Wanabodi,
Swali kuu la msingi ni jee Tanzania, can we stand by mabadiliko haya ya sheria zetu kwa kukata mirija ya wanyonyaji?. Jee do we have the guts to stand by the laws kwa mabadiliko haya?. Isije ikawa tunashangilia sasa, kisha tunakuja kugeuziwa kibao kwenye mengine yote ili kushikishwa adabu na mabeberu hawa na mwisho wake tunakuja kujutishwa na mabeberu kwa vilio na kusaga meno?. Nani anakijua kilichomkuta Patrice Lumumba wa Congo kwasababu ya utajiri wa Almasi?. Nani anakumbuka kuhusu blood Diamonds za Angola?. Nani anakijua kilicho muondoa Saddam Hussein Iraq, au Muammar Gaddafi Libya?. Linapokuja suala la mabeberu kulinda interests zao, mabeberu sio watu kabisa ni ma beasts kabisa, hivyo tusipojiangalia, tutakuja kushangaa, mtu wetu anaondoshwa mzima mzima na tunabaki tukishangaa na tusiamini!.
Ushauri wa The Best Way Forward ni Renegotiation to Reach A Win Win Situation
Kupitisha sheria mpya kwa hati ya dharura bila ushirikishwa ni kosa, maadam tumeisha fanya kosa, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Hivyo huu ni ushauri wangu wa the best way forward kwa situation iliyopo ni kukaa mezani na wawekezaji wote tuliosaini nao mikataba kabla ya sheria hii mpya kupitishwa, kuwapigia magoti, kuwaomba wakubali kupitia upya mikataba yao katika win win situation, sisi tupate na wao wapate, hii ya kulazimishana, nawaombeni sana msishangilie na kumvimbishwa kichwa rais Magufuli kuwa tunaweza kila kitu, tuwalazimishe lazime wafuate, asiyetaka na afungashe, aondoke!, jee tunaweza?, tunayo jeuri hii?. Kuna watu kama Billy Gates au Dangote, akikohoa tuu, nchi zinatetemeka!, can we stand?.
Kitakacho Tokea
Kitakacho tokea ni ama baadhi ya vipengele vya sheria hii mpya vitapuuzwa, ama ili kuepuka aibu ya kupitisha sheria mbovu kwa mbwembwe, serikali itapeleka kimya kimya, marekebisho ya baadhi ya vipengele vya sheria hii, kikiwepo hicho kipengele cha arbitration, kitaondolewa ili kurejesha confidence kwa wawekezaji. Kwenye hili, time will tell, kama Nyerere na Sokoine walikuwa ni wakali ukweli ukweli, lakini walishindwa, hivyo kwenye hili la sheria kutekelezwa kwa retroactively, naowaomba mimi niwe mkweli bayana wa nafsi yangu, Mwalimu wangu Prof. Kabudi na wanasheria wake, waliotunga sheria hii kwa mtindo wa zimamoto, wamemdanganya rais Magufuli kwa kumtungia sheria yenye vipengele vya ajabu, halafu rais aka asent, then sheria hii itashindwa kutekelezwa, hivyo soon watapeleka marekebisho Bungeni na kumrudia rais a accent marekebisho hayo, na hili likitokea, naombeni hoja za bandiko hili zizingatiwe, Tanzania tutaonekana ni nchi ya ajabu, tunatunga sheria za ajabu kwa mbwembwe, tunazipitisha kwa mbwembwe, rais wetu ana zi asent kwa mbwembwe, lakini katika utekelezaji ndipo tunajikuta kumbe Bunge letu, na serikali yetu, iliyosheheni wanasheria manguli tena wengine ni waalimu wetu wa sheria wa chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam ambao sisi tulipokuwa wanafunzi tukisomea sheria, waalimu hawa ndio waliotufundisha kuwa sheria yoyote inayotungwa kama ita act retroactively is a bad law, it's illegal, lakini leo, waalimu hawa hawa ndio wamegeuka wanasiasa na wao sasa ndio hawa wametunga illegal law, wakaipitisha, wakampelekea rais akaisaini ianze kutumika, huku wanajua fika retroactively law is illegal law kwenye jumuiya ya Madola, lakini bado wamepitisha, sasa siku ya kurejea Bungeni kuyarekebisha haya madudu yao ya kisheria, hizi sura zao wataziweka wapi?.
Paskali