kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kuamua na kutamka mtu kafa ni kazi ya daktari, daktari anafundishwa namna ya kumtambua mtu aliyekufa. Ili daktari aweze ku declare kuwa mtu amekufa kuna mchakato na mlolongo mrefu wa matukio na vipimo kwa mgonjwa kabla ya mtu kupelekwa mortuary kama mfu. Hahati nzuri mortuary zetu nyingi Tanzania ziko hospitari na ni sehemu ya hospitali husika, hakuna anayepaswa kuingizwa mortuary bila kuonwa na daktari kwanza ku certify death ya mgonjwa.
Kila aliyekwenda kufufukia, kukoholea, kupigia chafya au kuongelea mortuary alikopelekwa kama mfu achukue hatua za kisheria kwa hospitali husika. Bila shaka hospitali itamtafuta mtu aliyeidhinisha kifo chake au cha mtu wake huyo. Kuna haja pia ya kuangalia na kukagua vyuo vyetu vya utaktari kuona kama vina sifa za kutoa wahitimu sahihi.