Kupenda timu 2 ligi moja

Wadau hivi inawezekana mtu akashabikia timu 2 ligi moja mfano pale uingereza uwe unashabikia Liverpool mda huo huo unashabikia arsenal hivi hii kitu inawezekana kweli
Ipo sana tu. Kupenda timu fulani mtu anakuwa na sababu zake. Nina rafiki mmoja yeye alikuwa anaipenda 5imba (kisa utani wa jadi na Yanga) na Ndanda FC (ya nyumbani kwao). Siku moja zilikuwa zinacheza pale Nangwanda Sijaona Mtwara. Alifika na jezi zote mbili hadi geti, lakini mwisho hakuingia uwanjani.
 
Kwa Hilo sawa sababu kibongobongo tuna timu zetu za nyumbani je mtu wa bongo upende tim Duh noma
 
inawezekana kama uliipenda timu A kwajili ya mchezaji then akaamia timu B, kama mashabiki wa ronaldo na messi wanaaenda nao kokote watakapo hamia, ila kama ni mfatiliaji mzuri wa mpira na kila mechi unaangalia, huwezi kushabikia timu mbili kubwa kwenye ligi moja, lazima kuna moja, labda kinachotokea ni ushabiki kwenye mechi moja moja, labda Man u vs Liverpool utakuta shabiki wa Arseno ataishangilia liver
 
Sawa sawa
 
Me Newcastle na man u

Yanga na singida na namungo
 
1. Arsenal the Gunners
2. Man City because of Pep Guardiola
 
Binafsi naipenda timu moja tu kwakila ligi. Kupenda timu mbili au zaidi kwa ligi moja ni sawa na Kutokujiamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…