie, na itakuongoza kwenye taratibu zote...
Option 2
Nenda ofisi za wilaya husika kilipo kiwanja chako huwa wanakuwa na maafisa ardhi na wanapima ardhi watakupa utaratibu...
Hata hivyo abc's za upimaji ardhi zipo kama ifuatavyo...
1. Hakikisha unatambulika na mjumbe wa eneo husika, huyu atakusaidia kwenye utambuzi wa mipaka ya eneo lako wakati wa upimaji.
2. Kuwa na mkataba wa mauziano au kielelezo cha namna ulivyoipata hiyo ardhi ulioidhinishwa na mwanasheria, ingawaje hata mkataba uliosimamiwa na serikali za mitaa unafaa.
3. Tafuta wapimaji wataochukua alama za mipaka na kwenda kuingiza kwenye ramani ya mipango miji, ambapo baadaye utapata mchoro uliosajiliwa, plot number n.k.
4. Utafunguliwa file ambalo ndani yake litakuwa na vielelezo vingi iwepo na fomu ambazo utatakiwa ujaze baadhi ya fomu kama fomu ya mwenye kiwanja na majirani (majirani watasaini), na fomu nyingine kama nne hivi (sijakariri majina yake maana zipo za kuonesha ukubwa wa kiwanja na nyingine unajaza matumizi ya kiwanja, eneo kiwanja kilipo, plot number n.k), fomu hizi zote mwisho wa siku italizimika zipitishwe kwa mwenyekiti wa mtaa na watu wa kata.
5. File likikamilika linapelekwa manispaa ardhi kwa ajili ya kuscan ili kumbukumbu zako ziwe kwenye mfumo wa kompyuta, na hapo utapewa control number ya kulipia malipo ya awali ambayo huwa ni 20,000/=. Ukishakamilisha malipo hayo, process za kuandaliwa hati zitaendelea na baadaye utatakiwa kulipia hati kwa control number pia na malipo haya hutegemea ukubwa wa kiwanja, jinsi kiwanja kinavyokuwa kikunwa ndivyo pesa hii nayo inakuwa kubwa. Malipo haya yakishathibitishwa, mwisho utajulishwa kuwa usajili wa kiwanja umetimia na hapo utakuwa na uwezo wa kuchukua hati...
Hitimisho:
1. Gharama kubwa zipo sehemu mbili ambapo ni gharama ya kufanya survey ya kiwanja na kuchukua coordinates na gharama ya hati.
2. Jiandae pia kuwa na hela ya "kiwi" maana mlolongo wa watu wa serikali za kijiji, mtaa au kata huwa gharama zao ndogo ndogo, ukiacha hao pia mtu wa ardhi anayedeal na mafile anaweza akawa anakuzungusha mara file halioni na kadhalika kumbe anataka umpe rupia tu mambo yasogee...
3. Kuhusu muda ni ngumu kutaja maana nadhani umeona kuna dependencies nyingi hapo, lakini mara nyingi ramani ikishasajiliwa na ukapewa go ahead ya kulipa malipo ya awali ya 20,000 basi unaweza ukapambana hati ukaipata same day au hata kesho yake...
Umetisha sana mkuu. Mi pia nipo kwenye hatua ya kupata hati mbezi goba ila muda nimekua sina so namtumia jamaa wa kampuni ya upimaji ambae juzi tu kanilamba 150k kwa ajili ya kuweka mawe halafu next step apate plot number maana tayari vilikua vilishapimwa. Ila nahisi mchakato utawahi sababu wilaya ya ubungo kitengo Cha ardhi wamepiga kambi pale kimara stopover wameweka kama clinic ya ardhi kusaidia kuharakisha michakato yote ya mambo ardhi wilaya ya ubungo. Ila nishatenga kama 1.5 pembeni kuhakikisha napata hati maana viwanja vimeungana viwili
Unanitisha mkuu...jamaa wa kampuni ya upimaji nilimpa 150k kuweka mawe na kweli kaweka. Saiz nimempa 900k akimbize file tupate plot number na michakato mingine kupata hati..atazingua yeye au watu wa wizara?Itkuchukua hata miaka 10
Wengi matapeli
Wakishachukua hela yako utaisoma namba
Jerry ashughulikie kwanza Maafisa ardhi ,wapima ardhi na mipangomiji matapeli ,ndo ataimudu hii wizara
Wengi matapeli,hawakai ofisini na kazi hawafanyi na ndio waanzilishi wa migogoro ya Ardhi
Afumue wizara,aanze upya
Tena wanawatumia hao wanaojitolea,wasio na check namba kufanya huo upuuzi.