Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka

Kwa hiyo waliuza kwa sababu ya hilo saga?
 
The it is the responsibility and reliability of the company to employ unethical employee and to let the company easily manipulated.

Hapa hakuna kukwepa lawama Shekhe.

Kwa mtindo huu Tigo au Milcom wamechafuka kibiashara popote watakapo tia mguu duniani.
 
Kwa hiyo waliuza kwa sababu ya hilo saga?
Ndo maana yake walishaona mbele nini kinaweza kuwakuta.

Kumbuka kesi ipo London na Makao makuu ya Millcom/Tigo yapo London. Jiongeze.

Tukio la 2017 kesi ipo mahakaman toka 2019 na Millcom kamuuzia Rostam Tigo 2022
 
Mambo hayafanyiki kwa mihemko kama unavuodhani!
Kwa hiyo yafanyike hayo kisa Lisu alifanyiwa hiyo!
Who is Lisu mpaka tigo ifanyiwe hivyo?
Juzi hapa maandamano umeona kilichotokea?
Kwanini mlitaka kumuua?
Kwanini mlitumia policcm kuyadhibiti ?
 
Kama ni tushauriane ni mawasiliano yapi yatakuwa salama kwetu maana hatupo salama kwa namna hii ya tunaotumia mawasiliano yao kutuuza kwa watu wabaya.
 
Tuko nyuma sana kwa technology. Wametupita kwa kila kitu . Mzungu anatuchungulia mpaka ndani ya mapafu, acha vyumbani. Simu ni zao, satellite ni zao, hata savers ni zao, mimi siwabishii.
Asiyejua atakubishia
 
Sahihi kabisa
 
Kama ni tushauriane ni mawasiliano yapi yatakuwa salama kwetu maana hatupo salama kwa namna hii ya tunaotumia mawasiliano yao kutuuza kwa watu wabaya.
Tupa laini tupa simu tumia njia ya barua kupitia kwa mtu kwenda kwa mtu ukiweza nenda mwenyewe ukamfuate usipige simu usitembee na simu haupo salama
 
Tigo Tanzania ilivujisha data za simu za Lissu kwa serikali ya Tanzania kabla hajapigwa risasi September 7, 2017. Mahakama ya Uingereza imeanza kusikiliza kesi.

Michael Clifford alikuwa mfanyakazi wa Tigo Tanzania ameiambia mahakama huko Uingereza kuwa aliachishwa kazi na kampuni ya Tigo Tanzania ambayo ipo chini ya Millicom kwa sababu alionyesha kutoridhishwa na Tigo kuvujisha taarifa za mawasiliaon ya Lissu.

Tigo ilivujisha mawasiliano ya Lissu na location yake kuanzia August 22, 2017. Tarehe 29 mwezi huo huo Tigo iliendelea kuvujisha location na mawasiliano ya Lissu kwa serikali muda wote (24/7) na kwa kasi hadi siku anashambuliwa Dodoma.

Clifford ni mpelelezi/ mchunguzi wa ndani wa mitandao ya mawasiliano wa Tigo.

Tigo haijakataa kubujisha mawasiliano na location ya Lissu kama ilivyo daiwa na Clifford.

Clifford alianza kufanya uchunguzi siku tano baada ya Lissu kushambuliwa, hii ni baada ya kusikia kwenye conference call kuwa Millicom illikuwa inatoa data za Lissu kwa serikali ya Tanzania bila idhini yake. Baadaye akakabidhi majibu ya uchunguzi kwa maboss wake.

Millicom ilikuwa inapeleka data za Lissu kupitia WhatsApp na baadaye kuwaambia wa-delete kila kitu kwenye WhatsApp.

So, Clifford anasema alifukuzwa kazi na Tigo kwa kuonewa kwa sababu ya kufichua mpango mbaya wa Tigo kuvujisha taarifa za Lissu kwa serikali ya Tanzania na kushambuliwa kwa Lissu.

Imechukua miaka minne hadi kesi hii kuanza kusikilizwa (trial) kwa sababu Kulikuwa na jitihada nyingi za kutaka isikilizwe sirini (restriction).
 
Sasa Tigo ni ya Rostam, huyo huyo anapambania favours kwenye makampuni yake mbele ya serikalii, hapo taarifa lazima zimwagike tu
 
Kwahiyo Clifford anatuambia kuwa kampuni ya TIGO ni kampuni ya KIGAIDI?

LISSU anaenda kuwa billionaire katika hii kesi.
 
Aibu kwao sasa.....tutende mema,ubaya unamwisho kufichika
 
Uzuri Mheshimiwa mwenyewe aliyenusurika kuuwawa alishawahi kuwataja wabaya wake kupitia mahojiano aliyofanyiwa na vyombo vya habari. Na kupitia huu ushahidi, ni wazi wahusika ni wale wale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…