Kupiga Honi ovyo au maeneo ya Shule, Mahakamani na Hospitali ni kosa kisheria

Kupiga Honi ovyo au maeneo ya Shule, Mahakamani na Hospitali ni kosa kisheria

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Dereva anatakiwa kutumia honi tu iwapo ni lazima katika kuwaonya watumiaji wengine wa barabara au kuwajulisha kuwa kuna gari nyingie ipo karibu nao.

Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 Kifungu cha 39 (3) Sura ya 168 inawakataza Madereva kutumia Honi katika #Kusalimia, Kuonesha hisia zozote au kumueleza dereva aliye mbele kuharakisha na kuongeza mwendo.

Dereva haruhusiwi kutumia Honi nje ya Hospitali, Mahakamani, maeneo ya Shule na katikati ya miji kuanzia saa 5 usiku na saa 12. Pia, hairuhusiwi kupiga Honi ndani ya Hifadhi za Taifa na Mbuga za
Wanyama.
 
Ukiwa Mtwara mjini inakubidi uzoee kelele za honi za bodaboda kwani wanazipiga muda wote kuitia wateja. Ni kero kubwa sana ambayo sijaiona katika mji mwingine wowote hapa nchini.

Nadhani hata askari Traffic wanaona ni jambo la kawaida kwa sababu hawawakanyi wala kuwachukulia hatua.
 
Wenzetu Norway honi hazipigwi pigwi ovyo,labda itoke emergency
Kwa bongo sasa kila saa pipiiii pipiiii
Pipiiii piipiiii
Alafu unakutana na honi za eiacher
Sikio+kichwa lazima kistuke

Ova
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kuna hizi honi za sasa zinazofungwa kwenye bajaji, yaani zinastua utadhani bus liko nyuma yako.
 
Nimepata kusikia Jaji Eusebia Munuo akiwa Hakimu Arusha alimzingua mmewe (Nicholas Munuo) baada ya kupiga honi ndani ya viunga vya Mahakama alipokuja kumchukua kwa gari.
 
Sasa hii sheria iliyotungwa mwaka 1973 wakati huo magari ni mia tano nchi nzima ndio itumike hata sasa kweli?!
 
Sasa hii sheria iliyotungwa mwaka 1973 wakati huo magari ni mia tano nchi nzima ndio itumike hata sasa kweli?!
Swali zuri
Sheria zetu nyingi zinahitaji mabadiliko
Kwa mfano kuna Sheria nyingine za miaka hiyo zilitoa adhabu ya faini shilingi mia tano..mpaka leo ukisoma bado ziko hivyohivyo
 
Back
Top Bottom