Kupenda timu 2 ligi moja

Kupenda timu 2 ligi moja

Mimi ni mshabiki wa Yanga ila Yanga inapokuwa inacheza na vitimu vidogo vinavyopeleka moto kama ihefu na Kagera sugar huwa nafurahi sana.
 
Wadau hivi inawezekana mtu akashabikia timu 2 ligi moja mfano pale uingereza uwe unashabikia Liverpool mda huo huo unashabikia arsenal hivi hii kitu inawezekana kweli
Mimi Hispania napenda zaidi Barca kisha Atletico Madrid. Uingereza napenda zaidi Arsenal kisha Man City.

Hapa Bongo Dar es Salaam napenda Simba Sports Club kisha Young African Sports Club
 
Kwa huh ushabiki wenu usio na michango yoyote hata ukiamua shabikia timu zote zinazoshiriki hakuna wa kukuuliza
 
Ndio inawezekana kushabikia timu 2 kwa wakati mmoja. Kiongozi wetu ni Mwigulu.
 
Wadau hivi inawezekana mtu akashabikia timu 2 ligi moja mfano pale uingereza uwe unashabikia Liverpool mda huo huo unashabikia arsenal hivi hii kitu inawezekana kweli
Inawezekana mfano umekaa na mfadhili ambaye ni shabiki lialia, (kindaki ndaki),na mfukoni huna Hela utashibikia upande upi?
 
Wadau hivi inawezekana mtu akashabikia timu 2 ligi moja mfano pale uingereza uwe unashabikia Liverpool mda huo huo unashabikia arsenal hivi hii kitu inawezekana kweli
Mimi napenda Simba na Yanga.
Yanga naipenda wakati wote iwe mvua liwe jua.
Simba nitaishibikia ikicheza na timu za nje. Ila hata wakifungwa napo poa tu.
 
Huwezi kua mshabiki wa timu mbili kwenye ligi moja labda uwe sio mtu wa mpira, ushabiki kwenye ligi ni wa timu moja tu ila unaweza kuvutiwa na timu mojawapo nyingine kwa sababu tofautitofauti lakini huwi mshabiki. Ushabiki ni pale timu husika inakupa maumivu au furaha kwa matokeo yake kutoka moyoni kabisa
 
Back
Top Bottom