Kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania, kutokupiga kura pia ni haki ya kila Mtanzania aliyeamua hivyo. Tusibembelezane

Kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania, kutokupiga kura pia ni haki ya kila Mtanzania aliyeamua hivyo. Tusibembelezane

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Binafsi nitatumia haki yangu kutokupiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.
Kuna watu hata sura moja ya katiba ya JMT hawajawahi kuisoma lakini wanakwenda kupiga kura, safi wanatumia haki yao, Mimi katiba karibu yote nimeisoma nimeamua kukaa nyumbani au kwenda kazini siku ya Uchaguzi. Mkanichagulie viongozi, niko tayari kutawaliwa na hao mtakaowachagua.

Binafsi naona hizi chaguzi ni kama kuwaridhisha wahisani tu, nothing more. Mimi maishani mwangu siwezi kufanya jambo la kumridhisha mwanadamu mwenzangu.

Pia soma:LGE2024 - Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?
 
Kwa CCM hii?
Cc:- speech ya Nape, na wale viongozi wengine kuhusu wao kushinda.
Walithibitisha, hata mfanye nini, CCM Lazima ishinde.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Mkuu sahivi CCM inalazimisha wanaccm wote wajiandikishe na wapige kura, hivyo bila kupiga kura CCM itatwaa mitaa yote, lengo la CCM ni usipige kura bora mpige kura wengi waone aibu kuiba kumbuka mfumo wetu ni wakijinga sn hata wakipiga wawili wakachagua basi anakuwa mshindi. Twendeni tukapige kura
 
Ukipiga wewe inatosha mkuu, kwenye fursa za ulaji hatupeani Ila kwenye kura tupeane aisee safari hii mtatusamehe kaka.
Sipo kwenye system wala CCM, mi napenda mageuzi nisiposhiriki kuyatafuta nitaendelea kuongozwa na hawa wajinga na mafisadi wa CCM, kumbuka lengo la CCM ni usipige kura ndiyo furaha yao maana Mwenyekiti anaweza kuchaguliwa hata na watu 5 tu akatangazwa, nadhani tubadili mindset zetu. CCM wapo serious na uchaguzi huu wa serikali za mitaa
 
Mkuu sahivi CCM inalazimisha wanaccm wote wajiandikishe na wapige kura, hivyo bila kupiga kura CCM itatwaa mitaa yote, lengo la CCM ni usipige kura bora mpige kura wengi waone aibu kuiba kumbuka mfumo wetu ni wakijinga sn hata wakipiga wawili wakachagua basi anakuwa mshindi. Twendeni tukapige kura
Ni lini CCM ilikuwa na aibu?
Umesahau ya 2019 na 2023 bila shaka
 
Sipo kwenye system wala CCM, mi napenda mageuzi nisiposhiriki kuyatafuta nitaendelea kuongozwa na hawa wajinga na mafisadi wa CCM, kumbuka lengo la CCM ni usipige kura ndiyo furaha yao maana Mwenyekiti anaweza kuchaguliwa hata na watu 5 tu akatangazwa, nadhani tubadili mindset zetu. CCM wapo serious na uchaguzi huu wa serikali za mitaa
Kwahiyo 2015 Lowasa alishindwa kwasababu wana CCM walipiga kura kwa wingi?
2020 majimbo yote upinzani chali , CCM hawana aibu.
 
Ni lini CCM ilikuwa na aibu?
Umesahau ya 2019 na 2023 bila shaka
Sasa lazima tushiriki kuzuia, akina Nyerere wangekata tamaa kama wewe huende Tz ingepata uhuru 1980 lakini walipambana bila kukata tamaa na kuna wakati alishitakiwa akalipa faini ya elf 3 ni kama milioni 300 ya sasa, akina Lisu wamepigwa risasi 36, Mbowe kafungwa kwa uonevu Lema alikimbia familia, kwenye mapambano hakuna kukata tamaa unakatia tamaa kizazi chako.
 
Back
Top Bottom