Kupelekwa mortuary kwa mtu hai, ni kosa la daktari

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuamua na kutamka mtu kafa ni kazi ya daktari, daktari anafundishwa namna ya kumtambua mtu aliyekufa. Ili daktari aweze ku declare kuwa mtu amekufa kuna mchakato na mlolongo mrefu wa matukio na vipimo kwa mgonjwa kabla ya mtu kupelekwa mortuary kama mfu. Hahati nzuri mortuary zetu nyingi Tanzania ziko hospitari na ni sehemu ya hospitali husika, hakuna anayepaswa kuingizwa mortuary bila kuonwa na daktari kwanza ku certify death ya mgonjwa.

Kila aliyekwenda kufufukia, kukoholea, kupigia chafya au kuongelea mortuary alikopelekwa kama mfu achukue hatua za kisheria kwa hospitali husika. Bila shaka hospitali itamtafuta mtu aliyeidhinisha kifo chake au cha mtu wake huyo. Kuna haja pia ya kuangalia na kukagua vyuo vyetu vya utaktari kuona kama vina sifa za kutoa wahitimu sahihi.
 
Na huenda hawa watu wanaofanyiwa operation wengi wanapelekwa mochwari wakiwa hai
 
Hii kitu inatokea duniani, kuna watu wanasikia sauti wanafikiri majini kumbe ni mtu yupo hai anaishia kufa kwa mengine kwenye jeneza.
 
Kweli. Kuna jirani yangu mmoja huko nyanda za juu kusini anaitwamama fulani, alikutwa na mauti feki. Wakiwa katika harakati za kumsafisha marehemu ghafla bin vupuu akaamka. Hakuna aliebaki zaidi ya wanawe, waombolezaji wote walitoka mbio. Huyo mama hadi leo hii yupo hai na tukio lilitokea miaka mitano iliyopita.
 
kweli yaan sijui ikija kukukuta umefufuka na upo kabulini itakuwaje
 
Nimesikia kesi nyingi za kiivi na sijaona aliyefungwa

Dr hawa tuombe tuuu ILA kuua watu kwa uzembe Ni wengi saana
 
VIPIMO KM KIPI MKUU?
aaah kaka hufahamu vipimo anavyostahili mgonjwa kuthibitisha kuwa amekufa? uganga gani huu jamani. Ngoja nikukumbushe basi hapa. Pima/chukua mapigo ya moyo (yapo hayapo) kwa kutumia hicho mnachotundika shingoni mwenu kwa kutafuta ujiko, pima pulse rate (zipo hazipo?) kwa kutumia vidole vyako juu ya mshipa mkubwa wa damu wa artery, chest movements (anahema hahemi?) kwa kutumia macho yako, mboni za macho (pupils) reaction to light kwa kutumia mwanga tu wa tochi., Je mboni ziko widely dilated or constricted, je zinabehave vipi ukizimulika na tochi. Usifanye haraka kusema kafa kama hazipo, rudia tena baada ya nusu saa hivi bado hazipo?. Kaka upo, hivyo sio vipimo? be serious with your work. Lupango tu nyie tumechoka kuonewa na vihiyo!!! kama umelewa viroba huwezi kusikia wala kuona kitu hata kama ukichukua hizi vital signs za mgonjwa, utakimbilia kafa, na vile umeambiwa ni panya road!!
 
Nimesikia kesi nyingi za kiivi na sijaona aliyefungwa

Dr hawa tuombe tuuu ILA kuua watu kwa uzembe Ni wengi saana
Uzembe wa wananchi kutohoji sababu za vifo (causes of death) za wagonjwa wao zinawafanya madaktari na wauguzi kufanya uzembe mwingi saaana kwa wagonjwa. Ndugu akiambiwa mgonjwa wako kafa utamsikia inalilah...., mungu kampenda za...., mungu katoa..... na kutoa kamasi kwa kulia, hana muda wa kuhoji ndugu yake kafakafaje? nini kilishindikana? nini kilikosekana? nani hakufanya nini? kipi kingefanyika? n.k
 
Acha mbwembwe,, ingekuwa rahis hivyo,, wote icu wangeenda motury
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…