Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

KWA UFUPI, KESI ZOTE TUNAZOSHINDWA SASA NA KUPELEKEA KUPOTEZA FEDHA KWA KULIPISHWA FAINI ZA MAMILIONI YA WALIPA KODI ZIMETOKANA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.
Upo sahihi kabisa.

Ni mpaka pale uchaguzi 2025 utakapofanyika, ndipo tutajua awamu inayofuata imefanya nini.

Mpaka hapa tulipofikia, ni vijiti tu vilivyobadilika(wamerithi). Awamu ni ya Tano..

Awamu ni ile ile iliyochaguliwa 2020!
 
Hayo yoteee uliyoyataja ndiyo walioshika mpini wanayataka yaendeleee kuwepo ili wafurahie.waliobaki ni wala makombo tuuu harafu wanajigeuza kujiita chawa. 2025 tuanze na wabunge robo tatu , au hata nusu kwa nusu , tuone kama hatutapiga hatua kwenda kanani.
 
Upo sahihi kabisa.

Ni mpaka pale uchaguzi 2025 utakapofanyika, ndipo tutajua awamu inayofuata imefanya nini.

Mpaka hapa tulipofikia, ni vijiti tu vilivyobadilika(wamerithi). Awamu ni ya Tano..

Awamu ni ile ile iliyochaguliwa 2020!
Awamu ya sita hoyeee. Kubalini matokeo kwambaaa, bibi phd ni failure leader.
 
CCM oyee,chama cha upinzani cha kuitoa CCM madarakani bado hakipo. Najiuliza CCM hii inayolea ufisadi kama huu wa kuingia kuvunja mikataba hovyo kisha wananchi tunabeba mzigo wa madeni,ina kitu gani kinacho iwezesha kuhodhi madaraka?

CCM bila nguvu ya dola (polisi) ingekuwa kama chama cha congres India,inaumiza wananchi . Viongozi wanatanguliza maslahi ya chama chao kwanza kabla ya maslahi ya taifa .
 
Watu wapuuzi, wajinga na waovu hutumia mwavuli wa chama na serikali kwa sababu ya fikra zetu za kutoa lawama za jumla namna hii.
Waovu na wahalifu wengi hutumia fursa hii kama kichaka cha kujificha na humo humo hupata fursa zaidi na kusababisha hasara zaidi kwa taifa.
Waovu na wahalifu hao wakiungisha nguvu zao katika kichaka hicho ni vigumu kuwadhibiti na mbaya zaidi wao ndiyo hudhibiti taifa kwa ujumla wake.
Sasa, ni muhimu kujenga utamaduni wa kupambana na mmoja mmoja kwa msalaba wake mwenyewe.
Kwa njia hiyo, wengi watafikiria sawa sawa na kutoa maamuzi yenye tija kwa umakini zaidi kwa kuogopa madhara yatokanayo.
 
Kama Kuna sheria inazuia mashauri yote kusikilizwa Nje ya nchi. Inakuwaje haya malipo yanafanyika? Au hiyo sheria ilifutwa baada ya mabadiliko ya awamu?
====
Naomba ufafanuzi, Mkuu wangu kwenye mambo haya.
Nina imani, Mheshimiwa Pascal Mayalla unafanyia kazi ya kuleta majibu ya Maswali haya.

Asante
 
Kipande hicho hakina maana yoyote zaidi ya kuwa hapo umegeuka kamusi tu ya Kiswahili kufafanuwa ujinga na upubavu kwa mtazamo wako.

Halafu unatujulisha tatiao ambalo tunalo kabla hatujapata uhuru, ujinga, Nyerere, katika kutupumbaza, aliliweka katika mambo aliyobuni yeye kuwa ni kundi la maadui zetu, sina sababu ya kurudia kwa sasa.

Binafsi naaminiujinga kuwa ni adui pekee tuliyenaye.

Upumbavu haujalishi kama u mjinga au hu mjinga, unaweza kuwa mpumbavu.

Hilo la upumbavu siyo tatizo letu hata kidogo, tatizo letu ni ujinga.

Sitaki kujikita sana kwenye hilo, bali naamini tu wajinga.

Post yangu ijayo itaendelea kuchambuwa hoja zako Ingine.
 
Hapo umejipumbaza tu, lakini ukweli ni kuwa umekuja kusomesha siyo kuelimisha. Kwa kipande hicho tu cha maandiko yako, nimefahamu na nna uhakika hauelewi tofauti ya kusomesha na kuelimisha.

Naona umekuja kutowa maoni yako kwa mtazamo wako, hilo halimaanishi kuwa wewe umeelimika zaidi ya unaowapa maoni yako mpaka ufikie kuwaelimisha. Wenye kuelimika ndiyo husema elimu hiyo kawapa nani lakini siyo wenye kuelimisha. Unaweza kuwa na elimu kubwa sana na ukajihisi unaelimisha kumbe huelimishi bali unajaza watu ujinga tu.

Nakaribisha mahojiano kwenye hilo ambapo sijaeleweka, sitaki kupumbaza mtu.
 
Kesi hii haikuendeshwa Kivukoni au Kisutu. Kwa kiingereza kile ulidhani mwanasheria gani wa Tanzania atakubali kwenda mahakamani? Hiyo miezi miwili pia ilikuwa mingi walitamani wapewe hukumu hata mahakamani wasiende.
Hawa wanasheria wetu wanatuonea sisi hapa nakesi zetu za kupigiana simu. Huko kwa watu hawathubutu hata kusema "objection".
 
CCM kwa deal za kuiba hawawezekani. Usishangae kuta wao ndio wamemshawishi muwekezaji akafungue kesi wagawane pesa. CCM wakikosa wa kumuibia wanajiibia wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…