Kupauka kwa bati. Je, Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu?

Kupauka kwa bati. Je, Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu?

PVA ni rangi maalum kwaajili ya paa tu,hata ukienda dukani utaona maandishi ya PVA kwenye ndoo.
Namna ya kuipaka inategemeana na bajeti Yako,Kuna watu wanatumia brush,mifagio ya kudekia yenye tambi nyingi halafu wenye uwezo wanachukua mashine ya kuspray.
Ok mkuu hapo nimekusoma,Asante sana
 
Kweli tumetofautiana vipato, ww unawaza kupaka rangi bati zako wakati sisi tunahangaika kupata msosi walau mlo mmoja na hela ya kodi.
No mkuu kila mtu na kipaumbele chake,mimi ni mwoga wa maisha
 
Kweli tumetofautiana vipato, ww unawaza kupaka rangi bati zako wakati sisi tunahangaika kupata msosi walau mlo mmoja na hela ya kodi.
"Hatufanani kama alama za vidole na bado naziamini falsafa za mwenda pole". Professor jay katika wimbo wa "Ni hayo Tu"​
 
Hakuna bati lisilopauka acheni kudanganya watu hapa,ingawa yapo makampuni yanaweka rangi zinazokaa kidogo,nimeshudia bati la ALAF ndani ya miaka 11 limepauka na limeanza kutengeneza kutu mwishoni kabisa maji yanakomwagikia,jamaa sasa hivi kapiga rangi nyingine ili kuresque the situation...
 
Mleta mada naamini umepata ushauri wa kutosha...
 
Jibu kwa adabu.Usiwe unadhani unajibishana na wehu wa mitaani kila muda.Nadhani umeelewa.
Mpuuzi wewe adabu ipi Mimi nimeanzisha thread unaleta mapuuza yako hapa ukitaka kila mtu kumjua mwenzie utajikimbia hapa Jf Kama unajiona mtu mkubwa weka namba yako hapa nitakupigia alafu tupimane vifua Ila najua huniwezi Wala kunifikia bado mtoto tu
 
Angalia sasa ulivyo na utoto.Ngoja nikuache na utotoutoto wako upake kucha zako rangi.
 
PVA ni rangi maalum kwaajili ya paa tu,hata ukienda dukani utaona maandishi ya PVA kwenye ndoo.
Namna ya kuipaka inategemeana na bajeti Yako,Kuna watu wanatumia brush,mifagio ya kudekia yenye tambi nyingi halafu wenye uwezo wanachukua mashine ya kuspray.
Brush inaacha vialama vya mistari kwa mbali hasa ukimpata fundi asiekuwa mzoefu, ufagio wa kudekia kidogo unafanya kazi nzuri ila changamoto yake atatumia rangi nyingi sana, kuspray ndo mpango mzima rangi kidogo kazi nzuri ila inategemea na aina ya paa lake kama ni yale ya usukumani paa limepanda sana juu ataua mafundi
 
Angalia sasa ulivyo na utoto.Ngoja nikuache na utotoutoto wako upake kucha zako rangi.
Utoto unao wewe ambaye unataka heshima kwenye thread ya mtu Kama huna Cha kuchangia tulia ndg maana mimi nimeomba ushauri wewe unakuja na dharau zako za kishamba Mimi sipo hivyo,JF tunaheshimiana sote tu Great thinkers so heshimu wazo la mtu.
 
Mpauko sio kesi, kama ww sio mtu wa kujali vitu vidogo, muhimu mvua haipigi ndani, sio kesi kabisa.
Sio kesi wapi ? umeambiwa hatua ya kwanza ni kupauka kinachofuata ni bati kupata kutu na mwisho ni kutoboka kwa sababu ya kutu.
 
Sio kesi wapi ? umeambiwa hatua ya kwanza ni kupauka kinachofuata ni bati kupata kutu na mwisho ni kutoboka kwa sababu ya kutu.
Hiyo kutu mpaka itoboke sio leo wala kesho.

Kisha nikajibu, ikishatoboka ndio nitaweka nyingine na nitakuwa nimejifunza, safari ijayo sintofanya kosa lile lile.
 
Pale liliingia neno silo: - "kupajua." Daah! Unajua auto-correction tena.

Meant kupauka.

Bati original ndizo sote tunataka. Hakuna anayetaka fake. Sote tuna tatizo kama lako.

Sote tunaugulia maumivu makali na bidhaa fake yakiwamo mabati hayo. Kuwa bila kupenda tumeingizwa mkenge!

Keamba TBS na hasa serikali tunaowalipa kodi kumbe majukumu yao yalikuwa nini?

ni washenzi tu, hawana muda wa kufuatilia hivyo vitu feki.
 
Back
Top Bottom