Kupauka kwa bati. Je, Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu?

Kupauka kwa bati. Je, Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu?

Hakuna bati lisilopauka acheni kudanganya watu hapa,ingawa yapo makampuni yanaweka rangi zinazokaa kidogo,nimeshudia bati la ALAF ndani ya miaka 11 limepauka na limeanza kutengeneza kutu mwishoni kabisa maji yanakomwagikia,jamaa sasa hivi kapiga rangi nyingine ili kuresque the situation...
Miaka 6 hadi 11 muda mrefu sana.
Hayo fake ya mchina bei rahisi mwaka tu yanaanza kupauka kwa mikoa ya pwani.
 
Screenshot 2024-11-26 104030.png
Ukifanikiwa kupaka hii kitu kwenye bati lako utasahau hicho kitu kinaitwa kutu kwenye bati au kupauka,hata wale wenzangu na mimi tunaonaunua yale mabati ya bei rahisi weka hii kitu utakuja kunishukuru...
 
Tangu ujenge unatusumbua sana.Yapake rangi za kucha.
NB:Unapoishi hakuna mafundi/wataalamu uwaombe ushauri?
ww akili zako zimeganda..kwani humu hakuna mafundi na wataalamu wa ujenzi wa kumpa ushauri na zaidi humu kuna wenye nyumba walipata changamoto kama ya mleta mada kwa bati za nyumba zao zilipauka basi nao wanaweza toa ushauri wa kiuzoefu njia gani walitumia kurudisha rangi halisi za bati zao zilizokuwa zimepauka na sasa bati zinang'aa na wamesaidia wengi sana.. ww tuliza kipago na endelea kujifungia ndani ya box
 
Mi mwenyewe leo naenda kununua bati ila kila nikisoma maoni ya watu najiona kabisa ndani ya miaka 5 naenda kuungana nao kuimba wimbo mmoja.

Kwa maono ya wadau Alaf pekee ndio wameonekana kuwa serious, the rest ni risk.
 
Hatari sana ,wafanyaboashara wanabambikia wateja tena wanawauzia kwa bei sawa na hizo ambazo hazipauki.
Na vitu vyenyewe sio vya elfu 2,

Bati pekee yake unaweza kununua za milioni 2 na kitu, hapo bado mbao, bado ufundi.
 
Sio kesi wapi ? umeambiwa hatua ya kwanza ni kupauka kinachofuata ni bati kupata kutu na mwisho ni kutoboka kwa sababu ya kutu.

Na huu ndugu mleta mada makaveli10 itabidi atambue kuwa huo ndiyo ulio ukweli mchungu:

"Kupauka -> kutu -> kutoboka; wala asidhani ni muda mrefu."

Bila rangi:

3Fe + 2O₂ = FeO • Fe₂O₃.

Na huyo ndiye kutu mwenyewe.

Kwamba kama hatakuwa amechukua hatua za kurejesha rangi hiyo sasa, miaka 5 ijayo kutu itakuwa imeshamhusu.

Mitano mingine baada ya hapo, asishangae kujikuta uelekeo wa aliye chini ya mwembe!
 
Na vitu vyenyewe sio vya elfu 2,

Bati pekee yake unaweza kununua za milioni 2 na kitu, hapo bado mbao, bado ufundi.
Duuh bati za milioni mbili mbona ni kuezeka chumba na sebule? Bati za kupima wanauza mita 1 hadi elfu 16....Na nyumba zina range kati ya mita 250 hadi 400.
 
Duuh bati za milioni mbili mbona ni kuezeka chumba na sebule? Bati za kupima wanauza mita 1 hadi elfu 16....Na nyumba zina range kati ya mita 250 hadi 400.
Inategemea na bati za aina gani na za thamani gani, kwa hizi bati zeti za 22k mpaka 25k maana yake hapo unapata bati 100 mpaka 120 ni bati nyingi, hizi unaezekea nyumba ya vyumba vi4 kama upauaji wako hauna mbwembwe nyingi,
Mie jengo lilikuwa kubwa na bado bati 110 hivi zikatosha.
 
Bati 110 means ni mita 330 hizo.
 
Naam nashukuru Sana kwa comments zenu wadau zimenijenga
umepiga rangi gani mkuu blue,kijani,kijivu au damu yamzee..ninamaana yangu kuuliza hivi mzee ,kuna muda binafs naamini kuwa bati za rangi nyekundu hazipauki kiasi chakuchosha macho ukilinganisha na rangi blue,au kijan
 
Mi mwenyewe leo naenda kununua bati ila kila nikisoma maoni ya watu najiona kabisa ndani ya miaka 5 naenda kuungana nao kuimba wimbo mmoja.

Kwa maono ya wadau Alaf pekee ndio wameonekana kuwa serious, the rest ni risk.
Alaf kuna famba pia!! Wachina wasengelema ya mwanzaa
 
Alaf kuna famba pia!! Wachina wasengelema ya mwanzaa
Basi leo ndio nilikuwa nachukua

Mwanzo nilijua option nyingi ni bora lakini option nyingi ndio zimeniongezea kunichanganya.

Nimechukua hivyo hivyo potelea mbali.
 
Back
Top Bottom